Nimedhulumiwa MilionI 10, siku ya Tano sasa sijapata Usingizi

Nimedhulumiwa MilionI 10, siku ya Tano sasa sijapata Usingizi

Wakuu nawashukuruni sanaa, meseji zenu zimenifariji sanaa, nimefarijika kuona kuna wengine wamewai kupoteza vikubwa sanaa zaidi yangu, bado naendelea kujifunza taratibu ntaanza kurecover ila moyo wa kusamehe sidhani kama nnao ila ntasahau tu. Shukrani sana🙌🏾🙏🏾
 
Kuna mwamba humu aliwahi kutoa tangazo la kulaani kunyimwa haki na hakimu mmoja halafu akatoa na siku kadhaa za matazamio.......The rest is the subject which deals with past events.....
Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri jamaa anaitwa mng'oa kucha
 
Halafu humu kuna ID za kitapeli zinajiuliza na kujijib....humu jf inabidi ufungue macho matatu ndo utaweza kushtukia huu mchezo[emoji848][emoji848]
 
Kuna mwamba humu aliwahi kutoa tangazo la kulaani kunyimwa haki na hakimu mmoja halafu akatoa na siku kadhaa za matazamio.......The rest is the subject which deals with past events.....
Nakumbuka kilichofuata ilikuwa tanzia kutoka idara ya Mahakama.
Niliogopa SANA, aisee! Na muda alitaja.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Pole sana.

Umemuamini sana, ulitakiwa ku verify na kuwa karibu kwenye ku finalize malipo.

Inawezekana ikawa bora umemjua mapema, usiwe naye kwenye deal kubwa zaidi.

Whether utapata au hutapata hela zako, hesabu hili kama funzo. Inaonekana wewe mtafutaji na utapata pesa nyingine tu, epuka kuamini watu sana tatizo hili lisijirudie.

Never underestimate people's greed or overestimate their virtues.
Mi ntamuamini mtu nalala naye kitanda kimoja... kazini enyewe kuna watu nimefanya nao kazi miaka 4 ila bado siwaamini... verification ni muhimu sana
 
Pole Sana Boss.
Hawa marafiki aisee, jamaa tunapambana, tuna hussle pamoja kumbe kuna Muda ananizunguka anakimbia nyumbani kumtongoza wife.


Marafiki sio wa kuamini Sana hasa hawa wanaojinesha wako loyal.
 
Nakumbuka kilichofuata ilikuwa tanzia kutoka idara ya Mahakama.
Niliogopa SANA, aisee! Na muda alitaja.

Everyday is Saturday............................... 😎
Yule jamaa huwa natamani sana nimfahamu. Kiboko ya dhulma. Dawa ya watu wanaodhulumu watu ni kumalizana nao tu
 
Alikua ni kijana wa gheto tu maana alifukuzwa kazi akashuka sanaa kiuchumi na hii project ndio ilimpa walau nafasi ya pili, anapokaa nilifika na vitu alivyoviacha thamani yake haizidi au haifiki milioni moja.

Kipi kilichosababishwa afukuzwe kazi!?
 
Sisi ni marafiki, alikua na kazi nzuri baadae akafukuzwa alishuka sanaa sanaa, akaanza upya... hii project yeye ndio mwanzo alini invite kwakua alikua hana hizo sifa zote timilifu zilizokua zinahitajika.
Mkuu Mimi nilipata tatizo linalofanana na la kwako miaka 2 iliyopita.Mbaya zaidi Mimi nilidhulumiwa na ndugu yangu.Ushauri wangu ni kwamba chukulia tukio hilo kama fundisho,achana na mawazo ya kulipiza kisasi hayana maana yoyote.Pesa zinatafutwa,utapata zingine,samehe na sahau.
 
Niliungana na rafiki angu tukaunda timu na tukafanya project na kampuni ya wa Asia, project tuliifanya kwa muda wa miezi tisa. Na hapa kati hakukua na malipo ya ziada au ya kazi zaidi tu ya malipo ya vitu vinavyohitajika wakati wa Project hasa accomodations na transports tu.

Huyu jamaa angu ni kama ndugu kabisa, tulikuwa na urafiki unaovuka mipaka, the guy was so deep na alikuwa Loyal yaan ni rafiki yule wa haswa haswa, rafiki ambae tumeshibana na tunaelewana mno mno wazee.

