Nimedhurumiwa Tsh. Milioni 2.4 na Mtu niliyekuwa nafanyanae biashara

Wabongo kwenye uaminifu ni tatizo...

Kuna jamaa anataka kunidhurumu elfu 70 kwa dharau sana...

Hapa nina option 2..

1. Nitumie 70 elfu kumfuata alipo ili nimalizane nae kiume

2. Nimshitaki.
 
acha tu ndugu yangu
Kipindi hiki kigumu kufanya biashara na wateja wapya au wa zamani kwa kuwaamini kwa mzigo wa thamani sana ni kupunguza mimi niliacha kukopesha bora mali ikae store maana nilikua na madeni mengi nje tena kwa wateja waaminifu mali hawana na hela hawana madeni yao ya bank wanaona hela yako alipe bank wewe anabaki kukusumbua tu nina muda mrefu mafanya hivi naona ipo vizuri..
 
dunia haina huruma kabisa
 
Huwa tunakosea kwenye biashara kwenye wepesi wa kumuamini mtu.

Binadamu kusema kweli hatutakiwi kuaminiana hata kama mtu ataonesha uaminifu mkubwa vipi kwako.

Kama ungekumbuka ungewahi kuwasiliana na bus ulilotuma mzigo uwaambie wakifika wasiukabidhi kwa mtu, baadae mzigo ungerudishwa kwako.

Usihuzunike sana, pesa tunazitafuta amini utapata nyingine zaidi ya hizo 2.4, jitahidi kusahau tukio ukiweza futa mawasiliano ya huyo tapeli, lakini kwanza toa taarifa polisi unaweza kumpata kama bado yupo online.

Wezi nao huwa wajinga wakati mwingine.
 
Duh hizi biashara za bongo an mpaka sometimes unaogopa, Pole mkuu..hapo option ni police tena kama una mshkaji Askari ukimtangazia posho chap TU,lakini hata kutrack namba Ili mjue specific wapi alipo,,nawasilisha
 
Mimi nahisi nina pepo la kudhulumiwa.
Pole sana. Wakati mwingine kama mchakato wa kukomboa hela ni mgumu au ghali au utakuacha na hatia, ni vema kujifunza kuachilia ili uweze kusonga mbele.
 
Nenda Mahenge kamroge hela yako unarudishiwa kesho yake tena na mbuzi juu..

But anyways inakuwaje wewe mtoto wa mjini Daslam unatapeliwa na mtu wa katoro?
 
Pole sana mkuu, ila kwenye biashara huwa tunatumia sana imani hivyo kudhurumiwa ni rahisi sana. Kwakua bado anapatikana online kuna mwana kashari ufungue jarada polisi mnaweza mfikia.
 
Mjomba, mimi sitakuwa kwenye lile kundi maarufu la watu wa kukukejeli kwa uzembe ulioufanya wa kumuamini mtu mwenye ngozi nyeusi usiyemfahamu! Na akaishia kukutapeli. Huu ni uzembe wa hali ya juu sana.

Mimi nipo kwenye lile kundi la wasema kweli. Na hapa ninataka nikuambie tu ukweli; acha kuhangaika kuomba ushauri au kwenda kushtaki mahali popote! Kwa maana hakuna utakacho kipata.

Ushauri wangu kwako; kama wewe ni mkristo, basi piga goti na umshukuru Mungu kwa yote. Yaani ukubali ukweli umetapeliwa (na hili ni jambo la kawaida sana kwenye maisha, hata mimi nimetapeliwa mpaka na watu ninao wafahamu), na hiyo hela haitarudi kamwe.

NB: Ukienda kwa waganga wa kienyeji (wataalam) au polisi, utatapeliwa zaidi.
 
Mm nipo dar yeye yupo mkoani- alisema yupo katoro hata mizigo niliokua namtumia nilikua naandika jina lake na sehemu hio katoro ila tulionana mtandaoni (mara yakwanza alinitumia laki 9 bila hata kuniona) alituma kama advance
Itakuwa tu mambo hayajakaa sawa Kwa upande wake,,

Lakini angekuwa mkweli tu,
 
Mm nipo dar yeye yupo mkoani- alisema yupo katoro hata mizigo niliokua namtumia nilikua naandika jina lake na sehemu hio katoro ila tulionana mtandaoni (mara yakwanza alinitumia laki 9 bila hata kuniona) alituma kama advance
Hizo ndio mbinu mpya za matapeli.
Hiyo kukupa advance kwa mara ya kwanza alikua anakuvuta ujae..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…