Nimecheka sana, kumbe wabunge ni weupe hivi!

Nimecheka sana, kumbe wabunge ni weupe hivi!

Kwanza bunge lenyewe lipo? naona wananchi wamelisusia. Hakuna hata mwenye habari
Lipo mkuu na linatafuna posho kila kikao, wanaendelea kujadili bajeti na siku chache zijazo wanaenda kuamua mustakabali wa watanzania kwa mwaka mzima wa fedha.
 

Attachments

  • maxresdefault.jpg
    maxresdefault.jpg
    79.1 KB · Views: 14
  • 1-B-950x633.jpg
    1-B-950x633.jpg
    65.3 KB · Views: 14
  • IMG-20200908-WA0005.jpg
    IMG-20200908-WA0005.jpg
    60.5 KB · Views: 11
  • Screenshot_20220526-121519.png
    Screenshot_20220526-121519.png
    182.3 KB · Views: 13
  • Screenshot_20220526-121938.png
    Screenshot_20220526-121938.png
    318 KB · Views: 10
  • Screenshot_20220526-121511.png
    Screenshot_20220526-121511.png
    164.3 KB · Views: 11
Leo nikawa nasikiliza Bunge, kwanza wakavuruga ratiba na kuweka session ya kumpongeza Rais Samia kupata tuzo kila mmoja akawa anampamba anavyoweza, kama ungekuwa humjui wanaemsifu haki ungejua malaika ameshuka. Mjadala wa kutumia kodi zetu kufanya hivyo niache kila mtu auamue moyoni anavyopenda..

Akaja huyu mama maendeleo sasa kuupamba umaarufu wa 'Royal Tour'

"Lakini mheshimiwa spika, umaarufu wa royal tour, kwa wale ambao wanaangalia tamthilia ya 'Revenge' kwenye king'amuzi cha azam, jana Melan alimwambia mchumba wake, nikufanyie nini au nikupeleke Tanzania'. Kwa maana hiyo inaonesha jinsi ambavyo royal tour imezaa matunda."

Mimi sio mfatiliaji wa hizi tamthilia lakini siku niliyowakuta wanangu, ilinichukua dakika kung'amua wale wanaotafsiri wanazi- localize ili ziendane na mazingira ya Tanzania, tamthilia inataja hadi Manzese, mbunge anaamua kuitumia kufanyia reference bungeni kumpongeza Rais!

Jaffo nae akasema hadhani kama mama analala kwa jinsi anavyofanya kazi🤣🤣

Basi 'session' ikaisha kwa Bunge lote kusema 'ndiooo' kuafiki hoja ya azimio la Bunge kumpongeza Rais Samia kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawashi Duniani kupewa tuzo

Nikikumbuka 'PAYE' yangu inawezesha haya, nachoka kabisa!

=======

View attachment 2239164

Huyu si ni miongoni mwa COVID 19??? khaa bange(makushabu) mbayaaaa bora watumie skanka watapata akili.
 
Back
Top Bottom