Nimefanikiwa kupambana na kunguni na kuwapunguza kwa kiasi kikubwa sana

Nimefanikiwa kupambana na kunguni na kuwapunguza kwa kiasi kikubwa sana

tena usije danganywa na wale jamaa wa kutembeza,wanajaza maji mengi mpaka makali ya dawa yanakatika,kisha wanajaza petroli kisoda kimoja.

mimi walisumbua sana nikawa nanunua kwa wale jamaa baada ya miezi miwili unashangaa haoo,tatizo langu ni moja,mimi wakiniuma sisikii na wala sivimbi wife na watoto wanasikia na wanatoka alama.nikawa napata malalamiko tu,ila siwaoni.

siku moja nikawa natafuta kitu uvunguni nikageuza godoro aisee,nilichoka,yaani niliidharau kazi yote ambayo nimekua nikiifanya miezi kadhaa ya kuwapulizia pafyumes kumbe wana mahandaki chini mpaka wanaweka ile ramani nyeusi kwenye pindo la godoro,nikakaa chini natafakari nini nifanye???wazo likaja ninunue mafuta nipake kila kona,lakini kwanza nivue cover ile ya draft kwenye godoro,nikaichana na wembe nikaitoa,kisha nikamwaga mafuta ya taa mpaka ndani kukawa hakukaliki.
nimekaa miezi kadhaa nashangaa hao tenaa.
bahati haikuwa yao maana kipindi si kirefu alikuja jamaa wa furmigation kazini,nikampora dawa halisi ikiwa haijachanganywa,nikamimina na kuondoka nayo nyumbani kwa akiba.

nilichofanya safari hii nikaenda kutafuta kopo la spray,na kuchanganya solutiona kali sana,na kuanza kuwapulizia bila huruma.naona kwa sasa kimyaa zaidi ya miezi 7 sasa.
Hasa maelezo yote haya na dawa hujaitaja ndugu
 
Kunguni wanakera sana, unakosa usingizi wakati mwingine unadhalilika!

Basi bwana kuna hii dawa inaitwa diazinone, niliitumia mwaka 2015 na nikafanikiwa kuwaangamiza hawa wadudu korofi.

Ghafla tena naitwa nyumbani kwamba wadudu wanasumbua, njoo utupe msaada, nikaenda kweli nikakuta wamejaa kwenye neti, godoro mpaka kitandani, hadi watoto wamehamishiwa vyumba vingine.

View attachment 1938474View attachment 1938476

Nilivyoona hii hali basi nikaingia mjini na sh elfu 10 tu nikiwa na uhakika hii inamaliza kila kitu.

Kweli, nikapata dawa chupa 1 sh elfu 2.5 nikachukua 2 kwa elfu 5.

Chupa ya spray nikabeba kwa elfu 4.

View attachment 1938493

Chupa 1 unachanganya na lita 2 za maji safi.

View attachment 1938504

Kisha unakoroga vizuri (hakikisha kama unaweza uvae gloves, barakoa kuoa suffocation, PPE ni muhimu maana hii ni sumu hatari sana)

Nikachanganya dawa vizuri na maji mpaka ikawa kama maziwa

View attachment 1938512

Baada ya hapo nikaweka kwenye chupa nikaanza spray, vitu vyote lazima viwe katika sehemu ya wazi yenye hewa na mwanga wa kutosha ili mdudu aonekane vizuri na kuepuka suffocation.

Kusema kweli hii dawa ilileta matokeo mazuri sana mpaka sasa wadudu wamepungua kwa asilimia 90
Hivi wale wa Paris waliwamalizaje?
 
Back
Top Bottom