Nimecheka sana, kumbe wabunge ni weupe hivi!

Si mlitaka Bunge live, pokeeni hizo komedi kwa udhamini wa Kodi za wananchi
 
Leo nikawa nasikiliza Bunge, kwanza wakavuruga ratiba na kuweka session ya kumpongeza Rais Samia kupata tuzo kila mmoja akawa anampamba anavyoweza, kama ungekuwa humjui wanaemsifu haki ungejua malaika ameshuka. Mjadala wa kutumia kodi zetu kufanya hivyo niache kila mtu auamue moyoni anavyopenda..

Akaja huyu mama maendeleo sasa kuupamba umaarufu wa 'Royal Tour'

"Lakini mheshimiwa spika, umaarufu wa royal tour, kwa wale ambao wanaangalia tamthilia ya 'Revenge' kwenye king'amuzi cha azam, jana Melan alimwambia mchumba wake, nikufanyie nini au nikupeleke Tanzania'. Kwa maana hiyo inaonesha jinsi ambavyo royal tour imezaa matunda."

Mimi sio mfatiliaji wa hizi tamthilia lakini siku niliyowakuta wanangu, ilinichukua dakika kung'amua wale wanaotafsiri wanazi- localize ili ziendane na mazingira ya Tanzania, tamthilia inataja hadi Manzese, mbunge anaamua kuitumia kufanyia reference bungeni kumpongeza Rais!

Jaffo nae akasema hadhani kama mama analala kwa jinsi anavyofanya kazi🤣🤣

Basi 'session' ikaisha kwa Bunge lote kusema 'ndiooo' kuafiki hoja ya azimio la Bunge kumpongeza Rais Samia kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawashi Duniani kupewa tuzo

Nikikumbuka 'PAYE' yangu inawezesha haya, nachoka kabisa!

=======

View attachment 2239164
Usisahau kuwa wanalipwa mamilioni na mafao yao wanachukua bila kujali umri wala kikokotoo!

Kuhusu weupe wao... Asilimia kubwa wakikaa kimya wanaonekana kama zimo!

NB: Jaribu kuwazuia watoto wako kuangalia vitu vya ajabu. Utanishukuru siku za usoni!
 
Leo nikawa nasikiliza Bunge, kwanza wakavuruga ratiba na kuweka session ya kumpongeza Rais Samia kupata tuzo kila mmoja akawa anampamba anavyoweza, kama ungekuwa humjui wanaemsifu haki ungejua malaika ameshuka. Mjadala wa kutumia kodi zetu kufanya hivyo niache kila mtu auamue moyoni anavyopenda..

Akaja huyu mama maendeleo sasa kuupamba umaarufu wa 'Royal Tour'

"Lakini mheshimiwa spika, umaarufu wa royal tour, kwa wale ambao wanaangalia tamthilia ya 'Revenge' kwenye king'amuzi cha azam, jana Melan alimwambia mchumba wake, nikufanyie nini au nikupeleke Tanzania'. Kwa maana hiyo inaonesha jinsi ambavyo royal tour imezaa matunda."

Mimi sio mfatiliaji wa hizi tamthilia lakini siku niliyowakuta wanangu, ilinichukua dakika kung'amua wale wanaotafsiri wanazi- localize ili ziendane na mazingira ya Tanzania, tamthilia inataja hadi Manzese, mbunge anaamua kuitumia kufanyia reference bungeni kumpongeza Rais!

Jaffo nae akasema hadhani kama mama analala kwa jinsi anavyofanya kazi🤣🤣

Basi 'session' ikaisha kwa Bunge lote kusema 'ndiooo' kuafiki hoja ya azimio la Bunge kumpongeza Rais Samia kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawashi Duniani kupewa tuzo

Nikikumbuka 'PAYE' yangu inawezesha haya, nachoka kabisa!

=======

View attachment 2239164
Ukiwa mwanasiasa akili unaweka matakoni, wapo wachache Sana wanaojielewa Sana lakini hawapewi madaraka, wakisema ukweli wanaambiwa wasaliti. Ndiyo bunge limebaki la hawa vilaza.
 
Ila ubunge ungekua unagombaniwa na watu wenye level fulani ya elimu.
Hii ya kuchanganya wote humo humo, weledi unapungua sana.
Mmoja akifanya ujinga basi wote wanaiga.
Wabunge wengi wana uwezo wa kuongea tu ila elimu zao ni za wasiwasi sana.
 
Back
Top Bottom