Nimechoka kupokea wageni

Nimechoka kupokea wageni

Kuna wengine watakunafkia hapa kujifanya wema sana ila kiukhalisia kwenye familia zao hata mgeni hakanyagi..!!

Ishi kulingana na budget iliyo ndani ya uwezo wako usitumie nguvu kubwa sana kuwafurahisha watu huku unateseka (mshumaa),

Habari mbaya ni kuwa at the end of the day baada ya kuwa hu-save wala kufanya maendeleo yoyote wewe ndiye utaonekana looser, hakuna mtu atakumbuka kile uli sacrifice kwa ajili yao..!! Shauri yako..!!

Mac Alpho
kabisa mkuu wala si uwongo ,shida ya watu wengi kutaka kujifanya wema
 
Ha haa umenikumbusha kaka (cousin) yangu mmoja aliwafanyia hivyo shemegi zake.

Yeye alikuwa ni mpiga maji mzuri sasa kila siku akirudi nyumbani kumejaa wageni mashemegi. Matokeo watoto wanalala ukumbini na mashemegi wanajitanafasi chumba cha watoto. Nyumba zenyewe za Dar vyumba viwili.

Siku moja aliamua kwenda kuuchapa vizuri na alipofika nyumbani mlangoni alianza kuwashambulia kwa maneno makali, kwa nini hawakai makwao kwa waume zao au wazee wao wanakuja pale kumjazia nyumba. Wale mashemegi walichukia sana na siku ya pili walifunga virago kurudi makwao.

Mke wake pia alijifanya kuchukia lakini alimwambia kama unaona mimi nimekosea na wewe funga virago uelekee kwenu, ikabidi mama anyamaze tu. Basi tokea siku hizo nyumba ile walikuwa wakiipisha kwa mbali sana.

Hii alinihadithia mwenyewe nikamuuliza kama alijisikia vibaya kwa kuwatimua mashemegi kivile. Aliniambia nilikuwa sina jinsi bajeti ilikuwa haitoshi tena ikabidi nijitoe akili ili mambo yangu yaende.

The guy is too clever[emoji23], ukitafuta uzuri utaishia kua maskini.
 
Mtoa Uzi utakuwa mchaga sio Kwa roho mbaya hivo,,, wachaga ndo wenye roho ya kwanini na uchoyo plus ukabila na hawataki kabisa ndugu wa mwenza wake waje

Na ndio maana wameendelea lbd kuzif makabila yote hawa jamaa na mara nyingi wanaoa wahaya sababu ni wabinafsi wenzao na hawataki tegemezi la kupitiliza, Africa hatuendelei sababu ya tegemezi...ni too much na cha maana hakuna zaidi ya kurudishwa nyuma kimaendeleo na kufitiniwa tu...jikute una roho nzuri sana tuone km hutakufa maskini! Kila kitu kiwe na kiasi
 
Back
Top Bottom