Nimechoka kupokea wageni

Nimechoka kupokea wageni

Umeoa msambaa nini?
We cha kufanya hapo ni kununua shamba moja kubwa kinyama na majembe ya mkono wakija hata kiangazi ni kuwajaza shambani wakapalilie hata yale majani yanayoitwa mashona nguo

Halafu suala la msosi usipike msosi wa sherehe man hapo ndo unakwama pilau ya nini sasa? Hapo pika ngumu kumeza mboga maji Mingi mchicha nne ili mradi tu maji yawe ya kijani kama chai wanatoezea tonge la ugali imeisha hiyo
Uone kama Kuna mtu atakaa hapo

Dah umeniwahi, watu wa tanga na wasukuma ni keroooo, na ni wanafki ukiwa nacho utawaona usipokua nacho hutakaa uwaone kamwe! Wa nini sasa? Fukuza
 
Wanamtegemea au wanakuja kusali hyo ni roho mbaya plus ghubu hamna kingine
Na ndio maana wameendelea lbd kuzif makabila yote hawa jamaa na mara nyingi wanaoa wahaya sababu ni wabinafsi wenzao na hawataki tegemezi la kupitiliza, Africa hatuendelei sababu ya tegemezi...ni too much na cha maana hakuna zaidi ya kurudishwa nyuma kimaendeleo na kufitiniwa tu...julikutenroho nzuri sana tuone km hutakufa maskini! Kila kitu kiwe na kiasi
 
Enzi hizo tukiwa wadogo mzee alikuwa amejenga karibu kabisa na stand ya mabasi ya mkoa, basi ilikuwa hazipiti wiki kadhaa bila kuwa na wageni pale nyumbani, wengine walikuwa wakifikia pale ili kujiandaa na safari zao, wengine walifikia pale wakitoka kwenye safari zao, waijazana sana pale.

Mzee alipofariki sasa, wageni wakapungua, hata wakiwa na safari waliona wawe wanalala kwenye lodge badala ya kupita pale, nadhani walihisi kuwa hakuna raha watapa tena pale zaidi ya kuhitajika labda kusaidia (kitu ambacho hakikuwa uhalisia vile kutona stable economy iliyokuwepo ila ni mama aliamua kuwapiga PIN tu[emoji1]).

Ndugu na jamaa watamiminika kwake wakijua kuna vitu watafurahia, the moment huo mrija umekatika hatawaona na watamcheka.

Hii ndio tabia halisi ya Muafrika, sasa chagua sifa za kijinga au maendeleo yako
 
Dah umeniwahi, watu wa tanga na wasukuma ni keroooo, na ni wanafki ukiwa nacho utawaona usipokua nacho hutakaa uwaone kamwe! Wa nini sasa? Fukuza
Bila roho mbaya hutoboi ukioa kwenye hilo kabila ukajifanya baba wa Iman utapika ugali pipa 13
 
Habari! Naelewa kuwa wewe na mke wako mmeishi pamoja kwa miaka minne sasa na tatizo lako kubwa ni kwamba wageni hawaondoki nyumbani kwako, na ndugu zake wanatoka na kuingia kiasi kwamba huwezi kuokoa pesa yako.

Siku chache zilizopita, mgonjwa wa vidonda vya tumbo alikuja nyumbani Jumapili, ambapo kawaida hupikiwa pilau, lakini wewe mlipika ndizi kwa ajili yake. Walakini, alikwenda kugombania ukoko wa pilau na mtoto wako mdogo mpaka alipokwenda kukuambia chumbani.

Ni muhimu kuwasiliana na mke wako na kujadili jinsi ya kushughulikia hali hizi. Labda unaweza kuweka mipaka na wageni, kama vile kuzuia muda wa kukaa kwao au kuwakataa wageni kadhaa kabisa. Inaweza pia kuwa na manufaa kuwa na chumba cha wageni au eneo ambalo wanaweza kukaa badala ya kuvamia nafasi yako binafsi.

