Kwa kweli kupata "A" ya physics miaka mitano nyuma elikua sio rahisi kwa mtihani wa Nect, hata Kenya na Uneb kule uganda haikua rahisi lakini leo Necta ina A za physics zaidi ya 500 nchi nzima, tena hapo hapo na "F" zikawa zipo nyingi, kuna logic gani? Mimi siamini upangaji wa matokeo wa Necta wana mfumo wa kuchangua shule ipi iongozePhysics ni ngumu ila ufaulu kama huo japo hiyo ni shule tunayoiamini kuwa ni shule bora, lazima kutakuwa na walakini. Physics imerahisishwa sana siku hizi. Sijui ubora wake bado ni ule ule.
Mwaka 2013, kulikuwa na C pekee ambayo ilikuwa marks kubwa kitaifa. Hiyo ndio ilikuwa Physics kwenye uhalisia wake.