Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Kwanza trailer ya film hii ilinidanganya nikajua tumepata bonge la filamu. Baada ya kuona filamu yenyewe naweza kusema haijaitendea haki Tanzania wala inaweza isizae matunda yale tunayoyatarajia. Zaidi naweza kusema uwekezaji uliotumika ulikosa malengo sahihi yenye kuweza kuleta tija kwa sekta ya utalii Tanzania. Kwa lugha nyingine, filamu ilikuwa haina focus.

Baada ya kusema hayo, haya ni baadhi ya mapungufu niliyoyaona:

1. Kwanza ni suala la Producer wa ile documentary kumsema Rais Magufuli mwanzoni kabisa mwa filamu hii kuhusu misimamo yake kuhusu Covid-19 na baadae kidogo Rais Samia kukubaliana na Producer huyu. Mimi nilikuwa nampinga Magufuli kwa vingi ila katika issue kama hii haijakaa sawa kabisa. Mada ya utalii unaingiza habari za Covid-19 kweli? Tujifunze kwa Wamarekani, hauwezi kuongelea siasa zao au Rais wao, hata katika private conversation wakakuacha hivi hivi. Kama alikuwa anataka kuongelea historia ya Tanzania si afadhali wangemuongelea hata Mwalimu Nyerere na historia ya Tanzania katika kupigania uhuru wa nchi mbalimbali? Hii filamu kama tumeweka pesa zetu, sisi si ndiyo tungesema tunataka nini kiwepo nini kisiwemo?

2. Mara kwa mara katika documentary ile, Rais Samia alikuwa anajigamba 'mimi si ndiyo Rais'. Najua alikuwa anasema hivyo kama utani fulani ila angekuwa na washauri, hasa wanaojua mentality ya raia wa nchi kama Marekani tunazotaka waje kutalii, hayo majigambo hayatapokelewa vizuri kabisa.

3. Kila mada ya utalii iliyokuwa inaongelewa, focus ilikuwa sana kwenye mapungufu ya utalii wa Tanzania. Mfano, walipokuwa wanaongelea Mlima Kilimanjaro, wakaanza kuongelea snow yake inayokaribia kuisha. Walipoongelea tembo, focus kabisa ikahama ikawa kuhusu ujangili hadi Samia akampeleka mwenyeji wake katika ghala zinapohifadhiwa pembe za ndovu. Hata walipoongelea Tanzanite, wakagusia kuwa na yenyewe inaenda kwisha. Hii ilitakiwa iwe 'feel good film' ya kuvutia watalii wajue mazuri ya Tanzania siyo masuala ya uanaharakati au mapungufu yetu. Mambo hayo yangetafutiwa njia nyingine ya kuyaongelea (na kwanza tayari yanajulikana na yameongelewa sana). Kwanza siamini mpaka leo kuwa Tanzania na majeshi yetu yote tumeshindwa kukabiliana na ujangili mpaka tuombe mataifa mengine watusaidie.

Kwa haraka haraka nimeona nigusie hayo. Kukiwa na ziada nitaongezea.
 
Kwa mtu alieyetoka na kuishi kwenye nchi za mabeberu, hii filamu ni upuuzi mtupu...
Lakini mwacheni Mama yetu...
Anaupiga mwingi kama tunavyotaka ......kushinda Mwendazake...
 
Kwani wakitumia gharama zao ndio fedha haitumiki?.
Hiyo bilioni 7 ndio fedha iliyotumika kuandaa hiyo filamu.
P
Ikulu kuna biashara gani? Kwa sauti ya Mzee alie timiza kumbu ya miaka [emoji817] ya kuzaliwa wiki iliyopita. (R.I.P)

Ktk hii filamu sijaskia sehemu wizara ya utalii, bodi ya utalii au hata bunge la Tanzania likitajwa kuhusika na biashara hii. Nashawishika kuamini ni biashara ya kijanja iliyohusisha IKULU yetu kwa kujua au kutokujua.
 
