Nimechukua mkopo benki, naomba ushauri katika namna niliyopanga kuutumia


Kila mtu ana test, interest na vitu anavyopenda, ukiyajua hayo utapunguza usumbFu na magomvi na watu yasiyo na lazina.
 
Mkuu na je kwa mfano Kama Nina nyumba yangu ambayo nakaa mwenyewe.
Na hyo nyumba hainiingizii pesa na wala hainipotezei pesa yaani iko neutral tu.
Nyumba hii tutaiita asset au liability?
 
Aisee ww jamaa una akili sana.
Yaani mm mwenyewe huwa nawaza hvyo yaani na ndio maana nachelewa kununua gari ingawa milioni kumi kumi huwa nakuwa nazo.
Vigari vya jamii ya IST,Spacio,Raum na vigari vingine Kama hvyo vinawafaa masistaduu wa mjini.
 
Tumia yote 30mil kununua gari SUV mambo ya wese usiwaze gari sasa zinatumua umeme zaidi, isitoshe jioni utakula vichwa za changia mafuta buku 2 kwa kichwa.
Mjengo achana nao, utajiseti huo baadae usiuache ushauri huu wala usiskilize ushauri mwingine, sasa ziba masikio
 
Mkopo huu si wa muda wa chini ya miaka 4, riba ni 19% kwa mwaka. Cumulatively atalipa kama sh 63mil hivi.

Gari atakuwa kanunua kwa tsh 30mil. Na kibanda kakianzisha kwa tsh 33mil.

HUU NI UZWAZWA.

Kopa kwa maendeleo ya biashara, sio kununulia liabilities.

Sawa Mwalimu?
 
Aisee ww jamaa una akili sana.
Yaani mm mwenyewe huwa nawaza hvyo yaani na ndio maana nachelewa kununua gari ingawa milioni kumi kumi huwa nakuwa nazo.
Vigari vya jamii ya IST,Spacio,Raum na vigari vingine Kama hvyo vinawafaa masistaduu wa mjini.
Aisee akili yetu moja mi nikitaka kununua gari nina nunua ambazo ni multipurpose unayoweza weka hata mkaa au ndizi nikienda uchaggani kwetu 😂😅 na hapo hapo naweza toka nayo.
 
Yani huyu mleta mada sijui atakuwa ndio yule ninae mfahamu mimi?

Maana kuna jamaa ni dereva kwenye ubalozi wa nchi flani, yeye kachukua mkopo wa mlion 30 kaenda kundelezea nyumba yake alafu nyingine kanunua gari subaru foresta, sasa aliniambia nyumba ameishia kupaua tu na hela imekata.
 
Dah

......... Ibaki pesa kidogo ya kula Bata [emoji22][emoji56][emoji22][emoji56]
 
...kwa hiyo Mkuu uliomba huo mkopo bila business plan yoyote ya kuzifanyia biashara hizo hela?
Marejesho ya mkopo utatoa wapi? Kwenye Mshahara?.. [emoji848][emoji848]
 
Hpna sio mimi
 
Duh yan kama bank wangenipigia mahesabu kam hyo yako ningeondoka bila kuaga. No research no right to speak
 
Aisee ww jamaa una akili sana.
Yaani mm mwenyewe huwa nawaza hvyo yaani na ndio maana nachelewa kununua gari ingawa milioni kumi kumi huwa nakuwa nazo.
Vigari vya jamii ya IST,Spacio,Raum na vigari vingine Kama hvyo vinawafaa masistaduu wa mjini.
Hayo ni mawazo yako binafsi
 
Nunua kagari kalikozeeka (usipende ufahari sasa) bei isizidi mil. saba. Fungua vitega uchumi vingine viwili visizidi milioni 10 kila moja ubaki na milioni kwa dharura usizitumie kabisa. Hela za kumalizia nyumba zitoke kwenye vitega uchumi vipya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…