Nimechoka, naenda kununua gari

Nimechoka, naenda kununua gari

Gari ni muhimu sana, kama una uwezo wa kununua na kulihudumia nunua tu.
 
Wengine watakwambia ukanunue kiwanja Kerege ujenge sababu ni asset.
Nunua ndinga hiyo leta heshima, binadamu hajawahi kukosa sehemu ya kulala, ila anakosa usafiri.
kama nimekuelewa hv mkuu
 
Japokuwa wanasema usifanye kitu kwa kuiga au kuhisi watu watakuonaje ila inafika point unaamua ufanye tu ili upate amani. Mimi ni kijana naishi Dar mshahara wangu ni kipato cha kati tu.

Sasa hapa ninapoishi vijana wenzangu wote wana magari kasoro mimi sasa naona kama najifeel inferior sana, niliwahi omba ushauri humu JF wengi walinishauri nisinunue gari kwa kufuata mkumbo ila sasa naona uzalendo umenifika hapa.

Nimepanga kununua gari nina akiba yangu ya 4M bank na ninaenda kukopa 3.5M naenda kununua ist. Kwa mliokwisha kuwa na magari ya mikopo staili hii ni changamoto gani ninaweza kukumbana nazo na je utakuwa uamuzi sahihi?

Kopa wala usiogope

Lakini kopa kene main fianancial instutions kama banks

Achana na hela za vikundi,microfinance na watu binafsi


Kwa taarifa yako hakuna tajiri ananunua liabilities kwa cash,hata hayo ma range wengi wamekopa na life linasonga

We vp bhn unaishije bila deni mjini apa[emoji23]

Kopa uongeze uwezo wa kufikiri utagundua mpk kipaji chako mradi deni liishe
 
Ukishanunua gari utaona ajabu yaani hutokosa hela ya mafuta, utapambana mpaka uipate kwa njia yoyote ile, huwezi amini siku nyingine napakiaga abiria wakati naenda job ilimradi nipate adjustment ya kuongezea mafuta.
We jilipue tu nunua mambo mengine yatafata.
 
C ununue tuh pikpik hilo gali l milion 7 mbn nd dharau zitazid kwan rafik zako wana magar y aina gan
 
Nimenunua gari sasa huu ni mwezi wa tisa toka ninunue gari na sijwahi kushindwa kuifanyia servicewala kuihudumia mafuta na ninaenda nalo kazini kila siku na weekend naenda nalo kutembelea....Kuwa na nia Mungu atafungua njia...Sasa ninampango wa kuupgrade kwenda kwenye crown
Ulinunua gari gani mkuu?
Crown ni mnyama.
 
Nimenunua gari sasa huu ni mwezi wa tisa toka ninunue gari na sijwahi kushindwa kuifanyia servicewala kuihudumia mafuta na ninaenda nalo kazini kila siku na weekend naenda nalo kutembelea....Kuwa na nia Mungu atafungua njia...Sasa ninampango wa kuupgrade kwenda kwenye crown
Ukinunua crown hiyo ya sasa uniuzie mimi mkuu.
 
Back
Top Bottom