Nimechelewa sana kugundua kuwa mimi ni masikini

Nimechelewa sana kugundua kuwa mimi ni masikini

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,508
Reaction score
15,276
Tangu utotoni nimeishi kwenye comfort zone. Kwangu, kula milo mitatu kwa siku, kupata mahitaji muhimu, kulipiwa ada na kuwa na mahali salama pa kuishi vilikuwa vitu vya kawaida.

Kwa kifupi, nilijiona ninaishi maisha mazuri sana.

Hadi nilipomaliza chuo na kuanza kujitegemea mwenyewe.

Hapo ndipo nilipoanza kupata picha halisi ya maisha.

Vitu ambavyo nilikuwa naviona ni vya kawaida kupata au kumiliki, nilianza kugundua kwamba ili uweze kuvipata kwa nguvu zako mwenyewe, zinahitajika juhudi kubwa, sacrifice na kujitoa sana.

Ndoto nilizonazo, ukiangalia kwa juu unaweza kusema, “Hizi ni achievable tu.”

Lakini unapokutana na uhalisia wa maisha ndipo unagundua kwamba kufikia hizo ndoto kunahitaji nguvu kubwa, discipline, consistency na mapambano makali.

Kuna wakati unajiuliza, “Kumbe maisha yana gharama hivi?”

Na hapo ndipo nilipogundua kitu kimoja:

Nilikuwa nimechelewa sana kugundua kwamba kumbe mimi ni masikini.

Sio kwamba sina kitu kabisa. Hapana.

Namshukuru Mungu kwa kila hatua niliyofikia, kwa nilichonacho na kwa uwezo wa kuendelea kupambana.

Lakini nikijiangalia kwenye level ninayotamani kufika, bado najiona niko mbali sana.

Bado nahitaji kwenda NEXT LEVEL.

Na labda hii ndiyo mindset ambayo wengi tunahitaji kuwa nayo.

Tusiridhike sana na comfort zone. Tusione mafanikio madogo kama mwisho wa safari.

Kama umefikia hatua fulani, congratulations — lakini endelea.

Jenge uwezo wako.
Jiongezee maarifa.
Ongeza vyanzo vya kipato.
Kubali sacrifice.
Fanya kazi kwa consistency.
Na zaidi ya yote, usiogope kuota big.

Maisha yanaweza kuwa magumu kuliko tulivyofikiria, lakini bado naamini kuna possibility ya kufika mbali zaidi.

Tujenge utamaduni wa kutoridhika na kiwango cha chini.

Tupambane kufika top level.

Kwa sababu mwisho wa siku, kila kitu kinawezekana ukiweka nia, juhudi na consistency.
 
Kumbuka pia kushukuru kwa hatua uliyonayo sasa. Ni vizuri kuwa na ambition ya kwenda next level, lakini usijihukumu sana ukahisi wewe ni masikini wa kutupwa. Kila mtu ana timeline yake kwenye haya maisha. Kikubwa ni kwamba umeshajua unachotaka na uko tayari kupambana kukipata.
 
"Mtu mjinga ni yule anaishi maisha yake yote kukimbizana na hela na kusahau kuishi na kuitunza afya yake ambapo atakapokuja kupata hizo hela anajikuta anaishi maisha yake ya mwisho kutumia hizo hela kujitibu kwa gharama mpaka kufa kwake"
Dalai Lama
 
Jenge uwezo wako.
Jiongezee maarifa.
Ongeza vyanzo vya kipato.
Kubali sacrifice.
Fanya kazi kwa consistency.
Na zaidi ya yote, usiogope kuota big.
Wewe bado Sana hata Uwezo wa Wazazi wako wa kukupa Milo mitatu sasa uko peke yako na unashindwa bado Una Dream Big?

Anza na small steps hizo big zinafuata

Ni ujinga kujiganba mbele za watu kwamba Una Dream kumiliki Kampuni ya ndege wakati hata Uwezo wa kumiliki pikipiki huna.
 
Unajiona ni masikini kwa mtazamo wako na viwango vyako. Hata mo ni masikini ukimlinganisha na viwango vya kina jef na gates
Na hii ndio shida ya kujilinganisha na Watu, kila mtu ana mafanikio kutokana na alipokuwa Mwanzo na alipo sasa.

Loth Hema anayemiliki magari matatu wakati Baba yake alikuwa na Kampuni ya Semi Trailers(Trucks) ni mdumavu wa maendeleo ukimlimganisha na BushDokta anayemiliki IST kutoka kwa Baba na Mama waliokuwa wanaishi nyumba ya makuti na majani bila hata baiskeli.

Nadhani nimeeleweka.
 
Hizo top level unazosema ndio zipi labda wengine tulisha zifikia ila hatujui

NAdhani kipimo kizuri ni wewe wa Jana dhidi ya wewe wa Leo. Kama wazazi wako walikua wanakupa Milo mitatu na wewe mlo mmoja unakupiga chenga apo kweli inabidi uongeze juhudi
 
Back
Top Bottom