Uchaguzi 2020 Nimebadili maamuzi, wacha watuone wajinga tu ila na mimi kesho naenda Kupiga Kura

Nipo kituoni kwa sasa. Nimetoka Dar jana kuja Moshi kwa ajili ya kupiga kura.

Kwakweli sikuwahi kuwaza wala kuwa na mpango wa kupiga kura. Ila kwa mambo yanayoendelea kwenye nchi yangu, nimeamua kupiga kura mwaka huu, na nimesafiri kuja mkoa kwa kazi hii.

I don't care what they're gonna do with my vote, ILA NITAPIGA KURA NA NIPO KWENYE FOLENI SASA HIVI na ninaenda kumchagua Tundu Lissu
 
CCM must go halafu kura hupigi?
Zile kauli za "mafuta niwajazie mimi, mishahara niwalipe mimi, halafu umtangaze mpinzani" zinakatisha tamaa ya mabadiliko! Wafanyakazi wote wa tume kuteuliwa na mgombea na Rais aliyeko madarakani,

ukija kwenye sarakasi za wasimamizi wa huo uchaguzi hasa wale Wakurugenzi wa Halmashauri na ambao wengi wao ni makada watiifu na walioshindwa kwenye kura za maoni ndani ya chama mwaka 2015, polisi wetu kuegemea upande chama tawala, nk.

Vyote hivi vinafikirisha sana kuwa na ujasiri wa kupiga kura ndani ya utawala huu wa awamu ya tano. Anyway, nimehama makazi pia. Na sijaona kama ni sahihi kwangu kusafiri umbali mrefu, kurudi tena huko nilikotoka eti nikapige kura ambayo nina imani kabisa haitaheshimiwa.
 
Mtu anayetaka mabadiliko, anatakiwa kutimiza wajibu wake.

Wajibu wake mdogo kabisa, akishindwa kuandamana, akishindwa kubadili sheria na mfumo, ni kupiga kura.

Akikataa kupiga kura, kwa makusudi, huyo hana haki ya kulalamika. Yeye mwenyewe anakuwa ameusaidia mfumo uliopo.

Kuna tofauti kati ya mtu anayepiga kura halafu kura yake ikabadilishwa, na mtu ambaye hajapiga kura kabisa.

Angalau aliyepiga kura anampa mwizi wa kura kazi ya kuiba kura.

Asiyepiga kura anamsaidia mtawala dhalimu kuwandeleza udhalimu wake.
 
Wako WAP wale waliokua wanajazana kwenye mikutano
 
Ninasikia Devota anaweza akamstaafisha mtu siasa za bungeni hapo Moro mjini,vp kunaukweli gani
Ukweli upo wazi kabisa, ila kwa aina ya wasimamizi waliochaguliwa, namna watendaji kata walivyojipanga, jumlisha calmness ya watu Morogoro na aina ya mtu atakayetangaza matokeo! Bado safari yake itakuwa ngumu sana labda tu kwamba uhalisia utaonekana kwamba Kuna mtu kabebwa
 
Hii ni kura ya haki,utu na demokrasia dhidi ya uonevu na ukandamizaji......
 
Siku ya kuondoka magufuli madarakani, nitarudi kupiga kura. Au itokee mchakato wa Rasimu ya Katiba ya Wananchi ukarejeshwa na hivyo Nchi kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, mamlaka yaliyopitiliza ya Rais kupunguzwa, nk! nitarejea bwashee.

Huu ni msimamo wangu tu niliojiwekea baada tu ya uchaguzi mkuu wa 2015 na ambao nikishiriki kwa moyo mkunjufu kama ilivyokua kwa michakato mingine huko nyuma.
 
Mkuu naunga mkono hoja Mimi nimeenda kutokana na figisu zinazondelea nikajua kumbe Hawa na wepesi Sana na wanaogopa kwahiyo nime piga kura wakiiba sawa, wakiharibu sawa ila ukweli watakuwa nao nafsini mwao na ahuhuda wao atabaki kuwa Mungu
 
Huna
Huna madhala yoyote kwa sababu siku zote upo hapo ulipo na tayari kura yako ilishajesabika huko.
 
baada ya kupiga kura, tunakukaribisha kwenye sherehe za kuapishwa JPM jijini dodoma, maendeleo hayana chama.
 
Mie naenda kupiga kura. Urais nampigia Magufuru aendeleea kutuletea maendelea, Ubunge Devota Minja kazi kwisha.
 
Katiba iliyopo imekupa haki ya kupiga kura, umeshindwa kuitumia.

Unataka katiba mpya?

Wewe ni kama mtu aliyepewa hela kidogo.

Kashindwa kuzimaliza.

Lakini, anadai apewe hela nyingi zaidi!

Huna haki ya kudai hela zaidi ikiwa hata ndogo ulizopewa hujaweza kuzimaliza.
 
Hakuna wa kukuibia kura,piga upendavyo. Ruzuku ale nani?! Wakala atatumalizia posho bure, tukimaliza tunalalamika tumeibiwa kura kazi imeisha! Halafu bila aibu unasema ukabidhiwe Nchi wakati kituo kimoja cha kupiga kura kimekushinda! Tusifanye majaribio ya kuweka Nchi rehani. Chagua maendeleo au maneno!
 
Kwel umeamua mkuu hongera
 
mkuu, na mimi leo nimepiga kura kwa mara ya kwanza toka nizaliwe, miaka yote nilikua sioni umuhimu ila leo nimeamua pamoja na mazingira kuwa magumu ila nampa Lissu,


kama wataiba waibe, kama watavuruga wavuruge, ila nina imani Lissu kuna jambo atafanya, sikumpigia mrema 95, sikumpigia Lowassa 2015 pamoja na zile amsha amsha, ila this time nimeamua!
 
baada ya kupiga kura, tunakukaribisha kwenye sherehe za kuapishwa JPM jijini dodoma, maendeleo hayana chama.
Nafahamu, sina tatizo na hilo. Ninatatzo na ufikiriaji wa watu wa namna yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…