Nimeanza kuzalisha Cricket Insects kwa matumizi yangu tu

Nimeanza kuzalisha Cricket Insects kwa matumizi yangu tu

Tunako elekea mtafuga hadi Nzi
Watanzania tuna ujinga sana, kuna siku nilipeaa storie na dada mmoja wa UNDP kulikuwa na fundi ya kuzalisha wale Black soldier Fly larvae kwa ajili ya mifugo, sasa Watanzania hakuna alie taka, kila mmoja eti anaona kinyaaa kinyaaa.

Ikabidi Fund wapewe wazungu ndio wakaanzisha shamba kule Mkulanga wakajiita Biobuu, Jamaa walipewa Dollar Million 3, Biliob 6 plus, na hii ni baada ya Wabongo kukataaa.

Sasa kwa sasa ndio watu wameshituja na wanazalisha.

So ni swala la muda tu wait you will see
 
Kuna mghana kafungua mgahawa Paris ya wadudu tu na ana wateja kibao anatengeneza hela sana
Kweli ni kawaida sana

Kwa Africa tuna ile mentality ya kusema ni masikini tu ndio wanakula hiki na kile
Mkuu kuna Fund ilitoleaaga Tanzania kwa ajili ya wale Black Soldie Fly Watanzania tukawa hatutaki tunaona kinyaa, fund wakaja pewa Wazungu wakaanzisha shamba Mkulanga, wamepiga pesa balaaa fikiria walipeaa Dolla million 3, nilipewaga hii habari niliumia sana, na wazungu mbaya zaidi waliendelea pia kuwa suppoted hata baafa ya kupewa hizo Million 3 USD.

Watanzania wanapenda wabanane wote kwenye ishu moja na ni ile ya kufurahishana yaani mimi nifanya kile amnacho kitafurahisha wengi
 
Wanakelele hao wadudu balaa.
Wanalia kama filimbi, tumewachezea sana tukiwa wadogo. Ni wale wakubwa siyo mole cricket.
Shamba wapo wengi wakubwa sana kama dole gumba (thumb) au zaidi.
Hawalii wakati wote, usha wasikia mchana wanalia? sasa wanatengenezewa mazingira tu hutawasikia tena wakilia
 
Mkuu hawa nashindwa kuwatofautisha na wale wadudu waharibifu wa mimea pindi ikiwa michanga/teke, wana tabia ya kujificha chini kwenye madongo nyakati za asbh b4 jua kuchomoza ukiwashtua tu wanarukaruka kwa kusambaa!!
Nyakati za ujana wangu nilikuwa nawafakamia sana senene na kumbikumbi! lakini siku hizi baada ya kuota kitambi salaleeh nikila domo linajaa mate mepesi kama mang'ati aliyetafuna tumbaku na magadi...!! yaani lazima nirudishe chenji fasta!!
Ni tofauti kabisa hawa ni wanakula vitu kama majani, na wanaishi juu hawaishi kwenye mashimo
 
Hao wadogo waharibifu wa mimea michanga wanaitwa mole cricket. Wanakata miche michanga.
Sasa wapo wakubwa sana kama dole gumba hawana vurugu ni hao anaowasema mdau kama sikosei.
Senene sijawahi kula ila kumbikumbi hata sasa wakati naandika vijana wamekamata wengi usiku uliopita wanakaanga ni watamu balaa.
Siku chache zilizopita walikamata wa kujaa roba la 50kg, tumekula hadi kuwachoka tunawatupia samaki.
Cricket na kumbi kumbi radha ni sawa kabisa mkuu, hawatofautiani
 
Nazalisha kwa ajili yangu tu,ingawa najua pia kuna Wazungu, Wa asia wanakula sana hii but kwa sasa sio ya biashara kabisa.

Na sili kwamba ndio sili chakula kingine,
 
Back
Top Bottom