Nimedhurumiwa Tsh. Milioni 2.4 na Mtu niliyekuwa nafanyanae biashara

Nimedhurumiwa Tsh. Milioni 2.4 na Mtu niliyekuwa nafanyanae biashara

Physical Address yake unaijua? Kama huijui ukefanya uzembe..Jifunzeni kufanya due deligence kwa wateja mnaofanya nao bishahara
Mm nipo dar yeye yupo mkoani- alisema yupo katoro hata mizigo niliokua namtumia nilikua naandika jina lake na sehemu hio katoro ila tulionana mtandaoni (mara yakwanza alinitumia laki 9 bila hata kuniona) alituma kama advance
 
I

Issue ni mbinu ya kuipata hela yake.

Sasa akimroga, fedha yake ataipataje?

Jaribu kuyafeel maumivu anayoyapata mwenzako ili umshauri kwa hekima.

Si unayaelewa maumivu yatokanayo na kuibiwa, kutapeliwa ama kudanganywa?

Nimemshauri vizuri sana.
akimroga vizuri akawa akapata mateso donda na kuwa anakumbuka ubaya alioufanya na tiba iwe ni kurudisha pesa!?!
kila ushauri unafaa inategemea mtu na mtu
 
Habarini humu ndani

Nimekuja kwenu najua nitapata msaada

_Kuna mtu nimefanya nae biashara bila kuonana nae ila alikua amejenga uaminifu mkubwa kwangu
- Maana alikua anatuma hela (advance) natengeneza mzigo namtumia kisha ananimalizia pesa iliobaki

Baadae akanambia nimtumie mzigo (mzigo nilikua naitumia karibu na shekilango) yeye yupo katoro

akanambia nikifika sehem ninayotumia mzigo kuna mtu atanipa namba zake niwasiliane nahuyo mtu atanipa pesa yahuo mzigo (huyo mtu yupo kariakoo)
nikaona sawa kwakua nishamuamini haina shida

mzigo nikaufikisha pale muda ule nafika gari nayo inataka kuondoka so mzigo mojakwamoja ukatiwa kwenye buti gari ikaondoka

Nikawa nampigia jamaa niliepewa namba yake ili anipe pesa yamzigo wangu . kutoka saa tisa jioni nampigia anakuja kupokea simu saa mbili usiku.

Anasema nilikua mbali nasimu .pesa yako nimepewa ila naomba tuonane kesho nikupe maana saiv nishafunga duka (maneno yake) nikasema sawa

kesho yake hakupokea simu mwisho ikawa haipatikani kabisa
_ Nikamrudia niliefanya nae biashara. akasema bas kama hapatikani hio pesa nitakulipa mimi mwenyewe

Ilikua 23/7/2026 (mwezi uliopita) mpaka leo 13/8/2026 namba zao wote hazipatikani

huyu niliefanya nae biashara anapatikana whatsapp tu kila siku anasema kesho kesho online anaingia siku anayotaka yeye
-Biashara anafanyia katoro (kwamaelezo yake) sijawahi kuonana nae hata picha yake sina

najua kwaupande wangu nimefanya makosa lakini tayari ishatokea hivyo .

Naomba msaada wenu nitumie mbinu gani ili niweze kuipata pesa yangu


AHSANTE
Dawa ni moja,je hizo sms zake au mlipokuwa mnaongea ulisevu sauti?Kama hukusevu chochote fanya maongezi nae kistaarabu tu ili akulipe.Kama ulisevu haya mawasiliano mfikishe polisi
 
Watanzania tunakwamishana kipumbavu sana, polisi ilitakiwa wawe serious sana kwenye issue za namna hii maana dunia sasa ishatoka kwenye biashara ya mazoea, kwasasa mambo yote mtandaoni, bahati mbaya zaidi hii "fursa" kwa nchi yetu wameiwahi matapeli kiasi kwamba inatuharibia sana wafanyabiashara kuaminika
 
Watanzania tunakwamishana kipumbavu sana, polisi ilitakiwa wawe serious sana kwenye issue za namna hii maana dunia sasa ishatoka kwenye biashara ya mazoea, kwasasa mambo yote mtandaoni, bahati mbaya zaidi hii "fursa" kwa nchi yetu wameiwahi matapeli kiasi kwamba inatuharibia sana wafanyabiashara kuaminika
yaah kunawatu wanatuma pesa china wanaagiza bidhaa bila hata kuwaona wachina mambo yanaenda bila shida tu japo changamoto hazikosekani
 
Shida ni kuwa ufuatiliaji wa hiyo pesa utakughalimu pesa zingine na unaweza usiipate mwisho wa siku ukapata hasara mara mbili

"Wakati mwingine inahitaji kuvunja haki ya mtu husika kupata haki yako"

 Japo sikushauri ufanye hivyo
 
Back
Top Bottom