Nimedhulumiwa/ kutapeliwa na tajiri na sioni pa kumpeleka

Mzee yaani miezi minne yote unapiga kazi hulipwi wakati hapa tu nilipo mwezi uliopita nilisaka gari nyingi sana kwa ajili ya tenda ya kupeleka mzigo kiwandani nikazipata kwa mbinde, kumbe kuna watu mna gari za uhakika zinasota.
Kama bado zimepaki naomba unishtue tuone tunafanyaje. Miezi MINNE HULIPWI NA BADO UNARUHUSU GARI ZIFANYE KAZI? Huo ni uzembe.
WhatsApp 0755963775
 
Komaa nae tu hakuna namna
 
Mkuu we chukua lori zako, ingiza sehemu nyingine kashakuzunguka huyo
 
Nitafute mkuu nikupeleke kwa mzee Mmoja wa kuitwa makombo ya gari, historia yake huyo mzee alipinduka na gari mara kumi na zote hajawahi hata kuchunika, yani huyo tajiri tunamtoa jipu la ulimi mchana kweupee na atakuja mwenyewe kuomba msamaha
[emoji16][emoji16]
 
bado napata ukakasi kdg.....umeweza kuwekeza kwa kununua 6 volvo trucks, mpya/used no matter,,, sio pesa ya kitoto....then unaingia mkataba usio na paper...( sijui kama mlikuwa nao).........mpuuzi mliyekubaliana anatumia lorry zako bure, unakuja hapa kulia lia....sitaki kukubali wewe ni MPUMBAFU grade 1!!!!!...sijui ni sh ngapi but bado nasema wewe ni pumbafu.....umekosa hata mwanasheria wa kukupambania kweli......tafuta mwanasheria mpe ishu.....force mahakamani.....tafuta docs zote (gate pass zenye namba ya gari)....mpelekee notice....unalipwa japo kwa mbinde....tengeneza fitina kuanzia kwenye mmiliki wa mgodi wenyewe.........hakuna wa kukupigania haki yako....pigana mwenyewe wanasheria wanamalizia.....usiwe zoba......sometimes unatakiwa kuwa na roho mbaya ...tena mbaya mno....
 
Jaribu kuwambia watu wake wa karibu anaowaheshimu anawezaa kuwasikiliza ukambulia chochote kitu. Note jaribu
Kwenda taratibu na malori yako mana ujio wako wabobezi wa sector hizo wasije wakayatumia wakayawachosha ukajikuta umenunua vituhavija kunufaisha.
 
Mbona ishu ndogo.
Kachukue RB umtie RUMANDE mwenyewe akili itamkaa Sawa.
Usiogope .
Matajiri wanaogopa rumande kinoma
 
Chagua:

1. Sheria (possibity ni ndogo kutoboa)
2. Kumshughulikia wewe binafsi kwa mbinu zako.
3. Mganga (uchawi)
4. Genge la wahuni.
5. Maombi (kama una ushirikiano mzuri na Mungu na upo vizuri kiroho.

Hakuna kinachoshindikana ukiamua. Ni mali yako. Ipambanie. Kama vyote huwezi kaa kimya endelea na maisha yako.
 
ngongoti2000 kama nilivyoandika kwenye mada husika nilikuwa mchanga kwenye hizi sijajua wap sijaeleweka
Mliandikiana mkataba? Jibu hilo swali ndio au hapana.

Ukikomaa tu kwa kusema ulikuwa mchanga watu hawataelewa wanakusaidia kuanzia wapi??

Tuambie mkubaliano yenu mliyafikia kwa njia gani??

Mlikubaliana kulipana kwa njia gani?? Malipo yako ya kwanza alikulipa kwa njia gani??

Elezea kidogo unaweza pata msaada.
 
Mikataba au makubaliano mnafanya kiholela, bila wanasheria?
 
Njoo mwanza nikupe mtaalam amshughulikie..

Nakuhakikishia atanyooka
 
"Listen to your internal voice it already know where you want to go".

" If you can't decide the answer is no"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…