Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Baba anajitolea kulinda Taifa, anafukuzwa kazi nakurejea Uraini. Anatafuta kazi yakumwezesha kulisha familia, Kwa kuwa hakufanikiwa kusoma sana na kwa kuzingatia ugumu wa Maisha uliopo na hili asiibe anaamua kuwa mlinzi anayelipwa ujira mdogo lengo alishe familia na kuepuka kuwa mwalifu. Anakamatwa kwa sababu tu amejitolea kumlinda mwanasiasa ambaye Kwetu tunaamini misimamo yake na ujenzi wake chama ni hatari kwa usalama wa Chama cha Mapinduzi.
Anatokea mkristo/ muislam anayekwenda kwenye nyumba za ibada kila siku ya ibada anaelekeza walio chini yake wamkamate wamtese na kumfungulia kesi ya ugaidi. Wanafanya walivyoelekezwa na waliotumwa kufanya unyama huu wanajitokeza adharani mbele ya Jaji kueleza walivyoshiriki, wanaambiwa mnadanganya na uongo wenu ni huu na huu then Jaji anasema awakudanganya. Hawa wote Wana watoto, wanajua kuna kifo, Wana kuna kupoteza madaraka lakini wanafanya haya Kwa sababu wao Wana nguvu kuliko MUNGU
Mtoto mdogo anayepaswa kusoma anashuhudia baba yake mzazi akiwa jela bila hatia kisa anatafuta ada, anafika Hadi mahakamani kujionea ukweli wa kinachoendelea Kwa baba yake. Viongozi wale walioshiriki kutengeneza njama wanaona haya yote na pia viongozi wa Dini wanayaona haya lakini hakuna anayekemea wala kutoka kwenda Kwa watesi wa watanzania Hawa na kuwakumbusha madhara na kiburi cha madaraka.
Wao waliopata nafasi ya kuongozi wanapeana nafasi ikiwezekana familia zao kila mwanafamilia awe na sehemu yakutawala na wanarudi nyumbani usiku wanakaa na familia zao kumwomba MUNGU awalinde. Kila section wanatamani kuombewa na Kila hatua wanatamani MUNGU awalinde ila wanasau namna madaraka kwao yalivyowapa upofu.
Mambo haya yanaumiza sana, yanasikitisha, yanatia simanzi na kutufanya tujiulize ni nani anayepandikiza roho hii ya kikatili miyoyoni mwetu? Ni kwanini tumejaliwa viongozi wa jinsia zote wasio na huruma hata kwa watoto? Hii ni kesi Moja, wapo wangapi ambao watoto na familia zimesambaratika Kwa kuwekwa mahabusu au kufungwa bila hatia? Wapo wangapi wenye Madaraka wametesa na may be kuua lakini awajafikishwa kwenye haki badala yake wanateuliwa kila kukicha?
HUYU Binti ambaye picha yake inasambaa mitandaoni yawezekana ni Malaika anatuonyesha watawala wana roho gani, lakini labda ni walkup call Kwa watawala Kwamba mnapopambana na watu wazima mnatesa watoto. Viumbe hawa hawakuzaliwa kuteseka, Wana haki ya kuishi na kupata elimu. Hakuna Mtoto wetu anayeweza kusoma huku akijua baba yupo mahabusu kwa kesi za kisiasa. Fanyeni MENGINE yote lakini haya mateso kwa watoto wadogo yanaweza kutuletea dhoruba huko tuendako.
Mwenyenzi My zijaalie familia zinazopita mateso bila haki zi tamaa, wape Moyo Mkuu.