Nimedhulumiwa MilionI 10, siku ya Tano sasa sijapata Usingizi

Nimedhulumiwa MilionI 10, siku ya Tano sasa sijapata Usingizi

Hana pesa uyo mkuu, hela imeisha hiyo tena anaweza kuwa karudi bongo tayari..pole sana
 
Mrejesho Mfupi wadau;

Baada ya kumtafta sana jamaa bila mafanikio, mwaka jana mwezi wa 12 alinitafuta yeye mwenyewe whatsap kwa namba mpya akaniambia aliitumia ile pesa kwenda South Africa kutafuta maisha, akanitumia na picha zake akiwa huko South na akaniomba sana msamaha(kitu cha kijinga tu ofcoz) na aka ahidi akirudi bongo atanirudishia hela yangu nimuwie radhi sana.

Nilimwambia "mzee bado sijakusamehe na sitokusamehe, nataka hela yangu kabla ya mambo mengine yote".

So najua now ata yeye huko alikokwenda ni kama aliitupa tu hio hela instead angeitumia hapa hapa bongo labda kuna uwezekano ingezaa, maana ukipiga hesabu hapo siku za kwanza kwanza tu kwenda South ni wazi nusu ya hela iliishia kwenye nauli na accomodations na ushamba wa mji tu.

Tukio hili limenifanya nijiulize maswali mengi sana, moja ni; inakuaje kijana wa umri wa miaka 30 ana waza kwenda kwenye nchi ya kiafrica kutafuta maisha sehemu ambayo ni very dangerous na kuna vitisho vikubwa vya mauaji kwa raia weusi wa kigeni? au shetani kazi yake kukupa ramani, matamanio alaf ana kuseti ufe? So sad.
Aisee huyo ni kenge kama Ontario tu
 
Na mbaya zaidi sidhani kama uchawi unavuka anga la nchi zaidi ya 2....

Huyo ungefungua jalada polisi then interpool wadili naye....
 
Huyo jamaa ni stupid age ya 30 unaenda south africa. Si bora angenunua ubber akawa KILA mwezi anakupunguzia.
 
Brothe me mwaka wa Tatu huu nimedhulumiwa gari na alienidhulum yupo mjini na nakutana nae Sana na haki yangu nilisema sina cha kumfanya Ila namuombea Dua mbaya Kila Siku Sasa Hivi anamadeni mpaka kichwani
 
Huyo ni wa RADI. Nenda Kigoma au Sumbawanga kwa 500k bila hata manyunyu wanamalizana tu
 
Niliungana na rafiki angu tukaunda timu na tukafanya project na kampuni ya wa Asia, project tuliifanya kwa muda wa miezi tisa. Na hapa kati hakukua na malipo ya ziada au ya kazi zaidi tu ya malipo ya vitu vinavyohitajika wakati wa Project hasa accomodations na transports tu.

Huyu jamaa yangu ni kama ndugu kabisa, tulikuwa na urafiki unaovuka mipaka, the guy was so deep na alikuwa Loyal yaani ni rafiki yule wa haswa haswa, rafiki ambae tumeshibana na tunaelewana mno mno wazee.

Hapa kati wakati Project inaendelea kuna wakati tuligombana na wabongo ambao walikuwa ni mamluki kwenye kampuni ilo la wa asia, huyu mshikaji wangu ndio aliwazingua sana baadae nikaingilia kati tukali-solve ilo tatizo na tukawa peace tena.

Sasa kuna wakati nilisacrifice kazi zangu za nje kibao ili tuisimamishe hii project sababu at the end of the day tulikuwa tunapata faida ya milion 20+ na tuko mtu mbili tu, so nikiwa na vimeo vingine nje (nna kazi nyingine nje tofauti na hii) nawaachia watu wengine wanifanyie kwa niaba.

