Ramon Abbas
JF-Expert Member
- May 4, 2021
- 1,964
- 3,913
Kwa wadau wanao kopesha, huwa wanafanya 3,000 au 4,000 kwa kila 10,000 , Ila hii ni kwa mwezi mmoja, na sio kwa siku kama ilivyo wewe.Je nikipandisha kwa kila elfu 10 izae buku kila siku nitakosea?
Yaani hapo ulichofanya ni riba ya asimilia 100, kwa siku 20 za kazi katika mwezi, kwa mtu aliyechukua 10,000.Kwa kila shilingi elfu 10, irejeshe Sh 500 kila siku.
Asante sana mkuu kwa ushauri wakoKwa hatua za awali na pesa ndogondogo bado hakuna shida na uko salama..lakini jitahidi ujisajili na kupata nyaraka husika.. Ila riba itakuwa sio hiyo bali ile ya mwongozo wa bank kuu
Ukiendelea bila nyaraka kuna wajuzi watakopa ndefu na hawatarejesha na hutakuwa na cha kuwafanya kisheria labda uwaroge
Kuna mtu aliwahi kunishauri kwamba kama nakopesha basi niandikishane na mtu kwamba nilimsaidia sio nilimkopesha kwa sababu sina usajiliOmba usikopeshe wanasheria
Wahitaji ni wengi ifanye official uwe na kinga likitokea tatizoAsante sana mkuu kwa ushauri wako
Hii biashara kweli haina nyaraka na ni rahisi kutapelika ukikopesha watu wasiowaaminifu
mimi niliwahi kuifanya kipindi cha nyuma lakini sikuwa serious na ilidum kwa miezi miwili tu.
nilichokuja kugundua, hawa kina mama walioko kwenye vikundi ni wakopaji wazuri na wanaweka bondi vitu vyao vya thamani na ni warejeshaji wazuri sana
Pia nilikuwa nakopesha watu wenye makazi ya kudumu na wenye kipato/mshahara mwisho wa mwezi.
Kwa kifupi nilifanya vetting kali sana kwa watu niliokuwa nawakopesha
MBALI NA KUISAJILI, NINI CHA ZIADA NAWEZA FANYA ILI KUIFANYA HII KAZI IWE SALAMA ZAIDI?Wahitaji ni wengi ifanye official uwe na kinga likitokea tatizo
Marejesho yasiwe cash..kubali makato ya tozo kuliko kupokea tasilimu.. Watu sio wema
Simama sana Mungu lakini pia fanya featuring kidoogo[emoji23]MBALI NA KUISAJILI, NINI CHA ZIADA NAWEZA FANYA ILI KUIFANYA HII KAZI IWE SALAMA ZAIDI?
[emoji23][emoji23][emoji23]Simama sana Mungu lakini pia fanya featuring kidoogo[emoji23]
Hii nzuriKuna mtu aliwahi kunishauri kwamba kama nakopesha basi niandikishane na mtu kwamba nilimsaidia sio nilimkopesha kwa sababu sina usajili
mfano, kama nakopesha elfu 40, rejesho ni 28,000 jumla 68,000 in two weeks
basi tuandikishane kwamba nimekusaidia elfu 68,000 umpeleke mtoto hospitali kisha utazirudisha baada ya wiki 2[emoji28][emoji28][emoji28]
Hapo Hao Wanamtengeza Taratibu Ili Baadaye Wamtandike Cash NdefuAnza kupiga chuma tu mkuu.
[emoji23][emoji23][emoji23]Anza kupiga chuma tu mkuu.
Business ni risk taking mkuu.Unakabidhi mtaji wako kwa watu, subiri muda kidogo utajua hujui. Bora ufungue genge ufanye biashara za kawaida. Sikia kukopesha, Mkopaji anaweza akaingia mkatabata wowote unaomnyonya ili mradi tu aipate hiyo ela, akishaipata utasubiri.