MawardatDellapina
JF-Expert Member
- Apr 27, 2021
- 30,232
- 152,252
Mchawi nida tu,
Kuna mwamba aliiba pikipiki,mfumo ulidaka family yake.
Kuna mwamba aliiba pikipiki,mfumo ulidaka family yake.
NIMEACHA KUSOMA BAADA YA KUONA HIIHabarini humu ndani
Nimekuja kwenu najua nitapata msaada
_Kuna mtu nimefanya nae biashara bila kuonana nae ila alikua amejenga uaminifu mkubwa kwangu
- Maana alikua anatuma hela (advance) natengeneza mzigo namtumia kisha ananimalizia pesa iliobaki
Baadae akanambia nimtumie mzigo (mzigo nilikua naitumia karibu na shekilango) yeye yupo katoro
akanambia nikifika sehem ninayotumia mzigo kuna mtu atanipa namba zake niwasiliane nahuyo mtu atanipa pesa yahuo mzigo (huyo mtu yupo kariakoo)
nikaona sawa kwakua nishamuamini haina shida
mzigo nikaufikisha pale muda ule nafika gari nayo inataka kuondoka so mzigo mojakwamoja ukatiwa kwenye buti gari ikaondoka
Nikawa nampigia jamaa niliepewa namba yake ili anipe pesa yamzigo wangu . kutoka saa tisa jioni nampigia anakuja kupokea simu saa mbili usiku.
Anasema nilikua mbali nasimu .pesa yako nimepewa ila naomba tuonane kesho nikupe maana saiv nishafunga duka (maneno yake) nikasema sawa
kesho yake hakupokea simu mwisho ikawa haipatikani kabisa
_ Nikamrudia niliefanya nae biashara. akasema bas kama hapatikani hio pesa nitakulipa mimi mwenyewe
Ilikua 23/7/2026 (mwezi uliopita) mpaka leo 13/8/2026 namba zao wote hazipatikani
huyu niliefanya nae biashara anapatikana whatsapp tu kila siku anasema kesho kesho online anaingia siku anayotaka yeye
-Biashara anafanyia katoro (kwamaelezo yake) sijawahi kuonana nae hata picha yake sina
najua kwaupande wangu nimefanya makosa lakini tayari ishatokea hivyo .
Naomba msaada wenu nitumie mbinu gani ili niweze kuipata pesa yangu
AHSANTE
nikweli nimefanya makosa- ila kabla yahapo ilikua tayari tushafanya biashara. alituma pesa nyingi ili nimuuzie mzigo so ilikua rahisi kumuaminiYaani mtu yuko Geita huko, anakuambia hela yako iko kwa mtu wa Kariakoo, kisha wewe unapakia mzigo kwenye gari la Shekilango bila kushika cash mkononi?
Honestly, you played yourself.
Hiyo pesa nyingi ilikuwa chambo tu mkuu, na wewe ukameza hadi ndoano! Dah pole sana.nikweli nimefanya makosa- ila kabla yahapo ilikua tayari tushafanya biashara. alituma pesa nyingi ili nimuuzie mzigo so ilikua rahisi kumuamini
Nguvu atakayotumia kujaribu kurejesha hela itagharimu vingi kuliko hela aliyopoteza.Mjomba, mimi sitakuwa kwenye lile kundi maarufu la watu wa kukukejeli kwa uzembe ulioufanya wa kumuamini mtu mwenye ngozi nyeusi usiyemfahamu! Na akaishia kukutapeli. Huu ni uzembe wa hali ya juu sana.
Mimi nipo kwenye lile kundi la wasema kweli. Na hapa ninataka nikuambie tu ukweli; acha kuhangaika kuomba ushauri au kwenda kushtaki mahali popote! Kwa maana hakuna utakacho kipata.
Ushauri wangu kwako; kama wewe ni mkristo, basi piga goti na umshukuru Mungu kwa yote. Yaani ukubali ukweli umetapeliwa (na hili ni jambo la kawaida sana kwenye maisha, hata mimi nimetapeliwa mpaka na watu ninao wafahamu), na hiyo hela haitarudi kamwe.
NB: Ukienda kwa waganga wa kienyeji (wataalam) au polisi, utatapeliwa zaidi.
Huyo tayari unae hachomoki.Voice zake ninazo- risiti aliokua nafanya malipo ya CRDB kwa wakala pia ninayo
Dunia ina huruma ndio maana hatujaangamia ila watu ndio hawana huruma mkuu wanadhurumu hao balaa na hawana hofu yeyote..dunia haina huruma kabisa
Daah aiseeUyo jamaa itakua yeye katapeliwa alafu akaamua kuingia mitini
Usimtafute huyo nae tapeli tu!shukrani sana mkuu nitakutafuta
Atenge na pesa mapema maana atakuwa fursa kwa maafande.Mawasiliano yake unayo tayari fungua jarada polisi la utapeli atafatiliwa tu