Nimedahiliwa na chuo kikuu nchini ila kutokana na hali iliyo nje ya uwezo wangu nimeshindwa kujiunga, naomba msaada wa mawazo

Nimedahiliwa na chuo kikuu nchini ila kutokana na hali iliyo nje ya uwezo wangu nimeshindwa kujiunga, naomba msaada wa mawazo

Joined
Nov 30, 2020
Posts
31
Reaction score
15
Ushauri tafadhali, nimepata udahili wa chuo kikuu fulani hapa nchini.

Sasa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu nimeamua kuhairisha kuripoti chuo hicho.

Nauliza endapo sitasitisha (cancel) hii application mwakani sitakuwa na vigezo vya kuomba tena?

Kama mwombaji mpya kwa vyuo vyote nchini kulingana na ufaulu wangu.
 
Kwa akili hizi Hukustahili kudahiliwa chuo kikuu
 
Sasa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu nimeamua kuhairisha kuripoti chuo hicho.
Njia uliyoitumia kusajiri tumia hiyo hiyo kuahirisha.
Sisi wazamani tuna ahirisha, sasa vijana wetu wao wana hairisha, wasiwasi wangu wajukuu zetu huenda wakaharisha (LoL).
Naona kiswahili kinazidi kuwa changamoto, hapa nyumbani kwangu hilo ni tatizo kubwa lakini hata JF kwa ujumla kiswahili kinakwenda mrama. Walimu, wazazi na jamii tunawajibu........ hapa.
 
Kwanini kiswahili kigumu kiongozi
 
Swali fikirishi: kwa nini unataka kwenda chuo? Ukafanye nini? Ili iweje? (usiniambie unataka kwenda kusoma)
Ukinijibu haya sasa twaweza kushauriana!.
Saws Mr.genius hii ndio sababu ya kuhairisha pia,ila wasiwasi Wangu niendapo nitapata udahili tena mwakani
 
Back
Top Bottom