Hapa kati wakati Project inaendelea kuna wakati tuligombana na wabongo ambao walikuwa ni mamluki kwenye kampuni ilo la wa asia, huyu mshikaji wangu ndio aliwazingua sana baadae nikaingilia kati tukali-solve ilo tatizo na tukawa peace tena.

Sasa kuna wakati nilisacrifice kazi zangu za nje kibao ili tuisimamishe hii project sababu at the end of the day tulikuwa tunapata faida ya milion 20+ na tuko mtu mbili tu, so nikiwa na vimeo vingine nje (nna kazi nyingine nje tofauti na hii) nawaachia watu wengine wanifanyie kwa niaba.

Long story short, project iliisha salama sasa tukawa tunaanda bills na documents zingine ili wa asia watulipe hela zetu, so mshikaji wangu amesomea haya mambo ya uhasibu so ikawa kazi yake kuandaa then mwisho wa siku tupeleke na tukiwa tume attach na account zetu za malipo, mie nikapata kazi (kama nilivyosema nina kazi nyingine nje ya project) ambayo ilikuwa inanilazimu niende Dodoma kuikamilisha siku hiyo.

Mazee huyu rafiki angu ameshirikiana na wale wabongo wenzetu kwa wa asia wamempa hela yote huyu rafiki na sijui makubaliano yao au walipeana shingapi ila ndugu rafiki amekimbia na hela zote na hajulikani alipo, too sad hela alipewa cash (imagine) na mafacilitator ni hawa wabongo wenzetu wa kwa waasia. Jamaa hayupo popote ndani ya mji huu wa Dar.

Bado napambana kumpata na nimeshachukua hatua kubwa ya kumtafuta popote alipo ndani ya nchi hii, ila nimejiuliza maswali mengi sana na ambayo yamepelekea leo siku ya tano tunaenda sipati usingizi kabisaa na kila saa moyo wangu unauma na kuumwa kama vile kila siku naumizwa upya.

1. Ni kitu gani kimempata huyu ndugu yangu? Hustles zote zile tukiwa nae hakumbuki? Hakumbuki namna alivyokuwa irrelevant kwenye hii project na namna alivyochangia padogo sana kiasi hata asingekuwepo mradi ungesimama japo yeye ndio alilileta ili tenda? Why amesahau nafasi yake kwenye hili?

2. Ubongo wa mtu mdhulumati hua unawaza nini kichwani? Yaani future yake hua anaiona vp? Anapata usingizi huko alipo? is he happy? for how long?

3. Unawezaje kumsaliti rafiki yako ambae yuko loyal kwako? Hizo ni akili gani na roho ya namna gani hio?

4. Kwanini watu wengi wanakosa ubinadamu na haki pale hela zinapokuja? Je ukichukua haki ya mtu unadhani na yeye hato react back?

5. Nimfanye nini huyu mtu? Mbona nna haki zote hata nikiwafuata wataalam wa radi kwenye hili hawatosita kunisaidia tena bila masharti! Je mdhulumati huko aliko kama atakufa au akipata matatizo ambayo akiyaona sio kawaida atafanya nini?

Mwisho kabisa, nimeumizwa sanaa na maamuzi ya ndugu rafiki na nimekwama sanaa ktk kipindi ichi hasa nikikumbuka ile sacrifice na hustles za days and nights na ningeomba nitoe angalizo tafadhali mtu kama hakuzaliwa na wewe usimwamini kwa namna ya aina yoyote ile sababu uliezaliwa nae atleast kuna sehemu unaweza kumkamata.
Mungu akupe moyo wa subra,ndo Mana watu wanachuk
 
Pole ndugu vuta subra na angekuwa ana ku copy kwa email na scanned bills mpaka final Transaction.
Ila Ni upumbavu kukimbia na ku risk dhulma ya 5m inaweza kuteketeza familia yake .
Tujifunze kuwa na hofu ya Mungu.
Someni habari za Yezebel jinsi maiti yake ilivyoliwa na mbwa kwa issue yake tu ya forgery.

Kaka fuata sheria na ukiona wanakuzungusha Basi chukua sheria mkononi
 
Mkuu tafuta mtaalam,
Amtupie kijini shoga.

Jamaa yako akiona wanaume awe anakata viuno hadharani..

Mloge tu,

Hakuna jinsi ,
*****.

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom