Nimeangalia picha ya binti wa Mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya inayosambaa, Watanzania tukubali tuna viongozi katili wasio na utu

Nimeangalia picha ya binti wa Mtuhumiwa Mohamed Ling'wenya inayosambaa, Watanzania tukubali tuna viongozi katili wasio na utu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Baba anajitolea kulinda Taifa, anafukuzwa kazi nakurejea Uraini. Anatafuta kazi yakumwezesha kulisha familia, Kwa kuwa hakufanikiwa kusoma sana na kwa kuzingatia ugumu wa Maisha uliopo na hili asiibe anaamua kuwa mlinzi anayelipwa ujira mdogo lengo alishe familia na kuepuka kuwa mwalifu. Anakamatwa kwa sababu tu amejitolea kumlinda mwanasiasa ambaye Kwetu tunaamini misimamo yake na ujenzi wake chama ni hatari kwa usalama wa Chama cha Mapinduzi.

Anatokea mkristo/ muislam anayekwenda kwenye nyumba za ibada kila siku ya ibada anaelekeza walio chini yake wamkamate wamtese na kumfungulia kesi ya ugaidi. Wanafanya walivyoelekezwa na waliotumwa kufanya unyama huu wanajitokeza adharani mbele ya Jaji kueleza walivyoshiriki, wanaambiwa mnadanganya na uongo wenu ni huu na huu then Jaji anasema awakudanganya. Hawa wote Wana watoto, wanajua kuna kifo, Wana kuna kupoteza madaraka lakini wanafanya haya Kwa sababu wao Wana nguvu kuliko MUNGU

Mtoto mdogo anayepaswa kusoma anashuhudia baba yake mzazi akiwa jela bila hatia kisa anatafuta ada, anafika Hadi mahakamani kujionea ukweli wa kinachoendelea Kwa baba yake. Viongozi wale walioshiriki kutengeneza njama wanaona haya yote na pia viongozi wa Dini wanayaona haya lakini hakuna anayekemea wala kutoka kwenda Kwa watesi wa watanzania Hawa na kuwakumbusha madhara na kiburi cha madaraka.

Wao waliopata nafasi ya kuongozi wanapeana nafasi ikiwezekana familia zao kila mwanafamilia awe na sehemu yakutawala na wanarudi nyumbani usiku wanakaa na familia zao kumwomba MUNGU awalinde. Kila section wanatamani kuombewa na Kila hatua wanatamani MUNGU awalinde ila wanasau namna madaraka kwao yalivyowapa upofu.

Mambo haya yanaumiza sana, yanasikitisha, yanatia simanzi na kutufanya tujiulize ni nani anayepandikiza roho hii ya kikatili miyoyoni mwetu? Ni kwanini tumejaliwa viongozi wa jinsia zote wasio na huruma hata kwa watoto? Hii ni kesi Moja, wapo wangapi ambao watoto na familia zimesambaratika Kwa kuwekwa mahabusu au kufungwa bila hatia? Wapo wangapi wenye Madaraka wametesa na may be kuua lakini awajafikishwa kwenye haki badala yake wanateuliwa kila kukicha?

HUYU Binti ambaye picha yake inasambaa mitandaoni yawezekana ni Malaika anatuonyesha watawala wana roho gani, lakini labda ni walkup call Kwa watawala Kwamba mnapopambana na watu wazima mnatesa watoto. Viumbe hawa hawakuzaliwa kuteseka, Wana haki ya kuishi na kupata elimu. Hakuna Mtoto wetu anayeweza kusoma huku akijua baba yupo mahabusu kwa kesi za kisiasa. Fanyeni MENGINE yote lakini haya mateso kwa watoto wadogo yanaweza kutuletea dhoruba huko tuendako.

Mwenyenzi My zijaalie familia zinazopita mateso bila haki zi tamaa, wape Moyo Mkuu.
 
Hata somalia alshabab ilianza hivi hivi huku baadhi ya viongozi wa dini wakilitetea kundi hilo kuwa linasimamia misingi ya dini na sheria za kiisilam, leo hii kundi hilo limekuwa hatari sio tu kwa Somalia pekee bali kwa ukanda wote wa East Africa na dunia kwa ujumla. Tukija Msumbiji pia lile kundi la kigaidi lilianza hivi hivi mdogo mdogo huku baadhi ya viongozi wa serikali wakilipuuza kuwa ni kundi dogo tu lisilo na madhara hata kwa kata au wilaya moja ya mkoa wao. Lkn sasa hivi serikali inapambana kulitokomeza inashindikana hadi wamefikia hatua ya kuomba msaada nje wa kijeshi nk.

Kwahiyo mleta mada unaweza kuwa umeshavuta mpunga ili uje utetee unachotetea bila kujali athari inayoweza kutokea kwa taifa endapo watu wa aina ya unaowatetea watapata mwanya wa kufanya yale yanayofanyika kongo, msumbiji, somalia nk. Lkn serikali haiwezi ruhusu ujinga wa aina hiyo utokee kwenye ardhi yake kwa sababu ya kuogopa propaganda kama hizi za mleta mada. Moyo wa mtu msitu, hata Osama mwanzo mwanzo wengi hawakujua kuwa ni gaidi, ila apofanya aliyofanya ndo wengi wakaaza kuamini kuwa jamaa alikuwa ni mtu wa aina gani. Tanzania ya sasa kila kitu kinachukuliwa kisiasa, hata yale yanayohusu usalama wa nchi na wananchi kwa ujumla.
 
Haya mambo yanasikitisha, wao wanaendeleza dynasty kwenye utawala wa nchi na kufurahia kufanya ukandamizaji, madaraka ni yao lakini Mungu ni wetu sote..........
 
Ila Hangaya anajitafutia uadui usiokua na ulazima.
Hata Hangaya akitoka madarakani usitegemee hao watu wataachwa hivi hivi.

Dola ni shetani kamili.

Ukitafuta LEAGUE na Dola pambana kivyako.

Usianze kulia lia kutafuta huruma kwa watu wakati ulikuwa unajitafutia ugali wako.
 
Kwa sababu anawanyoosha sukuma gang hamna tatizo.
 
Baba anajitolea kulinda Taifa, anafukuzwa kazi nakurejea Uraini. Anatafuta kazi yakumwezesha kulisha familia, Kwa kuwa hakufanikiwa kusoma sana na kwa kuzingatia ugumu wa Maisha uliopo na hili asiibe anaamua kuwa mlinzi anayelipwa ujira mdogo lengo alishe familia na kuepuka kuwa mwalifu.
Ukishapata kuberi jitahidi handasi ipungue kisha uje kusoma upya hii post yako nanuofanyie maboresho au uiondoe
 
Back
Top Bottom