Long story short, project iliisha salama sasa tukawa tunaanda bills na documents zingine ili wa asia watulipe hela zetu, so mshikaji wangu amesomea haya mambo ya uhasibu so ikawa kazi yake kuandaa then mwisho wa siku tupeleke na tukiwa tume attach na account zetu za malipo, mie nikapata kazi (kama nilivyosema nina kazi nyingine nje ya project) ambayo ilikuwa inanilazimu niende Dodoma kuikamilisha siku hiyo.

Mazee huyu rafiki yangu ameshirikiana na wale wabongo wenzetu kwa wa asia wamempa hela yote huyu rafiki na sijui makubaliano yao au walipeana shingapi ila ndugu rafiki amekimbia na hela zote na hajulikani alipo, too sad hela alipewa cash (imagine) na mafacilitator ni hawa wabongo wenzetu wa kwa waasia. Jamaa hayupo popote ndani ya mji huu wa Dar.

Bado napambana kumpata na nimeshachukua hatua kubwa ya kumtafuta popote alipo ndani ya nchi hii, ila nimejiuliza maswali mengi sana na ambayo yamepelekea leo siku ya tano tunaenda sipati usingizi kabisaa na kila saa moyo wangu unauma na kuumwa kama vile kila siku naumizwa upya.

1. Ni kitu gani kimempata huyu ndugu yangu? Hustles zote zile tukiwa nae hakumbuki? Hakumbuki namna alivyokuwa irrelevant kwenye hii project na namna alivyochangia padogo sana kiasi hata asingekuwepo mradi ungesimama japo yeye ndio alilileta ili tenda? Why amesahau nafasi yake kwenye hili?

2. Ubongo wa mtu mdhulumati huwa unawaza nini kichwani? Yaani future yake huwa anaiona vipi? Anapata usingizi huko alipo? Is he happy? For how long?

3. Unawezaje kumsaliti rafiki yako ambae yuko loyal kwako? Hizo ni akili gani na roho ya namna gani hiyo?

4. Kwanini watu wengi wanakosa ubinadamu na haki pale hela zinapokuja? Je ukichukua haki ya mtu unadhani na yeye hato react back?

5. Nimfanye nini huyu mtu? Mbona nna haki zote hata nikiwafuata wataalam wa radi kwenye hili hawatosita kunisaidia tena bila masharti! Je mdhulumati huko aliko kama atakufa au akipata matatizo ambayo akiyaona sio kawaida atafanya nini?

Mwisho kabisa, nimeumizwa sanaa na maamuzi ya ndugu rafiki na nimekwama sanaa ktk kipindi hiki hasa nikikumbuka ile sacrifice na hustles za days and nights na ningeomba nitoe angalizo tafadhali, mtu kama hakuzaliwa na wewe usimwamini kwa namna ya aina yoyote ile sababu uliezaliwa nae atleast kuna sehemu unaweza kumkamata.
Pole sana mkuu,ubinadamu kazi sana!
 
Mkuu nimeokoka mbona, huu utambulisho ni ukumbusho tu kwamba bwana yule yupo!
shida ni kuwa imekuwa kama umemkubali na unamtukuza! Dunia ya leo inamtaja zaidi antiChrist kuliko Christ mwenyewe. Hili ni tatizo.

JESUS IS LORD
 
watu wengine bana,yaani 10m ndio hela ya kukimbia kweli?! Halafu usiamini mtu kabisa hata kama ni baba yako
 
Mpuuzi tuu, sasa million 20 ndio ya kuvunja urafiki. Itaisha sasa hivi, uso wake atauwrka wapi?
 
Pole sana! Next time hakikisha kila unalolofanya ata na Baba ako au mama mzazi,rafiki na ata mke kuwepo na mikataba ya kisheria kukulinda! Mdogo angu alikuwa anatabia ya kuttust friends na ndugu alikuwa anakula za uso tena kubwa tu kushinda wewe ya hii 10 M jipe Moyo Dogo alipambanaga now yupo sawa na akuna anaemdhurumu tena na mazurumati wake wote alikuja deal nao na akapata haki zake mfano wake mmoja ni huu! Japo alipigwa tena kama mara 3 hivi ndipo alikuja kaa sawa😁
 
Back
Top Bottom