Nimechoka, naenda kununua gari

Nimechoka, naenda kununua gari

Japokuwa wanasema usifanye kitu kwa kuiga au kuhisi watu watakuonaje ila inafika point unaamua ufanye tu ili upate amani. Mimi ni kijana naishi Dar mshahara wangu ni kipato cha kati tu.

Ssasa hapa ninapoishi vijana wenzangu wote wana magari kasoro mimi sasa naona kama najifeel inferior sana, niliwahi omba ushauri humu JF wengi walinishauri nisinunue gari kwa kufuata mkumbo ila sasa naona uzalendo umenifika hapa.

Nimepanga kununua gari nina akiba yangu ya 4M bank na ninaenda kukopa 3.5M naenda kununua ist. Kwa mliokwisha kuwa na magari ya mikopo staili hii ni changamoto gani ninaweza kukumbana nazo na je utakuwa uamuzi sahihi?
Utaanza sasa kuitwa "baba mwenye gari" ingawaje "baba mwenye nyumba" ndilo jina lenye kusikika sana katika viunga vya miji mbalimbali.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Usinunue IST. Utakuja tena kutulalamikiaa kuwa haina heshima. Pambana kidogo, chukua benki 20m nunua gari ya kueleweka.
Kwa hiyo 20 ni kama ndinga gani ya kueleweka.

Sijaona haja ya kuanzisha uzi mpya nimekutana na uzi unaoendana na mawazo yangu nimeamua kutembea nao, naokota madini taratibu.
 
Trust me. Kwa DSM usipokuwa na gari status yako ni ndogo sana. Fedheha ya kuwa na deni ni ndogo sana ukilinganisha na kuwa na gari. Nilienda kwene kikao cha harusi wote walikuja na magari kasoro mimi na ninavuja jasho balaa. Nilikaa kwa unyonge sana siku hiyo.

Nilivotoka nikasema sasa sisikilizi mtu nilivoamka nikawahi bank nikakutana na dada wa mikopo nikamwambia nataka kukopa mil. 20 nikapewa mkopo within 2 weeks. Nikadaka ndinga. Guess what? Hio milioni ishirini niliipata baada ya miezi mi4. Niliitwa somewhere kuna dili la maana nikatinga na ndinga yangu suti ya maana nikasaini mkataba fasta. Maisha yakaendelea.

Acha kusikiliza watu humu hatujuani. Hata mimi niliyoyaandika usiyape kipaumbele sana utaumia.

Asalamaleko
🤣🤣🤣
 
Kama unafeel inferior, kuna options hizi;
1. Hama mtaa unaoishi nenda ambako inferiority complex yako itaisha
2. Unusual gari kama unavyowaza lakini, ujuwe kuwa siku utakayoishiwa hata hela ya mafuta utafeel inferior tena. Hebu waza, umekatikiwa mafuta barabara, ile unahangaika na dumu mmoja wa wale marafiki wanakuona na dumu..!!!

UJUWE KUWA INFERIORIY COMPLEX HAITIBIWI KWA KUKAMILISHA KILE UNACHOKIONA KINAKUPA HALI HIYO PEKEE.. UKIKAMILISHA HICHO, NDANI YA NKAMILISHO HUO KUTAZALIWA KINGINE KITAKACHOKURUDISHA KWENYE INFERIORITY COMPLEX ULIYOIKIMBIA.
Kama umemwambia kweli. Kutafuta external validation na ku feel inadequacy ni ugonjwa Kama ugonjwa mwingine.
Nashukuru Mungu hii makitu huwa hayanisumbui. Kama gari la biashara sawa Ila Sasa la kutembelea Kama hauna kipato Cha uhakika utaumia zaidi. Ile furaha ya kitu huwa inawahi kuisha ndani ya two years basi unaona Kama kawaida
 
Chukua gari kubwa kidogo, kuanzia Harrier siyo mbaya. Kuanzia 18 unaweza kupata. Lakini always remember changanya na zako
Hakika ndugu, mtu mzima hadi anachukua maamuzi hayo keshapiga hesabu nyingi sana.
 
