Habarini humu ndani
Nimekuja kwenu najua nitapata msaada
_Kuna mtu nimefanya nae biashara bila kuonana nae ila alikua amejenga uaminifu mkubwa kwangu
- Maana alikua anatuma hela (advance) natengeneza mzigo namtumia kisha ananimalizia pesa iliobaki
Baadae akanambia nimtumie mzigo (mzigo nilikua naitumia karibu na shekilango) yeye yupo katoro
akanambia nikifika sehem ninayotumia mzigo kuna mtu atanipa namba zake niwasiliane nahuyo mtu atanipa pesa yahuo mzigo (huyo mtu yupo kariakoo)
nikaona sawa kwakua nishamuamini haina shida
mzigo nikaufikisha pale muda ule nafika gari nayo inataka kuondoka so mzigo mojakwamoja ukatiwa kwenye buti gari ikaondoka
Nikawa nampigia jamaa niliepewa namba yake ili anipe pesa yamzigo wangu . kutoka saa tisa jioni nampigia anakuja kupokea simu saa mbili usiku.
Anasema nilikua mbali nasimu .pesa yako nimepewa ila naomba tuonane kesho nikupe maana saiv nishafunga duka (maneno yake) nikasema sawa
kesho yake hakupokea simu mwisho ikawa haipatikani kabisa
_ Nikamrudia niliefanya nae biashara. akasema bas kama hapatikani hio pesa nitakulipa mimi mwenyewe
Ilikua 23/7/2026 (mwezi uliopita) mpaka leo 13/8/2026 namba zao wote hazipatikani
huyu niliefanya nae biashara anapatikana whatsapp tu kila siku anasema kesho kesho online anaingia siku anayotaka yeye
-Biashara anafanyia katoro (kwamaelezo yake) sijawahi kuonana nae hata picha yake sina
najua kwaupande wangu nimefanya makosa lakini tayari ishatokea hivyo .
Naomba msaada wenu nitumie mbinu gani ili niweze kuipata pesa yangu
AHSANTE