Nimechaguliwa kujiunga na AZANIA SECONDARY SCHOOL A-LEVEL 2023 wanaoijua mnisaidie hapa

Nimechaguliwa kujiunga na AZANIA SECONDARY SCHOOL A-LEVEL 2023 wanaoijua mnisaidie hapa

Kama kichwa cha uzi kinavyosema, mimi nimemaliza form four mwaka jana hivyo form five selections zimetoka na nimechaguliwa kwenda Azania sec

Hivyo najua humu kuna watu wanaishi hapo karibu au wamesomea pale naomba mnipe hali ya maisha ya pale,ufaulu wake, n.k

Natokea mikoani na itakuwa mara yangu ya kwanza kuishi dar

Combination nimechaguliwa kusoma PCM

Natanguliza shukurani
Karibuni wajibu


Funny boe
Mkuu hongera na karibu United Nations (hilo ndilo jina la barabara iliyopo shule ya Azania).

Barabara hiyo ina shule kubwa kama Jangwani Girls Secondary School ambayo inapakana na Aazania, mbele huko kuna Tambaza High School.

Shule ya Azania imekaa sehemu nzuri sana mjini, kwenda mjini kabisa Dar au Kariakoo unatebea tu, ipo karibu na hospitali ya Muhimbili.

Sina uhakika kuhusu habari za elimu kwa sasa, nimetoka mitaa hiyo siku nyingi, lakini utapata huduma zote muhimu karibu.
 
Hongera , lakin haujasema je wewe ni mwenyeji wa hapo hapo Dar es salaam au unatokea mkoa na shule ndyo umekuleta jijini ??... Kwanini nimekuuliza

1)kama umetokea mkoa kaaa uelewe Dar es salaam hamna shule ya bweni ya serikali namaanisha shule zote maarufu Dar kama
  • Azania
  • Tambaza
  • kabasila
  • chang'ombe
  • jangwani
  • Benjamini na nyingine nyingine wadau watanisaidia

Siyo shule za bweni , hivyo basi kuna hostel za watu binafsi ambazo huwapangisha wanafunzi kwa gharama fulani , mfano zipo ambazo kwa mwezi ni tsh 20000 mbaka 45000
Hizi za 20000/= moja zina kunguni wengii sanaa hili lazima nisa lakini pia siyo nzuri sana kwa mwanafunzi kujisomea kumbuka kwenye hizi hostel uhuru ni wakutosha unaweza hata usikanyage darasani mwezi mzima na hamna atakae kuuliza hapo msala utakuwa kati ya wewe na walimu wa shuleni kwenu

- kwasababu Azania ni boys sina tatizo ila ingekuwa chang'ombe au kibasila kule hapa ningekushauri ukasome sanaa ufuate kilichokupeleka mimi nimeshuhudia wengi wakipoteza direction kutokana na maisha ya hostel maana huko ni kawaida kukuta jamaa na demu wake wote wanasoma darasa moja wanaishi kama mume na mke . Sasa kivumbi huja wakipigana chini hivyo mwenzangu na mimi kama na wewe ni wakuigaiga kufeli nje nje ..

Yapo mengi lakini machache ni hayo
 
Kumbe watu bado mnasoma na hamna ajira.mimi nakushauri nenda kariakoo jifunze uwinga utapata pesa elimu hailipi nowdays
 
Back
Top Bottom