Kuhusu tukio la mgonjwa wa vidonda vya tumbo na chakula, ni muhimu kuwa na ufahamu na kukidhi mahitaji yake, lakini pia kuwasiliana wazi kuhusu unachoweza kutoa. Inaweza kuwa na manufaa kujadili na mke wako chaguzi mbadala za chakula ambazo zinaweza kukidhi mahitaji ya lishe ya wageni, lakini bado ziko ndani ya uwezo wako.

Kwa ujumla, mawasiliano na kuwe.....


Shenzi! MTOTO WA 2006 UMEFUNGA LINI NDOA, ACHA KUCHEZA NA AKILI ZA WATU[emoji23][emoji23]
 
Mkuu hili kama halijakufika au kumfika mtu wa karibu unaposema watu hawatakuelewa na kauli zao zitakuwa acha roho mbaya ,ila hawajui wema ukizidi sana ni hatari maana unaweza jitoa kwa watu matokeo yake hao hao uliojitoa kwao wasione na unapoyumba wakawa wakwanza kukucheka

Si bora wacheke watanyamaza my dear, kuna wengine ndio wanakua chanzo cha wewe kuanguka kabisa
 
Hellow Africa

Dah ninaishi na wife huu mwaka wa nne sasa ila kero kubwa wageni hawakauki hapa nyumbani ndugu zake wanaingia na kutoka kiasi kwamba mtu huwezi kuweka akiba yako.

Juzi kaja mgonjwa wa vidonda vya tumbo Jumapili huwa tuna kawaida ya kupika pilau yeye tukampikia ndizi lakini wapi eti kaenda kugombania ukoko wa pilau na mwanangu wa mwisho mpaka kaja kuniambia chumbani.
Mhhh sawa, umasikini hawezi kuisha Afrika ukitaka kujikongoja kidogo ndugu haoooo
 
Si bora wacheke watanyamaza my dear, kuna wengine ndio wanakua chanzo cha wewe kuanguka kabisa
kabisa mimi haya nimeona kwa mzee wangu ,alivyokuwa na pesa zake watu walikuwa hawakauki nyumbani ,ila baada mzee kuyumba mpaka bi mkubwa ana lalamika hakuna anayekwenda hapo home,mimi mpaka nimekuwa na maisha yangu huwa sipendi mazoea na ndgu na hasa mnaotaftana baada ya kuwa na maisha ya afadhali ,
 
kabisa mimi haya nimeona kwa mzee wangu ,alivyokuwa na pesa zake watu walikuwa hawakauki nyumbani ,ila baada mzee kuyumba mpaka bi mkubwa ana lalamika hakuna anayekwenda hapo home,mimi mpaka nimekuwa na maisha yangu huwa sipendi mazoea na ndgu na hasa mnaotaftana baada ya kuwa na maisha ya afadhali ,

Yaani mkuu, kuna msemo unasema mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba, ukiendekeza mandugu na kutaka kuonekana mwema maendeleo utayasikia kwa jirani! Ni wanafki na washirikina wakutaka ufeli wacheke...achana nao jali familia yako tu, wwo wape kiasi na wasikuzoee watapeana taarifa tu.
 
Hakikisha hapo kwako kuna kazi za kutosha kama kuosha mabanda ya mifugo,kukata nyasi za mifugo,tafuta mashamba huko nje ya mji uwe unawapeleka kulima na kupanda

Okoka na muwe mnasali karibia masaa mawili kabla ya kwenda kulala iwe kila siku na lazima kila mtu awepo wakati wa kusali hata kama ni mgonjwa,tv weka chumban kwako,sebuleni liwepo sabufa la kupiga nyimbo za injili tu

Ukishindwa kabisa hayo yote,anza kuwala ndugu za mkeo kwa siri,ili ufaidi chakula chako

Fanya yote hayo afu unipe mrejesho
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom