Nimechoka kusindikiza wenzangu kwenye madini

Kwahiyo mkuu kati ya hizo sehemu ipi ni mzuri kuwekeza?
 
Nimepigwa mueleka huko itumbi chunya. Nimepoteza zaidi ya milioni 89 kuanzia mwaka 2020 mpaka 2023. Mtindo ulikuwa huo huo. Unapima nakutana na Ppm 6. Lakini mwisho wa kupeleka prant na elution kidogo nizimie. Nilitoa hela zote za duka nikahamishia huko. Nimerudi dukani najikongoja. Japo nitarudi tena kwenye madini
 
Kwa mtu mwenye mtaji wa milion 60 unamshauri kwa uzoefu wako awekeze sehemu ipi kwenye sekta ya madini?
 
Ni kama vile ulijaribu ushirikina ikashindikana?

Kuna mdau ameshauri ninunue dhahabu nikasema hiyo kazi nnaijua vizuri, unafilisika siku moja,

Usipouziwa fake, hela itaenda kwa kutoa advance na usipotoa hupati wauzaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…