Nimedhulumiwa MilionI 10, siku ya Tano sasa sijapata Usingizi

Pole mleta, vumilia kwa sasa kwa huna taarifa yoyote na mwachie Mungu, endelea kupambana na maisha ilimradi una nguvu na afya, mwombe Mungu atakupa nafasi nyingine.
 
Sijui ni mimi tu ndo naona hivi au wote wanaona hivi... Ninavyoona ni kama vile hii post yako imeandikwa na watu wawili tofauti... wakwanza ameishia kwenye 'hypothesis moja tu' halafu mwingine ndo akamalizia hii post..

Kuna busara mbili tofauti ndani ya hii post
 
Pole sana mkuu...Siku zote tunajifunza kutokana na makosa lakini makosa mengine yanaumiza sana...Hata mimi nilijifunza kutoamini the so called washikaji kwa kupoteza hela lakini haikuwa hela nyingi kama yakooo...Pole sana mkuu..Inaumiza lakini jitahidi kucontrol mawazo..maana the more unazidisha mawazo ndivyo unaweza jiletea matatizo mengi sana ya kiafya ambayo yatakutesa siku nyingi zaidi...pole sana mkuu..​
 
[emoji16][emoji16],mtu mmoja sema mood/minds mbili. ....kulingana na muktadha husika
 
Pole mkuu hii ndiyo dunia kuwa uyaone sasa umeshajifunza usiamini mtu yeyote mbele ya pesa!!!
 

Nakurekebisha hapo! Hata ndugu anaweza kukuzima na akatokomea kusikojulikana

Niliwaza nikushaur uende kwa waliowapa mradi labda kuna vitu viko nyuma ya pazia
 
Pole sana Mkuu issue kama hii ilinitokea mimi aliondoka na mil 30, nilimtafuta nikampata nikamwambia nipe changu akagoma, nilipiga moyo konde japo kwa maumivu makali sana nikasamehe, hauwezi amini jamaa sasa hivi ni amechoka vibaya mno hana kitu leo ananiomba mia tano ya nauli, maisha haya acheni tu kutapeliwa na mtu wa karibu kunauma kinoma, unakuwa unajiuliza kwanini huyu anifanyie hivi ila ndo imeshatokea, piga moyo konde samehe kama unaweza kubali umepoteza tu utapata amani ya nafsi kuendelea kuwaza utaumiza afya yako.
 
Nipe tender ya kumtafuta.

Malipo ni milioni 2 tukifanikiwa.

Nipe taarifa kamili inbox

Majina yake kamili na picha zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…