Kijakazi Chizi
Member
- Dec 9, 2025
- 89
- 213
Habari wana JF,
Kweli nimeamini kuna wakati tunatakiwa kuheshimu mawazo yetu ya awali hasa wakati tunapojaribu kufikiria jambo fulani linalotutatiza kiuhalisia.
Katika maisha yangu niliamini kuwambali na wanaume kunaweza kunipa amani ya moyo na maisha kiujumla nikijikita katika kazi kujikimu kimaisha binafsi bila kumtegemea mtu hasa wanaume na hii ilisababishwa na zile zote nilizokuwa napata kutoka kwa marafiki wanavyosalitiwa kwenye mahusiano yao.
Miaka mitatu nyuma niliamua rasmi kuingia kwenye mahusiano nilivyoona kuwa tayari nina kila kitu nililohitaji kwenye maisha yangu, na vile umri pia unakimbia nikasema ngoja nijaribu mahusiano.
Nikakutana na kijana wa kihaya mtanashati mwenye kazi yake nzuri tu, basi maisha ya mahusiano yakaanza vizuri nikiamini tunamwelekeo kwenye ndoa.
Mwanzoni tunaanza mahusiano alikuwa akinieleza mahusiano yake yaliyopita kwamba mpenzi wake huyo alikuwa akipenda sana hela kitu ambacho yeye alikuwa anachukia, hivyo mimi nikajiongeza kwamba wenda nikimwambia mahitaji yangu itakuwa najishusha hadhi kwake. Basi nikakaza nikijihudumia lakini hata yeye hakuwai labda kujiongeza kwamba huyu ni mwanamke wangu basi hata vijizawadi hakuna yaani ni kavu tu.
Tumeendelea na hayo mahusiano hivyo hivyo yaani ambapo kuna wakati naweza kwenda kukaa kwake hata wiki yaani kama mke na mume, Ila nikaanza kuhisi kitu hakiko sawa. Nikienda kwake bila taarifa anafoka na hasira juu, hata zile simu za njoo nyumbani hakuna tena
Ningejua ningebaki na mawazo yangu ya awali ya kuishi tu maisha yangu ya ubachela, imagine miaka mitatu kwenye mahusiano na mtu unayeamini mtafunga ndoa na kuwa na familia from nowhere tu anatoa hii kauli kwamba mwanaume atakayenioa ana bahati sana, hii kauli imenitafakarisha sana.
Nimewaza kapata mwanamke mwingine au vipi?, mbona sijawai kumfosi kunihudumia wala hata yeye hajawai toa hata senti mia kuninunulia chochote? au hivyo havikuwa vigezo tosha ya mimi kuwa wife material?
Nahisi hasira sanaaa!!!!!!!