Nimefanikiwa kupata mil 15 naomba ushauri maana hii ndo risasi yangu ya mwisho katika bunduki

Nimefanikiwa kupata mil 15 naomba ushauri maana hii ndo risasi yangu ya mwisho katika bunduki

timu moja daily weka double chance weka million hukosi 250k mpaka 300k per day, ..ndo kitu nafanya siku hizi najifungia ni mwendo wa kumtafuna muhindi mpaka mtaani washaanza kuni-doubt nasukuma sembe aka ERIC MANDALA ,.... nasisitiza usivuke zaidi ya timu moja utakuja nilaum.
 
Fungua duka la vipodozi,tafuta mrembo mwenye ngozi nzuri na ana idea ya vipodozi, utauza hadi uchanganyikiwe.
Tafadhali usiweke ndugu kwenye biashara yako tena changa utalia, pia usimamiz wa karibu sana untakiwa kwa biashara mpya la sivo utavuna mabua.
 
Wakuu.

Nipo DSM nimeuza Nyumba ya urithi na kupata mgao wa mil 15 .


Naomba ushauri nifanye Biashara gani yenye low risk .

Niliwaza hizi Biashara

Money transactions
Duka la vipodozi ambalo litakuwa na cheap products .


Duka matumizi ya Nyumbani .

Biashara zote hizi nimezitengea mtaji mil 10 na mfanyakazi atakuwa mdogo wangu ambaye namuani Ila Kwa sasa Anasoma Kemeboss Form four nategmea akimaliza shule ndo nimtumie in my hustle.

Ushauri guyz
Ipeleke hiyo hela UTT halafu ikopee bank, hapo utaweza pata around 12M kwenye mkopo, fanyia biashara unayotaka , biashara ikifaulu lipa mkopo umalizane na bank , biashara ikifeli , miaka 8 baadae utakuwa na 15M plus na interest utajiuliza upya tena
 
Leta 10ml tufungue genge la bei ya jumla dodoma utanishukuru baadae ,unauza vitu kutoka shambani unageuka soko dogo badala ya watu wote kwenda Sabasaba wanaishia kwako sija kulazimisha nime kupa wazo ambalo miezi miezi miwili ijayo naenda kulifanya

Pili fungua duka la electronics
Kuna jamaa hapa maili mbili kwa mudi kama kakopi idea yako vile. ...ila mkuu hyo business hakikisha una uhakika wa wateja coz jamaa japo anauza ila anavyotupa pia vng
 
Yaani mnalipa mamilioni ya Ada kemebos Ili uje umuajiri huyo mdogo wako kwenye tigo Pesa!
Wastage of resources!
Hamna mkuu huyu dogo amezaliwa 2010 na sasa yupo form four na sio kemebos tu primary kasomea Entebe na wajukuu wa Museven .

So dogo ana akili Sana za Biashara ndo maana nahitaji kuanza nae maana mpango uliopo akimaliza form four ataenda ulaya baadae matokeo yakitoka .
 
Biashara yoyote kati ya hizo ulizomention nashauri usiweke mtaji zaidi ya 5M.

Weka mtaji wa 5M uusimamie vizuri ndani ya miezi6 hadi mwaka, kama biashara itakufa utakuwa umepata uzoefu na umepoteza 5M nasio 10M. Endapo biashara itafanya vizuri utaiongezea mtaji kidogo kutoka kwenye akiba pamoja na faida uliyotengeneza.

Pesa unayobaki nayo itakuwezesha kunyanyuka Tena endapo utaanguka, lakini pia kukuezesha kujump in kwenye fursa nyingine zitakazojitokeza.
 
Biashara zipo nyingi,

Ila kitendo cha kuanza kumshirikisha mdogo wako ni dhahiri unaizika biashara kabla hujaianza.

1.ajili biashara yako waone BRELA.

2.Jenga ukaribu na TRA.usisubiri task force ndiyo ulipe.

3.Weka bidhaa zilizothibitishwa na TBS,

4.Tafuta mganga , sheikh,mchungaji,mzuri aizindike hiyo biashara
Namba nne irudie Tena 😂
 
Hamna mkuu huyu dogo amezaliwa 2010 na sasa yupo form four na sio kemebos tu primary kasomea Entebe na wajukuu wa Museven .

So dogo ana akili Sana za Biashara ndo maana nahitaji kuanza nae maana mpango uliopo akimaliza form four ataenda ulaya baadae matokeo yakitoka .
Mjukuu wa museven
 
Back
Top Bottom