Hiyo machine sio mchezo niliitumia kuua mende .Sehemu nilipomwagia kila mdudu aliekua anakatiza huo ukanda alikua anakufa kwa miaka 3 mfululilizo.Wakati niko hostel nilikuwa natumia dawa ya kupiga kwenye vyandarua maarufu kama NGAO. Ile ilikuwa kiboko. Inaua kunguni taratibu. Ndani ya wiki hakuna kunguni Wala Mtoto wa kunguni.
Sijui imeenda wapi,siku hizi haipo madukani!
Sawa sawa mkuu ila ukitaka iwe mujarabu unatia na chumvi lazma wakasimulieane uko akhera!Dawa ya kunguni mkuu ni mafuta ya taa na sabuni ya unga
Kumbe na wao wanaenda aheraSawa sawa mkuu ila ukitaka iwe mujarabu unatia na chumvi lazma wakasimulieane uko akhera!
Kweli mkuu hata mimi nimewahi kutumia hii njiainawauwa sanaDawa ya kunguni mkuu ni mafuta ya taa na sabuni ya unga
Kunguni hata MAJI YA POVU KALI unawaua vizur tu.. Nunua sabun ya buku 2 dofi alaf changanya yote na maji Lita 20 njoo nishkuru baada ya wiki alafu mwagia KO na zote Kama unaosha kitandaJapo imekaa kama tangazo la biashara ila asante sana mkuu, kizuri mgawie jirani yako.... Mkuu ungesema uko sehemu gani maana kunguni wa Mwanza hawasikii sumu yoyote!
Huku MWanza Kunguni ni janga kuu la Mkoa! Ngoja tu
Sema tuu chuo jirani na Azania secondary school [emoji23][emoji23][emoji23]Kuna chuo kimoja DSM msimu wa muhula kuanza wanafunzi hutaabika sana na kunguni, nakumbuka mdau alikuwa anakesha kusoma kumbe tatizo kunguni
nyumba ya jirani walikuwa wanaanika magodoro yao juu ya bati langu la bafu. kumbe wadudu wanatoka wanaingia bafuni ukienda kuoga wanadandia taulo. Tuligundua baadaye baada ya kuumiza vichwa sana kujua wanakotokea.Suluhisho pekee la Kunguni ni Maji ya Moto. Chemsha Maji yapate Moto kwa kiwango cha Juu kabisa halafu kamwagie Sehemu zote zenye Mazalia yao. Fua vitu vyote halaf anika Juani baada ya hapo kunguni utawasikia kwa wengine
Wasihamie kwenye vit vya gari tuKunguni hawangalii masikini wala tajiri.
Prado hizo ziko 2. noah 2. Amarok 1. Pick up 1, Terrano 1, Pikipiki XL 250 iko 1.
Vikorokoro ni vingi ndio maana wadudu wanaingia bila taarifa
Hivi kunguni mpaka leo wapo kweli, hawa si wanaletwa na tabia ya uchafu!
Nenda duka la dawa za kiliMo na mifugo uliza sumu ya kuua wadudu inaitwa Nuvan chupa moja sh 6,000/ hadi 7 utakuja kunishukulu baadaye,achana na hiyo D zonKunguni wanakera sana, unakosa usingizi wakati mwingine unadhalilika!
Basi bwana kuna hii dawa inaitwa diazinone, niliitumia mwaka 2015 na nikafanikiwa kuwaangamiza hawa wadudu korofi.
Ghafla tena naitwa nyumbani kwamba wadudu wanasumbua, njoo utupe msaada, nikaenda kweli nikakuta wamejaa kwenye neti, godoro mpaka kitandani, hadi watoto wamehamishiwa vyumba vingine.
View attachment 1938474View attachment 1938476
Nilivyoona hii hali basi nikaingia mjini na sh elfu 10 tu nikiwa na uhakika hii inamaliza kila kitu.
Kweli, nikapata dawa chupa 1 sh elfu 2.5 nikachukua 2 kwa elfu 5.
Chupa ya spray nikabeba kwa elfu 4.
View attachment 1938493
Chupa 1 unachanganya na lita 2 za maji safi.
View attachment 1938504
Kisha unakoroga vizuri (hakikisha kama unaweza uvae gloves, barakoa kuoa suffocation, PPE ni muhimu maana hii ni sumu hatari sana)
Nikachanganya dawa vizuri na maji mpaka ikawa kama maziwa
View attachment 1938512
Baada ya hapo nikaweka kwenye chupa nikaanza spray, vitu vyote lazima viwe katika sehemu ya wazi yenye hewa na mwanga wa kutosha ili mdudu aonekane vizuri na kuepuka suffocation.
Kusema kweli hii dawa ilileta matokeo mazuri sana mpaka sasa wadudu wamepungua kwa asilimia 90