Nimechukua mkopo benki, naomba ushauri katika namna niliyopanga kuutumia

Nimechukua mkopo benki, naomba ushauri katika namna niliyopanga kuutumia

Ninavyo faham kwa Ulaya mtu akiajiriwa moja ya mambo ya kwanza ni kupewa mkopo wa kununua gari kama hana na cha pili unapewa mkopo wa kukodi nyumba/kulipia nyumba.
Kwa mtazamo wa Waafrika walio wengi, huona gari kama anasa ila gari ni kitendea kazi kinachoweza kumuongezea mtu MUDA na hivyo kumuongeza kipatato.
Angeongelea GARI kama v8, prado nk hapo tungeweza kuona ni anasa
Sijamshauri mtoa mada ila ningependa kuliweka hili la gari vizuri
Usifananishe ulaya na bongo mkuu.
Ulaya mtu anapoanza kufanya kazi mshahara anaopata unakuwa ni mkubwa na umepigiwa hesabu kwa matumizi ya mahitaji yote.
Huwezi kulinganisha na bongo ambapo mishahara ni ya kunyonyana tu hata basic needs tu haijazingatia.
Kwa hayo mawazo uliyoyatoa hapo kwa huku bongo hata mkurugenzi akiyafuatisha anahangukia pua.
 
wekeza kwenye biashara.. kama unaona huna akili ya biashara kanunue viwanja vya kutosha kwa maisha bora ya baadae
 
Ulipaswa kuomba ushauri kabla hujachukua mkopo, sasa umeshachukua ndio unaomba ushauri, wa nini wakati ulishajipanga kitu cha kufahya?
 
Habari zenu

Nimekopa shilingi milion 30 bank CRDB. Nahitaji kununua gari mojawapo katika hizi IST, ALEX, RACTIS, CARINA na pesa itayobaki nikamalizie mjengo wangu chanika (15MIL) na ibaki pesa kidogo ya kula bata. Je, mpango wangu unafaa?

Naomba ushauri wadau

NB: Nimechagua hizo gari kwa ajili ya matumizi madogo ya "wese"

Sent using Jamii Forums mobile app
Ina maana umechukua mkopo ila hujui vizuri ufanye nini na huo mkopo?
 
Kina msemo; Kama hudaiwi huna akili.
Jamaa anaogopa kuitwa kilaza.
Alipoona kabanwa kwa idea yake akajiongeza na kusema ooh nina vitega uchumi na huku anasema mshahara huwa siugusi kabisa
Sasa najiuliza kwanini ukope wakati mshahara haugusi na vitega uchumi vina generate cash
Well kila mtu ana maamuzi yake lakini anaeleta mawazo yake humu lazima apate comments za kila aina
 
Alipoona kabanwa kwa idea yake akajiongeza na kusema ooh nina vitega uchumi na huku anasema mshahara huwa siugusi kabisa
Sasa najiuliza kwanini ukope wakati mshahara haugusi na vitega uchumi vina generate cash
Well kila mtu ana maamuzi yake lakini anaeleta mawazo yake humu lazima apate comments za kila aina
Kitega uchumi cha kunipa mil 30 cash sina. Mimi similiki viwanda .hio hela ya mkupuo utaipata kirahis? Ungeuliza kitega uchum gan
 
Ulipaswa kuomba ushauri kabla hujachukua mkopo, sasa umeshachukua ndio unaomba ushauri, wa nini wakati ulishajipanga kitu cha kufahya?
Ningeomba ushaur humu wengne wangesem nichukue wengine wangesema no.. sasa nimeamua kuchukua na hayo ndio mahitaji yangu nimeomba ushaur utakaonipendeza nitaufata
 
Bwana mdogo,..mil30 ni hela ndoogo sana ukiishika amini nakwambia,na sikushaur ufanyie biashara hyo hela sabab kwa ulivyo ulivyo tuu nmeona hutoweza,tuanzie hapo kwanza,so hako ka 30 kama ulivosema unataka gar na kumalizia nyumba na hela ya bata,..naona umejitoa muhanga,first of all ushafel so ngoja nikushaur kutoka kwenye hyo failure,..

Subir had december kuna yard nying tu hua wana ofa,mfano pale namanga ile yard ya wa pakistan,acha mbwebwe za IST ziko juu sana mpya,na usinunue gar mkonon,utakuja juta,..nenda pale yard tafta ractis or fun cargo or gar yoyote utakayokuta ,hua ofa znafika had 7.5m..kwa sis wateja wa kudum hua tunapigiwa sim kabsa,kuna gar hii na hii zna ofa..usinunue zaid gar zaid ya m9..then hela inayobak malizia tuu nyumba hyo,namaanisha hela yoteee,usiweke hela ya bata sabab bata hyo na wenge la hela,utapata majanga,ajali,kuibiwa,etc utarud nyuma utatumia hela zilizobak kujiuguza,so hela yote malizia ujenz,tenga 15mil,tafta fund ,tumia budget ndogo uwezavyo,..vifaa vyote nenda dukan usitume mtu..mil6 iliyobak weka bank ipige fixed,huku ukitafta kamrad kakukuingiza sh mbil tatu


Nmeshaur kutokana na experience

Sent using Jamii Forums mobile app
Yard gani hiyo mkuu?
 
Mkuu hela ya mkopo iheshimu sana usije ukaweka rehani familia yako, Ohoo!
 
UNGEOMBA USHAURI KABLA YA KWENDA KUCHUKUA MKOPO NA SIO UCHUKUE KWANZA, UNGEOMBA USHAURI KUHUSU MATUMIZI NA SI UOMBE USHAURI BAADA YA KU AINISHA MATUMIZI YAKO, SASA UNATAKA USHAURI UPI TENA NA UMESHAPANGA KILA KITU. TUKIKUSHAURI UTAKUBALIANA NA USHAURI WETU? HAYA TUNAKUSHAURI RUDISHA HIZO PESA ZOTE CRDB BENKI WAELEZE SIHITAJI TENA MKOPO WENU, BADALA YAKE WEKEZA KIDOGO KIDOGO KWENYE KIPATO CHAKO ILI UWEZE KUTIMIZA MAHITITAJI MENGINE, AU ACHANA NA MIPANGO YOTE KUHUSU MATUMIZI YA HIZO PESA TUTAKUPANGIA SISI LA KUFANYA. UNASEMAJE MKUU.
Wabongo vichwa vizito sana kuelewa,haya ndio madhara ya kula ugali hovyo hovyo
 
Kitu chako chochote kile ambacho kinakugharimu basi kitu hicho ni liability (dhima) na ambacho kinakuletea mkwanja basi hicho ni asset (mali).

Kama nyumba na gari lako zina kugharimu pesa, financially speaking tutaziita ni liabilities. Lakini kama una nyumba nyingine zina wapangaji na unakusanya kodi tutaziita nyumba hizi assets, hali kadhalika kama una magari mengine yanayokuletea kipato, magari hayo pia ni assets.

Chacharika ili uwe na assets (mali) nyingi kuliko liabilities (dhima). Hapo utakuwa umetoka kwa kiwango cha lami.
 
Back
Top Bottom