mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Utaanza sasa kuitwa "baba mwenye gari" ingawaje "baba mwenye nyumba" ndilo jina lenye kusikika sana katika viunga vya miji mbalimbali.Japokuwa wanasema usifanye kitu kwa kuiga au kuhisi watu watakuonaje ila inafika point unaamua ufanye tu ili upate amani. Mimi ni kijana naishi Dar mshahara wangu ni kipato cha kati tu.
Ssasa hapa ninapoishi vijana wenzangu wote wana magari kasoro mimi sasa naona kama najifeel inferior sana, niliwahi omba ushauri humu JF wengi walinishauri nisinunue gari kwa kufuata mkumbo ila sasa naona uzalendo umenifika hapa.
Nimepanga kununua gari nina akiba yangu ya 4M bank na ninaenda kukopa 3.5M naenda kununua ist. Kwa mliokwisha kuwa na magari ya mikopo staili hii ni changamoto gani ninaweza kukumbana nazo na je utakuwa uamuzi sahihi?
Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app