Nimefanikiwa kupambana na kunguni na kuwapunguza kwa kiasi kikubwa sana

Nimefanikiwa kupambana na kunguni na kuwapunguza kwa kiasi kikubwa sana

Suluhisho pekee la Kunguni ni Maji ya Moto. Chemsha Maji yapate Moto kwa kiwango cha Juu kabisa halafu kamwagie Sehemu zote zenye Mazalia yao. Fua vitu vyote halaf anika Juani baada ya hapo kunguni utawasikia kwa wengine
Hahahhaa ,unajua ukimwagia maji ya moto ndo unaharakisha mayai kutotoa ? hata ukimwagia maji kunguni hafi na anaweza akakaa muda mrefu hata miezi 6 bila hata ya kula
 
Hahahhaa ,unajua ukimwagia maji ya moto ndo unaharakisha mayai kutotoa ? hata ukimwagia maji kunguni hafi na anaweza akakaa muda mrefu hata miezi 6 bila hata ya kula
Dawa ya kunguni,sabuni ya unga,chumvi na mafuta ya taa changanya mwagiwa...wanaisha wotee

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Kunguni wanakera sana, unakosa usingizi wakati mwingine unadhalilika!

Basi bwana kuna hii dawa inaitwa diazinone, niliitumia mwaka 2015 na nikafanikiwa kuwaangamiza hawa wadudu korofi.

Ghafla tena naitwa nyumbani kwamba wadudu wanasumbua, njoo utupe msaada, nikaenda kweli nikakuta wamejaa kwenye neti, godoro mpaka kitandani, hadi watoto wamehamishiwa vyumba vingine.

View attachment 1938474View attachment 1938476

Nilivyoona hii hali basi nikaingia mjini na sh elfu 10 tu nikiwa na uhakika hii inamaliza kila kitu.

Kweli, nikapata dawa chupa 1 sh elfu 2.5 nikachukua 2 kwa elfu 5.

Chupa ya spray nikabeba kwa elfu 4.

View attachment 1938493

Chupa 1 unachanganya na lita 2 za maji safi.

View attachment 1938504

Kisha unakoroga vizuri (hakikisha kama unaweza uvae gloves, barakoa kuoa suffocation, PPE ni muhimu maana hii ni sumu hatari sana)

Nikachanganya dawa vizuri na maji mpaka ikawa kama maziwa

View attachment 1938512

Baada ya hapo nikaweka kwenye chupa nikaanza spray, vitu vyote lazima viwe katika sehemu ya wazi yenye hewa na mwanga wa kutosha ili mdudu aonekane vizuri na kuepuka suffocation.

Kusema kweli hii dawa ilileta matokeo mazuri sana mpaka sasa wadudu wamepungua kwa asilimia 90
Tangazo la biashara hili mkuu, uwalipe JF.
 
Kunguni Ni uchafu Kama unafua nguo na matandiko frequently sahau kuhusu kunguni,wanakaa mpaka kwenye nyufa,sofa ,dogoro Kama haoina cover ndio ususeme,hata mafuta ya taa yanaua pia Kama una kunguni deki Mara kwa Mara,fua neti
 
Kunguni Ni uchafu Kama unafua nguo na matandiko frequently sahau kuhusu kunguni,wanakaa mpaka kwenye nyufa,sofa ,dogoro Kama haoina cover ndio ususeme,hata mafuta ya taa yanaua pia Kama una kunguni deki Mara kwa Mara,fua
 
Kunguni Ni uchafu Kama unafua nguo na matandiko frequently sahau kuhusu kunguni,wanakaa mpaka kwenye nyufa,sofa ,dogoro Kama haoina cover ndio ususeme,hata mafuta ya taa yanaua pia Kama una kunguni deki Mara kwa Mara,fua neti
Tema mate chini kunguni ni hatari
 
Mkitaka kuwaua kunguni mix hivi vifuatavyo, Maji thinner or tiner (if I'm right) Ile ya ambayo hutumika kwenye rangi, sabuni ya unga au ukitaka weka kerosene Ila mostly ni thinner na sabuni.
Nilifanya zoezi Hilo Kwa kuwakamata na kuwaweka kwenye kopo wengi na kujaribu and it work instantly na hawarudi.
Ukiwapulizia thinner huwa wanainua juu abdomen (tumbo) zao ili kupata oxygen maana ndo kuna tundu za upumuliaji, hivyo hakikisha all corner za nyumba, nyufa, makutano ya sofa na sehemu zenye giza sababu hawapendi light 😄.
Hawarudi tena
 
Kunguni hawasababishwi na uchafu. Hii ni kwa sababu hali uchafu au kupendelea kuishi pachafu.

