Nimeanza Biashara ya Kukopesha, naomba ushauri

habari za asubuhi Jf people?

Mimi ni Dalali wa Viwanja Magari Nyumba & Co. Kuna pesa huwa naipata gjafla kutokana na shughuli zangu za u middle Nimeamua kuanza kukopesha.

watu ninaoanza nao ni waaminifu sana nawafahamu.

Kwa kuanza tu nimeamua kuwapa mkopo wa masharti haya

Kwa kila shilingi elfu 10, irejeshe Sh 500 kila siku.

Mkopo utakaa siku 14.

Jana nimetoa elfu 40, after two weeks ilete Riba ya Tshs 28,000

Je nipo sahihi au najiumiza kwa kiwango nilichoweka?

Je nikipandisha kwa kila elfu 10 izae buku kila siku nitakosea?

Note: mteja wangu ni mama ntilie
Sijui imani ipi inaruhusu riba. Kwa uoande wangu kitu asichokidhiria mola wako hakina faida kwako. Unaweza ukafaulu duniani na akhera ukawa mweny khasara. Fanya kazi isiyo na mushkel
 
Aisee kufa kufaana😅😅
Tunamsikilizia usione tumekaa kimya ukadhani hatua uchungu na 800K tunasubiri achoke zaidi tumshawishi jamaa aongeze bidii ya kumdai hala sisi wapambe utaenda kutoa offer kwa kupisha wakwanza anaenda na 350, wa pili anaongeza kidogo, wanne anakomaa watano anaenda na dau la chini kidogo,🙂🙂 hapo tunachocheaanayemda amkomalie. Lazima aachie

Watu wabaya nyie duh
 
Sijui imani ipi inaruhusu riba. Kwa uoande wangu kitu asichokidhiria mola wako hakina faida kwako. Unaweza ukafaulu duniani na akhera ukawa mweny khasara. Fanya kazi isiyo na mushkel
Hivi nchi za kiislam unauhakika hazikopeshi kwa Riba. Tanzania inadaiwa na Iran pesa ndefu kuliko china unadhani tunarudisha tulichochukua???
 
Sijui imani ipi inaruhusu riba. Kwa uoande wangu kitu asichokidhiria mola wako hakina faida kwako. Unaweza ukafaulu duniani na akhera ukawa mweny khasara. Fanya kazi isiyo na mushkel
Jamani ya kaisari mpeni kaisari

Mbona Bwana Yesu alishatolea ufafanuzi hili swala miaka buku 2 iliyopita?

au hukuwepo dada?😅
 
Hatuishi kwa kufwata nchi za kiislamu au waislamu tunaishi kwa kufwata quran na sunnah
Quran inaruhusu kuomba omba hela kwa wanaume kama sio waume zenu?

a.k.a vibomu na kudanga?
 
Sijaelewa unataka kuzungumzia nn maana havina uhusiano, aliekuomba pesa anajua kwa nn amekuomba and has nothing to deal with the quran
 
Dini ya Mungu kwa viumbe wake na haikua kwa ajili ya wasaudi na wa iran.
Sorry sipo ku argue na wewe just take what u belive na mimi nichukue ninachokiamini.
Wewe kama hutak mkopo kaa kmya dunia ishapotea hii hao wanaoshika dini ndio mtaan huku wanafanya mambo ya ajabu ata kwenye vitabu vya Mungu havipo, maduka ya kariakoo ukiwakuta utasema ni watu ila sasa vitu walivyoweka ndani sasa.
Watu wana shida wacha wakope na kupata pesa ngumu siwez nikakupa pesa yangu ukae nayo mwez et irud hivyo hvyo kama riba dhambi TAFUTA YAKO yakwangu iogope kama ukoma.
 
Wapi nimesema nataka pesa yako? Kama watu wameamua kufanya makosa haina maana kuacha kukumbushwa na zaidi hupaswi kufwata hao unaosema washika dini unatakiwa kufwata what your creator has allowed and prohibitted u to do.
seems like una stress za maisha. May Allah make easy every burden thts troubling you.
 
baby mama hebu njoo nikukopeshe hapa laki 1 urudishe 170,000 baada ya wiki 2😅😅
 
Mkuu mibiki mitali naomba uniongezee mtaji angalau laki 5 hivi nikuze biashara.

I know you can do this my friend.

Halafu uje inbox kuna ishu nataka nikupambanishe😅😅😅
 
HZO NI BIASHARA ZA UNYONYAJI MKUU,TAFUTA BIASHARA NYINGINE.MUNGU HAPENDI RIBA NA KAMA UKING'ANG'ANIA MUDA SI MREFU UTAKUJA KUJUTA MAJUTO MAZITO SANA.MWANZO UNAWEZA IKAKULIPA SANA ILA KUNA MAMBO YA AJABU KIUCHUMI UTAANZA KUYAONA MUDA SI MREFU UCHUMI WAKO UTABADILIKA GHAFLA NA UTAANZA KUONA MAUZA UZA HELA LUPOTEA,KUDHULUMIWA,NYUMBA KUUNGUA MOTO,MAUGONJWA YAN KILA ULICHOKIPATA KUPITIA HELA HIYO KITAYEYUKA NA UTAONEKANA KAMA CHIZI MTAANI JAPO WEWE MWENYEWE UTAJIONA MZIMA.
OGOPA SANA BIASHARA YENYE KITU NDANI YAKE KINACHOITWA RIBA/INTEREST utasaga meno na kufa hufi.

Nimeandika kwa herufi kubwa hifadhi haya maneno utakuja kuelewa vzr.
 
wenye mafanikio makubwa dunian hapa wote ni wanyonyaji na hatujaona punishment hapa labda tutegemee kwa Mungu.
Hao wakina mo, bakhresa, kwenye viwanda vyao wanalipa watu mpka 3000 kwa siku, wengine kutoa mshahara ni shida.
Matajiri wakubwa ata mikoan weng wanakopesha wakulima na wafanyabiashara wadogo kwa riba kubwa na wanazid tu kutoboa, swala ya kusema cjui malipo utayapata soon ndio ntakataa mpka coz hyo anaekuja hajalazmishwa amejipeleka mwenyewe.
 
Naona wadau wengine wamekuja kunitishia kabisaaa..

sasa biashara ya kukopesha ina uhusiano gani na nyumba kuungua ??😂😂😂😂

ukisikia kutishia nyau ndio huku
 
Back
Top Bottom