Wakuu mimi ni 26 Me, mzaliwa wa kanda ya ziwa, taaluma yangu Medical doctor degree, nimeletwa na mambo mawili;
Kwanza
Naota nakula sana mara nyingi ni wali na matunda na muda mwingine unajaribu kukataa kabisa ila kuna mtu anakubembeleza. Hii ya leo nimeenda sokoni nikakuta matunda mfano wa nyanya nkasema ninunue, yalionekana mabaya ila muuzaji ambae ni mwanamke, binti yake na mume wake wakayarekebisha na kunipa nile. Tena walikuwa wananisimamia nikila na kuyasifia ile naamka nshakula na mdomoni pamejaa mate na tumbo liko full.
Pili
Naota sana napiga mitihani au napambania kupiga mitihani ya level ambazo nishapita na utakuta napambania sana kupata hiyo nafasi huku wenye mamlaka wakinibania. Hii ya juzi nimeota nimefeli f4 nikarudi kurudia primary kusoma na wadogo zangu ambao nao hawako primary walishatoka kitambo.
Kuhusu maisha yangu mimi niko single, wanawake nakuwa nao kwa hamu, wengine wa kununua, wengine ni wale wanaojichanganya tu; sina mapenzi kabisa na nlishasahau mapenzi ya kweli yakoje.
Nliwahi na huwa nanunua malaya ambapo kwenye harakati hizo huwa natetemeka sana, moyo unauma na mapigo ya moyo kwenda mbio na kila nikifanikiwa kuwa naye mlingoti unazingua kusoma na nkifankiwa kumaliza naye mchezo roho inasuta hadi natamani kufa ila siku zikipita tena narudia.
Idadi ya malaya niliowahi kununua haiesabiki na hadi jana nimefanya hadi naandika hapa roho inauma mno. Nna uhakika asilimia mia hakuna anayejua na anayeweza kudhani hata kwa kuhisi kuwa mimi naweza kununua malaya.
Mahusiano yangu na wanawake ni mabovu sana nkishalala nae tu namsahau naanza kuangalia mwingine wengi wanalia na kuona nazingua maana kwa muonekano nlonao mwanamke akiniona atasema huyu ndo mwanaume ila akinijua vizuri ataishia kulia maana hatachoka kuona rangi za kila aina.
Mimi pia n introvert nachoshwa na watu waongeaji sana nafurahi kampani yangu mwenyewe, sinaga maneno mengi huwa naongea kufikia conclusion na sipendi majadiliano ya muda mrefu. Naweza kumkubalia mtu ashinde kwenye majadiliano na wakati ndani ya moyo wangu nmekataa.
Nna marafiki wachache sana ambao naweza sema ni quality, naweza kuzoeana na watu kwa muda mchache na kupotezeana nao kirahisi. Kuhusu wazazi na wadogo zangu nawajali sana kwa lolote wanalohitaji napambana waweze kupata.
Nilikuwa mtu wa dini na imani sana ila siku hizi sisali na mlango wa kanisa nmeusahau. Maisha yangu ya shule hayakuwahi kuwa magumu kwenye ufaulu, hadi sasa nina ajira kwenye taasisi binafsi, kama kazi za kitabibu napiga kweli ila naona ufahamu wangu unapungua sana sitaki kusoma na thinking yangu naona inapungua.vision na malengo yangu ya kimaisha hayako na mpangilio yani kuna namna nnavopangilia maisha ya mbeleni sio kama nlivokuwa awali.
Maswali nnayojiuliza ni mawili;
Kwann kila siku ndoto zangu ni hizo mbili na sio za maisha kama nlvokuwa hapo nyuma
Pili kwa nn nakosa vision na maisha yangu ya mbeleni yan naamka naenda napiga kazi narudi kulala cycle inaendelea.
Nliyoyaandika yote ndo nmekuwa nkipitia tangu nkiwa na miaka 20 nkiwa mwaka wa kwanza chuo. Baada ya miaka sita ya maisha ya namna hii nmeamua leo nifunguke niweke wazi wakuu mnisaidie maana hadi naandika hapa nmechoshwa na ndo mara ya kwanza nalizungumzia.
Mnisamehe uandishi wangu hauko vizuri sana.
Kwanza usisome chochote kitakokufanya ujione huna matarajio (hope) yoyote, au maneno yanatakayokufanya uone huna mwelekeo, au ujione hufai au ujione we ni mbaya au ujione una mapepo au ujione umefungwa. ACHANA NAYO hayakusaidii chochote. Ukweli ni kuwa ndoto zako ni ujumbe wa nafsi yako kwamba kuna nini kinatokea, au nini cha kurekebisha au nini cha kufanya, we unachotakiwa kufanya ni kuisikiliza nafsi yako majibu yote unayo.
.
