Nimeangalia takwimu za matokeo kidato cha sita, somo la physics hali ni tete. Shida iko wapi?

Kwa kweli kupata "A" ya physics miaka mitano nyuma elikua sio rahisi kwa mtihani wa Nect, hata Kenya na Uneb kule uganda haikua rahisi lakini leo Necta ina A za physics zaidi ya 500 nchi nzima, tena hapo hapo na "F" zikawa zipo nyingi, kuna logic gani? Mimi siamini upangaji wa matokeo wa Necta wana mfumo wa kuchangua shule ipi iongoze
 
Unajuaje mwaka huo labda mlikuwa vilaza wote labda huyo wa c.
Physics Ni tamu ukiielewa sema ukikariri utaumia
Ulipata ngapi Physics mkuu?

Mimi nilipata B, nilitumia mbinu zote nilizozibaini kujifunza, nikabahatika na hiyo marks
 
Katika masomo yote, naamini Physics A level ndio somo gumu kuliko yote.

Mambo yote mtu anasoma kwa miaka 4 O-level, yanarudi A-level tena kwa kwenda deeper zaidi, halafu kwa miezi kama 18 tu.

Mtu anayegonga A kwenye physics A-level, hakuna kitu kitamshinda kujifunza chini ya jua.
 
Somo la physics, somo la physics.

Je Tz hatuna waalimu wabobezi kwenye hili somo amaa ni somo gumu sana...
Physics ni somo ambalo halina waalimu wengi . Hili somo linahitaji kusomwa kwa nadharia na vitendo. Sijui katika kuangalia kwako shule kama Feza, Mariani Girls na zingine za binafsi ufaulu wao wa somo la Fizikia uko vipi- nategemea shule hizi zitakuwa na waalimu wengi, maabara na vitabu. Fizikia inahitaji uwekezaji katika kupata waalimu wanaolielewa vizuri na kufundisha kwa kujiamini.
 
Watoto wenu wote sahv wanataka wawe wakta mauno tu

Ova
 
Mimi mambo ya physical niliona niachane nayo, nimeamua sasa kuhamia spiritual!


YESU KRISTO NI BWANA NA MWOKOZI
 
Nimependa hapo mwishoni
 
Kufaulu physics inategemeana na shule unayosoma
 
Hilo somo hata walimu wake kwa advance huwa wanaruka ruka tu unakutana na swali la mechanics mda wenyewe wa mtihani masaaa matatu waongeze mda kwenye mtihani wa physics pia walete walimu walio serious
 
Pole mkuu. Daah nini kilifuata mkuu?
Eti mimi ndio nikawa naongoza physics japo nimepiga E 😂😂😂, na hata chuo, E ndio ilikuwa kali kabisa kwa physics kwa wadahiliwa wote wapya 😂😂😂; yaani physics, aagh
 
Uzuri ulishalisoma hilo somo.

Wewe unaona tatizo nini?

Una maoni gani juu ya hilo tatizo?
Physics ni SoMo rahis sn.tatizo hatuna walimu competent.wao wanafundisha kusolve maswali na sio kuumpa mwanafunzi knowledge.km mpo mliosoma mkwawa high school humu mliomaliza mwaka 2000 PGM AU PCM mkumbukeni yule mwl mzungu Mr ANDY.dah alikuwa anafundiaha knowledge.dah ANDY ANDY
 
Kwa sasa ingia youtube tu, utapata kila knowledge
 
Nakumbuka Kuna jamaa yangu alidisco chuo kwasababu ya courses za physics.

Okay physics inataka kichwa na sio kichwa Cha kitoto.
 
true
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…