Nimechoshwa na mada za Mbowe vs Lissu

Nimechoshwa na mada za Mbowe vs Lissu

Mfahamu sultan ibn mbowe king'ang'anizi
IMG-20241206-WA0083(1).jpg
 
Ajali zikwapi?
1736935388084.png

RPC Tanga na Mkuu wa Mkoa Batilda, walienda kushuhudia ajali.

Watu 11, wameuwawa na lori jana , Segera Tanga.
Walikuwa wameenda kushuhudia na kuokoa ajali iliyotokea awali.
Kuna kero nyingi za barabarani sasa hivi zinazoua watu wengi.
 
CHADEMA yenyewe inaelekea shimoni, hizi mada za Mbowe vs Lisu zimetuchosha.

N.b.
MODS: Hii si complaint, ni hali ya wana JF wengi, kuna kero nyingi kama ajali za kila siku.
Ni kweli lakini uchaguzi ukiisha Lisu akishndwa tu uchaguzi hizo mada hazitakuwepo tena

Team Lisu ndio kutwa wanapost mada humu
 
A anamuona B kama zuzu, kumbe A ni zuzu aliyekubuhu. Mtu kushindwa kuelewa mda wa kuondoka kwenye jukwaa ni "uzuzu kamili ".
Na ndio hiki kinawatesa binadamu kwenye kila angle ya maisha yao “kutokujua muda wa kuondoka” Walalamikaji simply ni watu ambao hawajui muda wa kuondoka.

Umeiweka kitaalamu sana mkuu.
 
CHADEMA yenyewe inaelekea shimoni, hizi mada za Mbowe vs Lisu zimetuchosha.

N.b.
MODS: Hii si complaint, ni hali ya wana JF wengi, kuna kero nyingi kama ajali za kila siku.
hii ni trend Lissu ndio habari ya mjini kwa sasa ndie anae trend,huwezi kumzuia,ni kama kuuzuia upepo kwa mkono au kuyazuia maji ya mkondo!。
P
 
CHADEMA yenyewe inaelekea shimoni, hizi mada za Mbowe vs Lisu zimetuchosha.

N.b.
MODS: Hii si complaint, ni hali ya wana JF wengi, kuna kero nyingi kama ajali za kila siku.
Kama hutaki habari za Lissu Kuna Majukwaa mengi tuu ndani ya Jamiiforums. Habari za Ajali sio jukwaa hili, hizo ni za Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko, ukitaka Mapenzi Kuna MMU, Kuna Jukwaa la Michezo, Mapishi, Elimu, Intelligence, Historia, Kilimo na Masomo and so much more for everyone.

Kuja Jukwaa la Siasa ni kiherehere chako tuu. Ni kama kuwa na irritating information inayotolewa na radio au TV fulani lakini badala ya kui skip hiyo radio au TV you keep switching on na utegemee habari tofauti. Badili chaneli utasikia habari tofauti. Ila hapa Jukwaa la Siasa Kwa Sasa na siku zote Habari Kuu ni CHADEMA na Harakati zao kuikomboa nchi hii kutoka mikono ya Mkoloni mweusi CCM.
 
Back
Top Bottom