Yuko sahihi... Fanya vitu unavyovijua na unaweza kusema ulifanya nini kwa hela yako ya mkopo... Mawazo afungue biashara, sio kwa hela ya mkopo huo.. Ndio maana benki, wamemkopesha kama mfanyakazi.. siyo mfanyabiashara.
Kiuhakika, ukitaka kuweka kwenye biashara, atataka kuweka hela nyingi kiasi.. Atajikuta amelipa kodi ya fremu, mshahara wa mfanyakazi, ulinzi, leseni ya biashara, kodi TRA, malighafi za kuanzia biashara.. Kufumba na kufumbua almost nusu ya pesa imekwisha na hakijaeleweka.
Nunua gari lako dogo, uzidi 10 m....malizia nyumba ... Fanya biashara ndogo ya mtaani , kama banda la chipsi au upikaji wa vitafunio.. Utatoka tu na maisha yanaendelea bila presha.