Su-gang on move...!huu ni wakati wa wengine kubalini tu kwa kweli,"mtapata tabu sana"
FILAMU NI NZURI NA INAVUTIA SANA PIA NI FAHARI KWA TANZANIA.
IMETENGENEZWA KWA PLAN YA KUDUMU KIUBORA KWA VIZAZI NA VIZAZI.
Mi mwenyewe naungana na sukuma gang kudeal viroboto wote wa bi kiroboto nawaomba wazalendo wote mliopewa jina la sukuma gang tusiache kuwapelekea moto hawa vibwengo
 
Jiwe alimuamin mwanamke haraka kisa ni mweupe akaona itakua ni burudani akiwa karibu yake sasa mwanamke huyo huyo kanunuliwa ndo kawa chanzo cha maangamizi yake
Hata Samson aliuzwa na delila
Hahahaha kama anasinzia kumbe anaona
 
Mi mwenyewe naungana na sukuma gang kudeal viroboto wote wa bi kiroboto nawaomba wazalendo wote mliopewa jina la sukuma gang tusiache kuwapelekea moto hawa vibwengo
Kubalini bana mkae tu pembeni na sisi tule bana,nyie si mlikula kibabe,dhulma,ujambazi,kupora,kutweza watu.
#SSH_2040.
 
Nimebahatika kuangalia filamu ya Royal Tour.

Mimi binafsi haijanivutia, na hata watoto wangu wamesema hawajaona jambo jipya.

Filamu imeonyesha mlima Kilimanjaro, Zanzibar, Ngorongoro, Serengeti, na hifadhi ya pembe za ndovu / nyara za taifa.

Sasa maeneo hayo yameshaonyeshwa katika filamu nyingi zinazotangaza utalii wa Tanzania. Nilitegemea filamu pamoja na kuonyesha vivutio vinavyojulikana, ingetambulisha maeneo mapya ya vivutio vyetu vya utalii.

Pia usimuliaji wa Rais Samia haukuwa wa viwango vya kuridhisha. Inawezekana filamu imeharakishwa kutolewa. Kuna baadhi yenu mtakereka sana na filamu hiyo. Naomba nisisema jambo hilo kwa sasa hivi.

NB:
Nadhani tunaweza kuandaa filamu nzuri zaidi ya kutangaza utalii wetu. Wadau wa utalii wakae pamoja na kujifunza kutokana na mapungufu ya Royal Tour Tanzania.

cc Nguruvi3, Pascal Mayalla, Chige, Kichuguu, Kilatha, Phillipo Bukililo, Statesman
Maeneo mapya ya utalii kama yapi ambayo ulitegemea kuyaona na hukuyaona? Hiyo filamu inachukua muda gani mwanzo hadi mwisho...? Je, filamu haina zuri hata moja?🙏🙏🙏
 
Nimebahatika kuangalia filamu ya Royal Tour.

Mimi binafsi haijanivutia, na hata watoto wangu wamesema hawajaona jambo jipya.

Filamu imeonyesha mlima Kilimanjaro, Zanzibar, Ngorongoro, Serengeti, na hifadhi ya pembe za ndovu / nyara za taifa.

Sasa maeneo hayo yameshaonyeshwa katika filamu nyingi zinazotangaza utalii wa Tanzania. Nilitegemea filamu pamoja na kuonyesha vivutio vinavyojulikana, ingetambulisha maeneo mapya ya vivutio vyetu vya utalii.

Pia usimuliaji wa Rais Samia haukuwa wa viwango vya kuridhisha. Inawezekana filamu imeharakishwa kutolewa. Kuna baadhi yenu mtakereka sana na filamu hiyo. Naomba nisisema jambo hilo kwa sasa hivi.

NB:
Nadhani tunaweza kuandaa filamu nzuri zaidi ya kutangaza utalii wetu. Wadau wa utalii wakae pamoja na kujifunza kutokana na mapungufu ya Royal Tour Tanzania.

cc Nguruvi3, Pascal Mayalla, Chige, Kichuguu, Kilatha, Phillipo Bukililo, Statesman
Time duration Ni saa / dakika ngapi
 
Nyani haoni kundule, "hiko" ndiyo nini? Kiswahili gani? Bora ungetumia kilugha chako ( your vernacular)

Yaani Kiswahili balaa tuu, kwa wenzetu utasikia OLD IS GOLD, huku kwetu eti NYANI HAONI KUNDULE.
 
Kama walitumia gharama zao ile bilioni 7 imetumika maeneo gani?
We unafikiri filamu Hollywood Kama bongo movie!!!...mnalipana 30 elf kwa siku!!?...Angelina Jolie kwenye salt alilipwa dola 30m,kwenye the tourist 10m,director na wasaidizi wengine watalipwa ngapi!?
 
Back
Top Bottom