Nimecheka sana, kumbe wabunge ni weupe hivi!

Nimecheka sana, kumbe wabunge ni weupe hivi!

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Leo nikawa nasikiliza Bunge, kwanza wakavuruga ratiba na kuweka session ya kumpongeza Rais Samia kupata tuzo kila mmoja akawa anampamba anavyoweza, kama ungekuwa humjui wanaemsifu haki ungejua malaika ameshuka. Mjadala wa kutumia kodi zetu kufanya hivyo niache kila mtu auamue moyoni anavyopenda.

Akaja huyu mama maendeleo sasa kuupamba umaarufu wa 'Royal Tour'

"Lakini mheshimiwa spika, umaarufu wa royal tour, kwa wale ambao wanaangalia tamthilia ya 'Revenge' kwenye king'amuzi cha azam, jana Melan alimwambia mchumba wake, nikufanyie nini au nikupeleke Tanzania'. Kwa maana hiyo inaonesha jinsi ambavyo royal tour imezaa matunda."

Mimi sio mfatiliaji wa hizi tamthilia lakini siku niliyowakuta wanangu, ilinichukua dakika kung'amua wale wanaotafsiri wanazi- localize ili ziendane na mazingira ya Tanzania, tamthilia inataja hadi Manzese, mbunge anaamua kuitumia kufanyia reference bungeni kumpongeza Rais!

Jaffo nae akasema hadhani kama mama analala kwa jinsi anavyofanya kazi🤣🤣

Basi 'session' ikaisha kwa Bunge lote kusema 'ndiooo' kuafiki hoja ya azimio la Bunge kumpongeza Rais Samia kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawashi Duniani kupewa tuzo

Nikikumbuka 'PAYE' yangu inawezesha haya, nachoka kabisa!

=======

 
FB_IMG_16534718686023514.jpg
 
Changamoto sana. Yaani session nzima ya Bunge ni kumpongeza Rais tu na wengi ni kuzungumzia jinsia ya aliyepokea tuzo kitu inafanya hadi humu wanaopamba naona kama akili zao na wanawake wanaonadi jinsia zao ni zile zile.
 
Back
Top Bottom