Nimefanikiwa kupambana na kunguni na kuwapunguza kwa kiasi kikubwa sana

Nimefanikiwa kupambana na kunguni na kuwapunguza kwa kiasi kikubwa sana

Wakati niko hostel nilikuwa natumia dawa ya kupiga kwenye vyandarua maarufu kama NGAO. Ile ilikuwa kiboko. Inaua kunguni taratibu. Ndani ya wiki hakuna kunguni Wala Mtoto wa kunguni.

Sijui imeenda wapi,siku hizi haipo madukani!
Hiyo machine sio mchezo niliitumia kuua mende .Sehemu nilipomwagia kila mdudu aliekua anakatiza huo ukanda alikua anakufa kwa miaka 3 mfululilizo.
 
Nilitaka kuwaza kiboya ni tangazo I kwa hiyo picha nikajua umeandika kwa lengo la kutoa msaada kwa wahanga ambao wapo kimya. Kunguni wapo hata Mimi juzi nilikuwa na battle nao Ila niliwaangamiza kwa Nuvan na mafuta ya taa.
 
Hawa wadudu mimi hua nawateketeza kwa gharama ya shilingi miambili tu.

Ni Tsh200/-
 
Japo imekaa kama tangazo la biashara ila asante sana mkuu, kizuri mgawie jirani yako.... Mkuu ungesema uko sehemu gani maana kunguni wa Mwanza hawasikii sumu yoyote!
Huku MWanza Kunguni ni janga kuu la Mkoa! Ngoja tu
Kunguni hata MAJI YA POVU KALI unawaua vizur tu.. Nunua sabun ya buku 2 dofi alaf changanya yote na maji Lita 20 njoo nishkuru baada ya wiki alafu mwagia KO na zote Kama unaosha kitanda
 
Suluhisho pekee la Kunguni ni Maji ya Moto. Chemsha Maji yapate Moto kwa kiwango cha Juu kabisa halafu kamwagie Sehemu zote zenye Mazalia yao. Fua vitu vyote halaf anika Juani baada ya hapo kunguni utawasikia kwa wengine
nyumba ya jirani walikuwa wanaanika magodoro yao juu ya bati langu la bafu. kumbe wadudu wanatoka wanaingia bafuni ukienda kuoga wanadandia taulo. Tuligundua baadaye baada ya kuumiza vichwa sana kujua wanakotokea.
 
Dawa mojawapo kunguni ni mafuta ya ndege(airplane) .Namna ya kuyapata ni hasa kwenye viwanja vya ndege. Ndo shida kuyapata na yanaharufu kali sana. Waharifu huyatumia kama nusukaputi. Polisi wakikudaka nayo utaeleza ulipoficha mzigo.
Hayo mafuta ni kiboko kwa kunguni.
 
Kunguni wanakera sana, unakosa usingizi wakati mwingine unadhalilika!

Basi bwana kuna hii dawa inaitwa diazinone, niliitumia mwaka 2015 na nikafanikiwa kuwaangamiza hawa wadudu korofi.

Ghafla tena naitwa nyumbani kwamba wadudu wanasumbua, njoo utupe msaada, nikaenda kweli nikakuta wamejaa kwenye neti, godoro mpaka kitandani, hadi watoto wamehamishiwa vyumba vingine.

View attachment 1938474View attachment 1938476

Nilivyoona hii hali basi nikaingia mjini na sh elfu 10 tu nikiwa na uhakika hii inamaliza kila kitu.

Kweli, nikapata dawa chupa 1 sh elfu 2.5 nikachukua 2 kwa elfu 5.

Chupa ya spray nikabeba kwa elfu 4.

View attachment 1938493

Chupa 1 unachanganya na lita 2 za maji safi.

View attachment 1938504

Kisha unakoroga vizuri (hakikisha kama unaweza uvae gloves, barakoa kuoa suffocation, PPE ni muhimu maana hii ni sumu hatari sana)

Nikachanganya dawa vizuri na maji mpaka ikawa kama maziwa

View attachment 1938512

Baada ya hapo nikaweka kwenye chupa nikaanza spray, vitu vyote lazima viwe katika sehemu ya wazi yenye hewa na mwanga wa kutosha ili mdudu aonekane vizuri na kuepuka suffocation.

Kusema kweli hii dawa ilileta matokeo mazuri sana mpaka sasa wadudu wamepungua kwa asilimia 90
Nenda duka la dawa za kiliMo na mifugo uliza sumu ya kuua wadudu inaitwa Nuvan chupa moja sh 6,000/ hadi 7 utakuja kunishukulu baadaye,achana na hiyo D zon
 
Dawa ya kunguni ni petrol, weka kwenye sprayer nyunyiza pote unapohisi wapo,ila hakikisha unaponyunyiza usiwashe moto mpaka petrol ikauke. Hutaona kunguni tena kwenye ghetto lako.
 
Kuna dawa moja ya kuulia wadudu wa shamba ,nikichupa kidogo tu kama vile vya dawa za watoto.kuna kunguni walikuwa wakisumbua sana kwenye gari ,watu wanakimbia gari wakati wa usiku,ukiuliza nn jibu ni kunguni,kuna siku tukapewa gari moja wapo wa hizo,aisee kunguni akaleta valangati mchana huo huo,

Kuna jamaa akatuletea ile dawa bwana ,akasema hii ni komesha wala msisumbuke,hiyo dawa ni hatari ,mda wa nusu saa baada ya kupulizia tukapanda kwenye chombo safari ikaendelea,haina harufu wala nn.nitaiulizia jina nilete mrejesho,na bei yake 5k madukani,si unajua lori watu wengine wanahamisha wadudu kutoka majumban.hiyo dawa ni komesha
 
Back
Top Bottom