Nimechoka kusindikiza wenzangu kwenye madini

Nimepigwa mueleka huko itumbi chunya. Nimepoteza zaidi ya milioni 89 kuanzia mwaka 2020 mpaka 2023. Mtindo ulikuwa huo huo. Unapima nakutana na Ppm 6. Lakini mwisho wa kupeleka prant na elution kidogo nizimie. Nilitoa hela zote za duka nikahamishia huko. Nimerudi dukani najikongoja. Japo nitarudi tena kwenye madini
Utarudi kawaida au utafanya namna?
 
Kwa mtu mwenye mtaji wa milion 60 unamshauri kwa uzoefu wako awekeze sehemu ipi kwenye sekta ya madini?
Swali Zuri. Kwa uzoefu wangu kama ni upande wa huku Chunya.
1. Bora upambane upate eneo lenye mwamba mkubwa usiopungua Mita 1 ukubwa wake hata likianzia kusoma PPm 3 kwenye Mita 4,5 kwenda chini. Hakikisha pambania hilo eneo kama lina leseni kubwa za Shanta,halafu linamikiwa kienyeji. Ombea chap Leseni yako kwa jina lako. Yaani unakuwa na Leseni ndogo ndani ya Leseni kubwa. Yule mwenyeji utamalizana nae tu kabla ya kuanza kazi. Muhimu katia Leseni yako baada kujua pana mwamba na unasoma hivyo. Uzuri wa kufanya kazi sehemu yako ni kuepuka kumfanyia kazi mtu unaingia gharama kubwa lakini mawe anachukua 30% akiwa amekaa tu hajui gharama. (Hilo ni sehemu ya hasara).
MUHIMU. Wakati wa kuchukua sampling ya kwenda kupima maabara ikiwezekana simamimia huo uchimbaji kwa karibu sana au chukua wachimbaji wageni kabisa wa eneo hili HAPA NDIO WENGI TUMEPIGWA. UKICHUKUA WENYEJI WA ENEO HILO WATAKUNYUNYIZIA SAMPLE SAMPLE ZENYE DHAHABU UNGA UNAOENDA KUPIMA ILI IKAKUCHANGANYE PPM KWENYE VIPIMO. KUMBE UHALISIA SIO HUO.

2. Wekeza kwenye kuchimba,huku ukiwa umefunga kalasha lako. Jitahidi funga kalasha sehemu iliyopita umeme. Funga la kutumia umeme sio mafuta.

3. Simamia mwenyewe kwa karibu. Kila sehemu fuatilia kwa karibu kuanzia uchimbaji na kalashani

4. Nenda kupima sample kila baada ya Mita 5 ya urefu wa duara lako.

5. Sehemu ya mwisho ya kuwa makini ni Elution.
 
Umenena vyema mkuu,
 
Milioni 40 ungewekeza kwenye biashara nyingine saa hii ungekuwa unahesabu faida ya ya laki tatu au nne kwa siku.

Hizi biashara hazifanywi kwa kubeti zinataka utaalamu mzuri wa miamba ambao utaweza kukuonyesha mahala madini yalipo. Vifaa vya kisasa vipo na vinakusaidia kuona madini yalipo. Nadhani unatakiwa kujipanga upya kwenye hii kazi.
Hiyo 40 sidhani kama alikua nayo cash, nadhani ile kidogokidogo kwa kipindi chote alichokaa.
 
Back
Top Bottom