Habari zenu nyote,
Ni takribani miaka 6 sasa tangu niwe na huyu msaidizi wa kazi za nyumbani, nilimchukua akiwa mdogo akiwa na umri wa miaka 15 baada ya kumaliza elimu yake ya msingi.
Maisha ya nyumbani kwao yalikuwa ni duni sana, na wazazi wake walionekana kushukuru sana binti yao kupata hii kazi ambayo mshahara kwa huo mwaka tulikubaliana elfu 30.
Baada ya kukaa nae kwangu, ndugu niliokuwa nakaa nao akiwemo mke niligundua hali ambayo sio nzuri ya kumtumikisha kazi nyingi zinazomzidi umri wake na zingine zingewezwa kufanywa na wao.
Nilizungumza nao na nashukuru walinielewa na wakawa wanamchukulia Kama mdogo wao na hata utambulisho wake kwa wageni haukuwa tena mfanyakazi wa ndani bali mdogo wetu.
Nilimshurikisha mke wangu juu ya kumuendeleza huyu binti na tulipomuuliza nini anapenda kujifunza, alitujibu anahitaji kuwa mshonaji wa nguo.
Tulimtafutia chuo akasoma mwaka mmoja hapo baadae tukamhamishia VETA kwa ajili ya ujuzi zaidi wa mafunzo hayo kwa mwaka mwongine, Alipomaliza aliomba kuendelea na fani nyingine ya urembo na upambaji hapohapo VETA tukamlipia na alimaliza vema.
Baada ya kumaliza tulimnunulia vyerehani viwili kwa kutumia pesa yake ya mshahara tuliyokuwa tunamtunzia na kuongezea ilipopungua na kumlipia frem kwa miezi 6 pamoja na kumuwekea vitenge na vitambaa kidogo kwenye frem akaanza kushona huku akiwa anakaa kwangu kwa miezi miwili.
Baada ya kumchunguza na kuona akili yake imekomaa, tukampangishia chumba cha 30k kwa miezi 4 akahamia na vyombo kidogo.
Nafurahi kuona hadi sasa anaendelea vizuri hakosi 40elfu kwa siku, sasa amepata mchumba anataka kuolewa.
Hili ni Jambo la kujivunia kwangu kuona maisha yake yamebadilika.