Trust me. Kwa DSM usipokuwa na gari status yako ni ndogo sana. Fedheha ya kuwa na deni ni ndogo sana ukilinganisha na kuwa na gari. Nilienda kwene kikao cha harusi wote walikuja na magari kasoro mimi na ninavuja jasho balaa. Nilikaa kwa unyonge sana siku hiyo.

Nilivotoka nikasema sasa sisikilizi mtu nilivoamka nikawahi bank nikakutana na dada wa mikopo nikamwambia nataka kukopa mil. 20 nikapewa mkopo within 2 weeks. Nikadaka ndinga. Guess what? Hio milioni ishirini niliipata baada ya miezi mi4. Niliitwa somewhere kuna dili la maana nikatinga na ndinga yangu suti ya maana nikasaini mkataba fasta. Maisha yakaendelea.

Acha kusikiliza watu humu hatujuani. Hata mimi niliyoyaandika usiyape kipaumbele sana utaumia.

Asalamaleko

[emoji28][emoji28] walekomsilam.
 
Hahaha utaishia kujisikia inferior kwa lingine tu.

Nimekuwa na uwezo wa kununua gari toka 2016 ila ni mwaka huu ndio nimeona ninunue. Kitu kilichokuwa kinanisukuma ni kupandikisha pesa zaidi katika biashara na kuepuka kuongeza gharama za maisha.

Sijui kipato chako ni bei gani ila kama ni chini ya 1 mil kwa mwezi bado si muda sahihi. Endeleza pesa yako katika biashara uwe na hata 20 mil savings na kipato cha 2 mil kwa mwezi utakuwa katika a more comfortable position.
 
Sabb zako za kununua gari ni dhaifu sana uwe na malengo ya zaidi na hilo, gari Dar ina hudumiwa kwa average ya 20,000 kwa kila siku mwezi ni 600k, mshahara wako kama ni 900k monthly, siunaona unaingia kwenye dimbwi la 'urban silent poverty'
Gari si lazima utembelee kila siku. Balance shobo tu unaweza ukalipaki ukawa unatumia dala dala siku za weekend unaendea kwenye vikao iwe bar au kanisani ila likiwepo tu ni advantage kwako.
 
Hakuna IST ya 7.5m nzima ndugu.. unaenda nunua matatzo... Utakua mteja wa fund kila siku..

Ni bora ukanunua gar ndogo ya brand nyingne kwa hela hyo lakin mpya..

Zipo swift, fun cargo.. vi nissan kibao..

Hyo gar ya mkonon utajuta
Gari ya mkononi wengi huwa sio waaminifu imeshakufa vitu vinawekwa vya kuunga unga uichkue ukafe nayo.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Ukweli kwa DSM gari si anasa. Gari ni kitu muhimu kwenye kuanzia maisha. Nunua Gari ambayo ni economy ila isiwe chakavu kwani Gari ya kwanza ikiwa chakavu itakufilisi. Hii ni kwa sababu hautakubali kupak utakuwa unapambana kwa namna yoyote kuhakikisha ipo barabarani.

Kuna adha kubwa sana utapata kama huna usafiri ikiwemo swala la matumizi ya muda. Ukiwa na gari kila unapotaka kwenda utafika kwa wakati tofauti na anaetumia daladala.

Hata kama utaamua kuanza na kujenga utakutana na changamoto kubwa katika usimamizi kwani ukiwa na gari unaweza chomoka kazini faster ukafika site na ukarudi kazini. Hata pale utakapokuwa unatakiwa kusafirisha vitu vidogo vidogo kupeleka site.

Changamoto nyingine ukiwa na familia kama huna usafiri unaoeleweka utajuta na gharama za kukodi magari zinakuwa kubwa sana kwani kuna watoto hospitali, mke clinic na ufuatiliaji wa mambo mengine.