Umekuwa unawakubalia watu hata kama moyoni unakataa, unachukua malaya lakini unajisikia vibaya ukiwa nao ni hicho hicho mwili wako unakuambia kuwa huwezi sema hapana kwa nyege zako au kwa watu wengine. Kwa kuwa haukulifanyia kazi ndo mana nafsi yako inakuletea ndoto kuwa unashindwa kusema hapana na unaendelea kulishwa.
Nafsi yako inaleta hiyo ndoto ili upate kuelewa hali uliyonayo katika maisha ya mchana, na ufanyie kazi.
Ndoto ya pili inakuonesha umerudi mpaka level uliyokua vizuri, maana yake hiyo ndo sehemu ya maisha yako uliyokua una ishi kwa malengo kulinganisha na sasa. Na kufeli ni kwamba tu ulikua vizuri mpaka ulipofeli kwenye maisha ya mchana. Kiurahisi nafsi yako inakuonesha wapi uliishia kuwa mtu bora zaidi.
.
Anza hivi;
- Jiwekee malengo mapya. Andika vile unataka uwe mbeleni kisha chukua iyo karatasi na ubandike sehemu utakayoiona kila siku.
- Badili mazingira unayoishi, hii iwe ishara kwa nafsi yako na akili yako kwamba unabadili maisha yako. Na wewe pia jikumbushe mara kwa mara kuwa unabadili maisha yako. Kumaanisha una break cycle uliyoisema.
- Washirikishe ndugu zako wa karibu kuwa upo kwenye mchakato wa kubadilika, na wanaweza wakakuona wa tofauti kidogo lakini lisiwatie shaka mana ni kwa ajili yenu nyote.
- Kubali ndani yako kuanza kivingine. Ukikubali utakua umejipunguzia mzigo wakati wa mchakato wa kubadilika. We ni tabibu najua unajua kwamba ili mwili ubadili mfumo unahitaji takribani siku 30, hivyo kubali itachukua muda.
Pia katika safari ya mabadiliko utakumbana na hali ya kutaka kurudi kama mwanzo kwa kuwa mwili haujazoea lakini huo ndo muda mwili na seli zako zinaandika mfumo mpya ndani ya mwili wako. Ulichoishi hadi sasa ni mfumo tu, pitia uzi nilioandika kuhusu mfumo, ila ubadili baadhi ya maneno na uchukulie kama ndo maisha yako.
Aisee ile topic ilikuwa na maana sana aiseee....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Kabisa
- Anza kujizoesha kuwa na misimamo na uwe na thamani zako (values). Hii ni mihimili ambayo itakuongoza kwenye kufanya maamuzi yako yote. Jitahidi usome kitabu kimoja kinaitwa 'The Confidence Gap by Dr Russ Harris'.
- Kutakua na siku utateleza. Sio kwa sababu umeweka malengo mapya basi utaenda moja kwa moja. Kwahiyo kuwa na amani siku utakazo poteza, jikumbushe kuwa na amani. ILA fanya juhudi siku mbovu ziwe chache kuliko siku nzuri.
- Nenda katoe tu shukrani kanisani, au shiriki chakula na mtu asiye na uhakika wa kula hiyo siku, au mnunulie kiatu asiye na kiatu, au chochote ambacho kitakupa furaha kinachohitaji ujitolee kwa mapenzi yako. Hii haijalishi umeshafanikiwa au bado.
- Hakikisha afya yako iko poa. Kunywa maji, fanya mazoezi. We ni tabibu najua utakua vizuri hapa.
.
Cha kufanya.
- Anza kujifunza kusema hapana, haijalishi ni nani, ila anza taratibu. Ukijizoesha hili litakusaidia kusema hapana hata kwa mwili wako pindi unajikuta unafanya kitu usichotaka.
- Weka malengo madogo madogo kwanza ili kujizoesha. Vuta kumbukumbu nyuma hadi muda uliokua una malengo na unaishi kimisingi. Kisha jikumbushe ulikua unafanyaje hicho kipindi, inaweza ikakuchukua wiki au mwezi au zaidi cha msingi tu ujikumbushie na upate ile hisia jinsi ulivyokua na uishi hivyo sasa.- Usibishane na nafsi yako. Anza kujifunza kuisikiliza nafsi yako, hata kama utaona kwa akili ya kawaida ni ngumu ila nafsi yako ina majibu mazuri. Acha nafsi yako ikuongoze. Fanya vile vitu nafsi yako inasikia furaha.
Ukitaka kujua (au ishara ya kwamba unakiuka nafsi yako) unabishana na nafsi yako, ni vile ukijisikia vibaya kama chuki, uoga, wivu, uongo au hisia zozote zinazokufanya ujisikie vibaya.
Na ukitaka kujua kama upo kwenye mstari utajisikia amani, faraja, matumaini na hisia zote za furaha.
Enjoy and have fun. Nikutakie kila la heri.