Hongera , lakin haujasema je wewe ni mwenyeji wa hapo hapo Dar es salaam au unatokea mkoa na shule ndyo umekuleta jijini ??... Kwanini nimekuuliza
1)kama umetokea mkoa kaaa uelewe Dar es salaam hamna shule ya bweni ya serikali namaanisha shule zote maarufu Dar kama
- Azania
- Tambaza
- kabasila
- chang'ombe
- jangwani
- Benjamini na nyingine nyingine wadau watanisaidia
Siyo shule za bweni , hivyo basi kuna hostel za watu binafsi ambazo huwapangisha wanafunzi kwa gharama fulani , mfano zipo ambazo kwa mwezi ni tsh 20000 mbaka 45000
Hizi za 20000/= moja zina kunguni wengii sanaa hili lazima nisa lakini pia siyo nzuri sana kwa mwanafunzi kujisomea kumbuka kwenye hizi hostel uhuru ni wakutosha unaweza hata usikanyage darasani mwezi mzima na hamna atakae kuuliza hapo msala utakuwa kati ya wewe na walimu wa shuleni kwenu
- kwasababu Azania ni boys sina tatizo ila ingekuwa chang'ombe au kibasila kule hapa ningekushauri ukasome sanaa ufuate kilichokupeleka mimi nimeshuhudia wengi wakipoteza direction kutokana na maisha ya hostel maana huko ni kawaida kukuta jamaa na demu wake wote wanasoma darasa moja wanaishi kama mume na mke . Sasa kivumbi huja wakipigana chini hivyo mwenzangu na mimi kama na wewe ni wakuigaiga kufeli nje nje ..
Yapo mengi lakini machache ni hayo