Mwisho, mimi ni mmoja ambao niliwahi kuwa na fikra kama zako. Lakini kutokana na changamoto mbalimbali niliamua kujilipua nikakopa. Tena sikuwa na hata ya kuongezea kama wewe. Nusu nilinunua eneo na nyingine nikanunua IST.

Sijawahi juta kwani ilinisaidia sana na iliniwezesha kufanya kazi zaidi ya moja na kuweza kuendeleza kiwanja kuwa makazi.

Gharama za usafiri zilipungua huku nikiwa na privacy kwenye mambo yangu ya kifamilia.

Gari linanunuliwa siku moja. Nyumba inajengwa Miaka kadhaa kama unakipato cha kawaida.

Huu ni ushauri waweza amua vinginevyo
Ndio inavokuwa hasa ukiwa na familia ni shida. Mtoto ili utoke nae unatokaa na full package yake anaweza kuoga njian kula na kulala.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Gari si lazima utembelee kila siku. Balance shobo tu unaweza ukalipaki ukawa unatumia dala dala siku za weekend unaendea kwenye vikao iwe bar au kanisani ila likiwepo tu ni advantage kwako.
Mkuu hapo ndo kuwa economically illogical mtu anajijenga bado kwanini upaki 13m bila kuitumia kuongeza value kwenye maisha yako hiyo inakua wastage of resources kwa kijana, hayo yana fanywa na watu kama nyie ambao mna magari mengi na mmesha jijenga kiuchumi tayari.
 
Japokuwa wanasema usifanye kitu kwa kuiga au kuhisi watu watakuonaje ila inafika point unaamua ufanye tu ili upate amani. Mimi ni kijana naishi Dar mshahara wangu ni kipato cha kati tu.

Sasa hapa ninapoishi vijana wenzangu wote wana magari kasoro mimi sasa naona kama najifeel inferior sana, niliwahi omba ushauri humu JF wengi walinishauri nisinunue gari kwa kufuata mkumbo ila sasa naona uzalendo umenifika hapa.

Nimepanga kununua gari nina akiba yangu ya 4M bank na ninaenda kukopa 3.5M naenda kununua ist. Kwa mliokwisha kuwa na magari ya mikopo staili hii ni changamoto gani ninaweza kukumbana nazo na je utakuwa uamuzi sahihi?
kanunue fasta,mimi nilinunua ninayo mwaka sasa,pamoja na vitisho vingi,nilipata amani ya moyo wangu,siku nikiamua napaki na nikiamua natembelea,sipangiwi na mtu...
 
Kama unafeel inferior, kuna options hizi;
1. Hama mtaa unaoishi nenda ambako inferiority complex yako itaisha
2. Unusual gari kama unavyowaza lakini, ujuwe kuwa siku utakayoishiwa hata hela ya mafuta utafeel inferior tena. Hebu waza, umekatikiwa mafuta barabara, ile unahangaika na dumu mmoja wa wale marafiki wanakuona na dumu..!!!

UJUWE KUWA INFERIORIY COMPLEX HAITIBIWI KWA KUKAMILISHA KILE UNACHOKIONA KINAKUPA HALI HIYO PEKEE.. UKIKAMILISHA HICHO, NDANI YA NKAMILISHO HUO KUTAZALIWA KINGINE KITAKACHOKURUDISHA KWENYE INFERIORITY COMPLEX ULIYOIKIMBIA.
Atahama mpaka wapi? Atakimbia mitaa mpaka lini? Maisha ni leo, kesho ni ya Mungu, acha anunue gari apate amani ya moyo, kukosa mafuta ya 20,000/ ni tofauti sana na kutokuwa na gari kabisa...
 
atahama mpaka wapi?,atakimbia mitaa mpaka lini?maisha ni leo,kesho ni ya Mungu,acha anunue gari apate amani ya moyo,kukosa mafuta ya 20,000/ ni tofauti sana na kutokuwa na gari kabisa...
Kuna wale wa mtaani utawasikia, UZA GARI KANUNUE MAFUTA..!! We mdanganye tu
 
Back
Top Bottom