Kunguni unaweza kumkuta hata katika 5 stars hotel. Ni kwamba mwanadamu anapolala huwa anatoa harufu fulani (pheromone) ambayo humvutia sana kunguni na harufu hiyo hutolewa na mwanadamu tu ndio maana huwezi kukutana kunguni kwenye banda la mifugo wala jikoni bali utakuwa chumbani.

Kunguni huweza kutumia 95% ya maisha yake mafichoni. Na atatoka kwenda Kula au kuhama maficho.
Kunguni wamekuwa sugu kwa sababu ya matumizi holela ya viuwatilifu ambapo husabibisha watengeneze chemical resistance. Hivyo matumizi sahihi ya viuwatilifu ni muhimu sana katika mapambano.

Natoa huduma ya fumigation kwa gharama nafuu popote nchini Tanzania. Napatikana kwa namba 071813106. Nipo Morogoro.
 
Dawa mojawapo kunguni ni mafuta ya ndege(airplane) .Namna ya kuyapata ni hasa kwenye viwanja vya ndege. Ndo shida kuyapata na yanaharufu kali sana. Waharifu huyatumia kama nusukaputi. Polisi wakikudaka nayo utaeleza ulipoficha mzigo.
Hayo mafuta ni kiboko kwa kunguni.
Hao wahalifu wanayapata sehemu gani,ama uku mtaani hayauziki,kama ni dawa ya kuua kunguni kama ulivyosema serikali hawajua
 
tena usije danganywa na wale jamaa wa kutembeza,wanajaza maji mengi mpaka makali ya dawa yanakatika,kisha wanajaza petroli kisoda kimoja.

mimi walisumbua sana nikawa nanunua kwa wale jamaa baada ya miezi miwili unashangaa haoo,tatizo langu ni moja,mimi wakiniuma sisikii na wala sivimbi wife na watoto wanasikia na wanatoka alama.nikawa napata malalamiko tu,ila siwaoni.

siku moja nikawa natafuta kitu uvunguni nikageuza godoro aisee,nilichoka,yaani niliidharau kazi yote ambayo nimekua nikiifanya miezi kadhaa ya kuwapulizia pafyumes kumbe wana mahandaki chini mpaka wanaweka ile ramani nyeusi kwenye pindo la godoro,nikakaa chini natafakari nini nifanye???wazo likaja ninunue mafuta nipake kila kona,lakini kwanza nivue cover ile ya draft kwenye godoro,nikaichana na wembe nikaitoa,kisha nikamwaga mafuta ya taa mpaka ndani kukawa hakukaliki.
nimekaa miezi kadhaa nashangaa hao tenaa.
bahati haikuwa yao maana kipindi si kirefu alikuja jamaa wa furmigation kazini,nikampora dawa halisi ikiwa haijachanganywa,nikamimina na kuondoka nayo nyumbani kwa akiba.

nilichofanya safari hii nikaenda kutafuta kopo la spray,na kuchanganya solutiona kali sana,na kuanza kuwapulizia bila huruma.naona kwa sasa kimyaa zaidi ya miezi 7 sasa.
Pole sn
Ila Wana dawa Yao ukienda maduka ya madawa ya mifugo!
Kikopo kidogo tu, aisee unachanganya na maji kita 4 tu, yaani ilibaki story
 
mpo uchumi wa kati aisee pongezi ziende kwa awamu ya tano
Anyway nilikua suwajui kunguni mbaka siku nilipokua Huko Unguja Zanzibar kwenye Bungalow za Hotel moja ya huko Nungwi aaaah aisee wale wadudu ni kijiji wanauma na hata hawasikii dawa yani!
Wanaletwa na wazungu
 
Back
Top Bottom