Nimedumu naye kwenye Mahusiano miaka 3, leo anasema mwanaume atakayenioa ana bahati

Nimedumu naye kwenye Mahusiano miaka 3, leo anasema mwanaume atakayenioa ana bahati

Hongera umefanya vizuri kujitegemea , pole kwakuwa hakuwa na malengo sawa nawe, Kaa pembeni Anza upya
 
Nampongeza jamaa kwa kukustukia mapema na hayo maigizo yako, maana ulikua unaagiza na angekuoa tu asingeacha kuona kila aina ya rangi

Safi sana tuendelee kuzichapa hivihvi
 
Pole mwaya, ila it’s clearly wewe ulikuwa mchepuko kwake..!
wanaume walivyo watoaji hivyo kwa watu wanaowaopenda, hata huombi mama angu kama wewe ni kipaumbele kwake..!

Japo yes, miezi ya mwanzo anaweza kukupima asikupe hata 100 na wewe wala usipeleke njaa zako, juaneni kwanza, tengenezeni bond kwanza, pendaneni kwanza, akishajua wewe ndiye alikuwa akutakaye hakuna siku atakunyima kilicho ndani ya uwezo wake..!!

huyo ambaye hata hajigusi kwa kinguo cha ndani ama ki perfume kizuri kaona mahali hapo umepigwa, unaenda kwa mwanaume wako badala afurahi kukuona anafoka..!? unasubiri nini hapo binti..!?
Uko na mahekima mengi.
 
Wanatuona mapoyoyo .

Na hapo wanataka waridhishwe 😂😂😂😂😂😂
Wanajiona wao wanahaki ya kupewa kisa tu wanakipochi manyoya. Wanasahau hata wao wanaweza kujipambania mahitaji yao. Swala la sex ni la asili zaidi, wote tunategemeana kupeana!
 
Mshukru MUNGU amekuonyesha mapema aina ya mtu uliyetaka kumkabidhi hatima yako ya mahusiano

1. usije fanya maamzi ili hali bado una hasira

2. hakuna kona kona huyo unaeenda kwake anahisi umemkosea hafai.

3. hapo hakuna mme, piga chini, tuliza roho kwa muda siyo chini ya miez sita, uanze safari upya ya mahusiano kama utaona umhimu

4. utanashati na kuwa na kazi syo sifa ya mme bora.
-UNAHITAJI KUWA NA MACHO YA KIROHO MAANA HUO SI MCHEPUKO BALI NI MME.

5. Kuwa busy na kazi yako, ongeza kipato, toa zaka, dumu katika maombi kwa imani yako na MUNGU wako atakufanyia wepesi.

6. msamehe huyo mwanaume kwa matendo yake, bila kufanya hvo roho ya kinyongo inaweza kukurusha pabaya

7. siku nyingine usitangulize ngono kabla ya ndoa
-ngono siyo sifa mmojawapo ya ndoa
-ngono yaweza leta roho chafu za kukuharibia ndoa (HAMTANIELEWA HAPA HADI YAKUKUTE)

8. siku nyingine jitahidi kumshirikisha MUNGU wa imani yako na wazazi wako(siyo ndugu waweza kukuharibia)

9. usirudipo, simama imara anza upya piga hatua kumi mbele.
 
Habari wana JF,

Kweli nimeamini kuna wakati tunatakiwa kuheshimu mawazo yetu ya awali hasa wakati tunapojaribu kufikiria jambo fulani linalotutatiza kiuhalisia.

Katika maisha yangu niliamini kuwambali na wanaume kunaweza kunipa amani ya moyo na maisha kiujumla nikijikita katika kazi kujikimu kimaisha binafsi bila kumtegemea mtu hasa wanaume na hii ilisababishwa na zile zote nilizokuwa napata kutoka kwa marafiki wanavyosalitiwa kwenye mahusiano yao.

Miaka mitatu nyuma niliamua rasmi kuingia kwenye mahusiano nilivyoona kuwa tayari nina kila kitu nililohitaji kwenye maisha yangu, na vile umri pia unakimbia nikasema ngoja nijaribu mahusiano.

Nikakutana na kijana wa kihaya mtanashati mwenye kazi yake nzuri tu, basi maisha ya mahusiano yakaanza vizuri nikiamini tunamwelekeo kwenye ndoa.

Mwanzoni tunaanza mahusiano alikuwa akinieleza mahusiano yake yaliyopita kwamba mpenzi wake huyo alikuwa akipenda sana hela kitu ambacho yeye alikuwa anachukia, hivyo mimi nikajiongeza kwamba wenda nikimwambia mahitaji yangu itakuwa najishusha hadhi kwake. Basi nikakaza nikijihudumia lakini hata yeye hakuwai labda kujiongeza kwamba huyu ni mwanamke wangu basi hata vijizawadi hakuna yaani ni kavu tu.

Tumeendelea na hayo mahusiano hivyo hivyo yaani ambapo kuna wakati naweza kwenda kukaa kwake hata wiki yaani kama mke na mume, Ila nikaanza kuhisi kitu hakiko sawa. Nikienda kwake bila taarifa anafoka na hasira juu, hata zile simu za njoo nyumbani hakuna tena

Ningejua ningebaki na mawazo yangu ya awali ya kuishi tu maisha yangu ya ubachela, imagine miaka mitatu kwenye mahusiano na mtu unayeamini mtafunga ndoa na kuwa na familia from nowhere tu anatoa hii kauli kwamba mwanaume atakayenioa ana bahati sana, hii kauli imenitafakarisha sana.

Nimewaza kapata mwanamke mwingine au vipi?, mbona sijawai kumfosi kunihudumia wala hata yeye hajawai toa hata senti mia kuninunulia chochote? au hivyo havikuwa vigezo tosha ya mimi kuwa wife material?

Nahisi hasira sanaaa!!!!!!!
Ukiona manyoya??
Hapo UMESHALIWA binti. Jikusanye, uendelee na safari, cha muhimu UJIFUNZE.
 
Mshukru MUNGU amekuonyesha mapema aina ya mtu uliyetaka kumkabidhi hatima yako ya mahusiano

1. usije fanya maamzi ili hali bado una hasira

2. hakuna kona kona huyo unaeenda kwake anahisi umemkosea hafai.

3. hapo hakuna mme, piga chini, tuliza roho kwa muda siyo chini ya miez sita, uanze safari upya ya mahusiano kama utaona umhimu

4. utanashati na kuwa na kazi syo sifa ya mme bora.
-UNAHITAJI KUWA NA MACHO YA KIROHO MAANA HUO SI MCHEPUKO BALI NI MME.

5. Kuwa busy na kazi yako, ongeza kipato, toa zaka, dumu katika maombi kwa imani yako na MUNGU wako atakufanyia wepesi.

6. msamehe huyo mwanaume kwa matendo yake, bila kufanya hvo roho ya kinyongo inaweza kukurusha pabaya

7. siku nyingine usitangulize ngono kabla ya ndoa
-ngono siyo sifa mmojawapo ya ndoa
-ngono yaweza leta roho chafu za kukuharibia ndoa (HAMTANIELEWA HAPA HADI YAKUKUTE)

8. siku nyingine jitahidi kumshirikisha MUNGU wa imani yako na wazazi wako(siyo ndugu waweza kukuharibia)

9. usirudipo, simama imara anza upya piga hatua kumi mbele.
asante sana kwa ushauri, hakika nimepata funzo
 
Back
Top Bottom