Nimeamua sasa kuachana na ualimu na kwenda kusoma

Wewe jamaa umemaliza kila kitu na inaonekana kigoma unaijua vizuri mno, huku kati ya watu 100, 99 wanaamini kuhusu mambo ya uchawi na 98 wanaufanya kabisa either kujikinga au kuroga, wasiofanya wengi ni watu wa kuja (watumishi)..

Kigoma ni ngumu kuwekeza kwanza kwa uchache wa watu, Kuna soko la mitumba seremala ukipita hata mchana hamna movement yoyote ya watu, ni kama kijiwe cha kwenda kukutana, masanga stand mpya napo hakuna biasahara, sasa najiuliza je niteketeze Millon 15 na Mimi nipate sifa Nina biashara ambayo haitanipa faida?.....niliwaza mpaka nifungue nafaka niwe creative kwa kutengeneza vipeperushi nivisambaze mji mzima, lakini nikaona kwa kigoma hii ukiwa wa utofauti lazima wakupoteze tu, ndio maaana nikapata wazo la kusoma kwanza, miaka 3 sio mingi, inaweza kua ni njia ya kuchomoka kwenda taasisi zingine.
 
Navyoelewa kwenye utumishi wa uma unapewa ruhusa ya kwenda kusoma iwapo utaongezea kwenye taaluma yako mfano hiyo Ualimu. Lakini ukiaga unaenda kusoma IT hawakupi ruhusa na hata wakigundua watafuta likizo yako ya kimasomo na kusimamisha mshahara.

Either uache kabsa au ufake lakini ruhusa hutapewa.

I stand to be corrected.
 
Shida ya gendo ni lazima ulisimamie mwenyewe hadi mzigo unafika salama, magendo yanataka muda wako sana kusimamia show mpaka mwisho......yeye ni mtumishi, muda ataupata?
 
Ndio hivyo mkuu umesema ukweli, na ukirudi ukawapa cheti cha IT Wala hawakusumbui wanakubadilishia muundo chaap, ndio maana nimeamua kusoma open tu.
 
Mbona una hasira na maamuzi yangu mzee? Wewe umemalizana na ya kwako na ndugu zako mpumbavu kabisa.
Mzee ni mtu gani ,mpumbavu ni mtu gani na umejuaje mi ni mzee na nina hasira,umejuaje mi yangu nimemaliza au ndo kama kawaida unaongea kutokana na akili yako shallow ya ualimu?Kutangatanga kimaamuzi ilihali una milioni 15 unadhihirisha ufinyu wako wa akili kama ilivyo kwa walimu wenzio. Kuna maeneo mengi sana hiyo milioni 15 unaiweka na baada ya muda kadhaa unakuawa na financial freedom.
 
Tafuta biashara ufanye achana na elimu umri unaenda
Unadhani kigoma kufanya biashara ni rahisi mkuu? Kwenye biashara niko smart nafahamu biashara mno lakini kwa kigoma nimegonga mwamba, nimrjaribu kuhama huu mkoa hata kwa kuhonga lakini mambo yamekua magumu.
 
Umeona kwanini nimekuita mpumbavu? Nilijua akili yako itapotaka kwenda na ungeweza kunijibu vizuri bila kutanguliza kuongea matusi hapa.

Nikwambie kitu kimoja, nilipata mkopo wa hazina million 20 nikapata kiwanja sehemu nzuri plus saving zangu nilizokua nazo nikanunua kiwanja million 7 hapo mwanza, hela niliobakiza ni million 15, haziniathiri chochote maana baada ya makato naweza kuishi na salary iliyobaki vizuri tu, kwa hiyo hizo hela naweza weka UTT au bank na nisiathirike kwa chochote, mkuu kuhusu biashara naifahamu sana nimeifanya na juzi hapa likizo nilikua daresalam kukutana na wadau niliokua nafanya nao harakati hapo karume, nimeenda Moshi,Arusha watu wanapambana mtaani na mtaji usiozidi million 5 na wanapata faida nzuri tu, hata mimi ningekuepo hiyo mikoa ningefanya kwa ukubwa wake.

Mimi hapa nazungumzia kigoma na fursa zilizopo kigoma, unajua nimeshafanya harakati ngapi hapa? Nimeleta dagaa wa kwanza kuuza sehemu wanapaita kibirizi, nimefungua nguo za mitumba then nikaanza kufungua viatu, unajua kwanini nimeachana navyo?

Kwa hiyo usijifanye huko smart sana kuhusu elimu ya mtaa, wazo langu la kwenda kusoma naiona fursa upande huo pia hata nikienda kusoma sitoigusa hiyo million 15 na biashara naweza kufanya muda wowote wakati wowote.
 
Rudia tena kusoma mkuu.
Soma hiyo 15milioni utarudi tu.


Ila naona kila RAIS ANAYEINGIA MADARAKANI anaendelea kuufanya ualimu kama laana akati watoto wananufaishwa na kufahamishwa na walimu wetu.

Ukiangalia mgogoro ni posho tu. Wangekuwa na posho basi manenonyote yangekwisha.

Mbali na mishahara yao wapewe posho jamani.

Kwamfano


Mshahara wake ubaki vilevile ya kufundishia kusimama nk ibaki 750,000 kwa mwezi wamuwekee na posho hizi
1. Posho ya nauli. Labda 80,000
2. Posho ya nyumba tufanye 60,000
3. Posho ya maasiliano 30,000
4. Mazingira ya kazi 25,000
5. Mavazi 38,000
6. Vifaa vya kazi 21,000
7. Majukumu mengine 10,000.

Kanakoongezeka ni 236,000

750,000 + 236,000 atapata 1,036,000

Wenye mishahara ya 900,000
900,000 + 236,000

Wenye mishahara ya 1,100,000

1,100,000+ 236,000

Nakadhalika nakadhalika

Hiyo inakuwa posho ya jumla kama wanavyopata posho wakurugenz wakuu wa idara nakadhalika nakadhalika


Hutamsikia mtu kwenda kusoma.wala kukimbia chaki

Wala walimu wakuu kuvutana na walimu wao.
 
Shukurani mkuu, kwasababu nasoma open naweza soma huku najipanga nifanye nini, miaka 3 sio mingi.
Sasa mzee umekopa halafu hiyo million 15 unaifungia ndani utarejesha riba Gani maana hizo sio pesa zako binafsi ni za bank
 
Sasa mzee umekopa halafu hiyo million 15 unaifungia ndani utarejesha riba Gani maana hizo sio pesa zako binafsi ni za bank
Wanakata mshahara mkuu, sema inabidi niwekeze maana baada ya miaka 5 itakua tena siyo million 15 thamani ya pesa ya kibongo inashuka kwa speed
 
Kasome hadi PhD, achana na hawa wachuuzi wadikudanganye.

Hivi unaweza kumwambia Dr.Mwigulu aache uwaziri akafanye biashara, basi Mshaurini Zitto Kabwe asigombee ubunge, au Mshaurini Msukuma Kasheku afanye biashara aache ubunge.

Jamani kila mtu ana maono yake, na kwa Tanzania Elimu bado inalipa sana hamuwezi jua anaweza soma akapata nafasi mpya akapiga mpunga mrefu kama wanavyotuibia waliopo, na akawa katusua.

Kasome usidanganywe biashara ni side gig kwa nchi hii na wengi mitaji wanaipata huko maofisini kwetu hawakopi bank.
 
Asante sana neno la hekima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…