Nimefanikiwa kupambana na kunguni na kuwapunguza kwa kiasi kikubwa sana

Nimefanikiwa kupambana na kunguni na kuwapunguza kwa kiasi kikubwa sana

Kuna dawa moja ya kuulia wadudu wa shamba ,nikichupa kidogo tu kama vile vya dawa za watoto.kuna kunguni walikuwa wakisumbua sana kwenye gari ,watu wanakimbia gari wakati wa usiku,ukiuliza nn jibu ni kunguni,kuna siku tukapewa gari moja wapo wa hizo,aisee kunguni akaleta valangati mchana huo huo,

Kuna jamaa akatuletea ile dawa bwana ,akasema hii ni komesha wala msisumbuke,hiyo dawa ni hatari ,mda wa nusu saa baada ya kupulizia tukapanda kwenye chombo safari ikaendelea,haina harufu wala nn.nitaiulizia jina nilete mrejesho,na bei yake 5k madukani,si unajua lori watu wengine wanahamisha wadudu kutoka majumban.hiyo dawa ni komesha
Bila shaka ni lava
iangalie kama unaweza ikumbuka
IMG_20210910_082654_818.jpg
 
Kuna denti kawaleta kwangu! Hapa nacheza rhumba kuliko Mokili Mobimba, kunguni wasikieni tu jamani! Nishapiga fatiki hadi nimezipa slogan kama operation tokomeza, War in Bunju (WIBU) lakini wapi [emoji56]
Wadau wame suggest dawa nyingi sana mpaka za mia 2
hebu fuatilia comments za nyuma utapata suluhisho
 
Kunguni hawangalii masikini wala tajiri.

Prado hizo ziko 2. noah 2. Amarok 1. Pick up 1, Terrano 1, Pikipiki XL 250 iko 1.

Vikorokoro ni vingi ndio maana wadudu wanaingia bila taarifa
Au ndo vileta pesa vyenu?
 
Kunguni hata MAJI YA POVU KALI unawaua vizur tu.. Nunua sabun ya buku 2 dofi alaf changanya yote na maji Lita 20 njoo nishkuru baada ya wiki alafu mwagia KO na zote Kama unaosha kitanda
Kitambo nimewahi kutumia hiyo mbinu ya sabuni ya unga, tukaambiwa tuweke na ugolo na diesel lakini wapi....
 
Mkuu kama maji yake ni meusi itakuwa hiyo,mana kopo pia lilikuwa jeupe hivo hivo
Sikuijaribu mkuu.
niliona nianze na Diazinone, ikigoma nichukue hio LAVA.
LAVA ikishindwa nabeba ile ya kupulizia kwenye pamba😅😅
 
Mkuu kunguni hawaji sababu ya uchafu, ni viumbe tu wapogo wanahamisha makazi na kuzaliana sana hata kama uwe msafi vipi, na chakula chao ndio hivo damu.
Na siku unawaona wawili watatu ujue mafichoni wapo kama mia.
 
huyu mdudu anakaa kwenye kona za kitanda, chaga na sehemu za godoro lililochanika.

kumbuka baada ya dawa zingatia usafi, muhimu sana kurudia dawa baada ya mwezi mmoja.

kumuangamiza kunguni ni kazi ngumu sana.
Mimi, dawa niliyotumia haikuwa hata na haja ya kurudia,Mara moja tu,halikubaki hata yai la kunguni! Na siikumbuki ile dawa sio kama hii!
 
tena usije danganywa na wale jamaa wa kutembeza,wanajaza maji mengi mpaka makali ya dawa yanakatika,kisha wanajaza petroli kisoda kimoja.

mimi walisumbua sana nikawa nanunua kwa wale jamaa baada ya miezi miwili unashangaa haoo,tatizo langu ni moja,mimi wakiniuma sisikii na wala sivimbi wife na watoto wanasikia na wanatoka alama.nikawa napata malalamiko tu,ila siwaoni.

siku moja nikawa natafuta kitu uvunguni nikageuza godoro aisee,nilichoka,yaani niliidharau kazi yote ambayo nimekua nikiifanya miezi kadhaa ya kuwapulizia pafyumes kumbe wana mahandaki chini mpaka wanaweka ile ramani nyeusi kwenye pindo la godoro,nikakaa chini natafakari nini nifanye???wazo likaja ninunue mafuta nipake kila kona,lakini kwanza nivue cover ile ya draft kwenye godoro,nikaichana na wembe nikaitoa,kisha nikamwaga mafuta ya taa mpaka ndani kukawa hakukaliki.
nimekaa miezi kadhaa nashangaa hao tenaa.
bahati haikuwa yao maana kipindi si kirefu alikuja jamaa wa furmigation kazini,nikampora dawa halisi ikiwa haijachanganywa,nikamimina na kuondoka nayo nyumbani kwa akiba.

nilichofanya safari hii nikaenda kutafuta kopo la spray,na kuchanganya solutiona kali sana,na kuanza kuwapulizia bila huruma.naona kwa sasa kimyaa zaidi ya miezi 7 sasa.
 
Back
Top Bottom