Nimefanikiwa kupata mil 15 naomba ushauri maana hii ndo risasi yangu ya mwisho katika bunduki

Nimefanikiwa kupata mil 15 naomba ushauri maana hii ndo risasi yangu ya mwisho katika bunduki

Nunua mzani uwe unanunua chupa za plastic kwa wanaookota mtaani, utakuja kunishukuru
 
Angalia bishara itakayohitaji mtaji mdogo kwanza, uifanye upate uzoefu kisha utakua unakuza na pesa nyingine.

Kwa herufi kubwa SIMAMIA BIASHARA YAKO MWENYEWE!!! tena kwakua ndio inaanza kaa mwenyewe kama unajua hauna muda hiyo pesa kanywe tu mkuu.
Jirani za masiku?
 
Ipeleke hiyo hela UTT halafu ikopee bank, hapo utaweza pata around 12M kwenye mkopo, fanyia biashara unayotaka , biashara ikifaulu lipa mkopo umalizane na bank , biashara ikifeli , miaka 8 baadae utakuwa na 15M plus na interest utajiuliza upya tena
Mkuu hii ungefunguka zaidi, akishapata mkopo marejesho ataanza lini, coz kwa biashara mpya kuanza direct na mkopo, atakua kwenye pressure kubwa sana
 
Ukiwa na risasi ya mwisho kwenye bunduki ukiwa unataka kujimaliza usimparie jirani, au ndugu akumalize. Ni bora ujimalize mwenyewe ili ukijikosa utasave uhai wako na ukijioatia unakuwa umekufa kihalali...
 
Wakuu.

Nipo DSM nimeuza Nyumba ya urithi na kupata mgao wa mil 15 .

Naomba ushauri nifanye Biashara gani yenye low risk .

Niliwaza hizi Biashara

Money transactions
Duka la vipodozi ambalo litakuwa na cheap products .

Duka matumizi ya Nyumbani .

Biashara zote hizi nimezitengea mtaji mil 10 na mfanyakazi atakuwa mdogo wangu ambaye namuani Ila Kwa sasa Anasoma Kemeboss Form four nategmea akimaliza shule ndo nimtumie in my hustle.

Ushauri guyz
Nakuombea kwa Mungu upate utulivu na uelewa kwa kile ukiwazacho mbele yako na uweze kutoa maamuzi yaliyo bora na faida ktk maisha yako.
Pesa ina vishawishi vingi sana uwe mwangalifu isije kukugombanisha na ndugu yako. Mtumainie Mungu.
 
Wakuu.

Nipo DSM nimeuza Nyumba ya urithi na kupata mgao wa mil 15 .

Naomba ushauri nifanye Biashara gani yenye low risk .

Niliwaza hizi Biashara

Money transactions
Duka la vipodozi ambalo litakuwa na cheap products .

Duka matumizi ya Nyumbani .

Biashara zote hizi nimezitengea mtaji mil 10 na mfanyakazi atakuwa mdogo wangu ambaye namuani Ila Kwa sasa Anasoma Kemeboss Form four nategmea akimaliza shule ndo nimtumie in my hustle.

Ushauri guyz
Mpaka hapo umeishafell! Hela ya kuuza nyumba ya baaako aliyopambana kuijenga ndo utobolee hela yake? Nakushauri nunua kiwanja cha 4mil jenga kiband cha vyumba viwili pangisha kama tayari una nyumba. Hizo biashara sijui mpesa/vipodozi ni story za vijiweni na ni biashara ya wanawake wadangaji hamna kitu hapo
 
Dodoma sehemu gani unaweza kufanya hiyo kitu
Chamwino itafaa maana wote wa kuanzia nyuma ya chamwino ulazimika kwenda Saba saba
Kuna jamaa hapa maili mbili kwa mudi kama kakopi idea yako vile. ...ila mkuu hyo business hakikisha una uhakika wa wateja coz jamaa japo anauza ila anavyotupa pia vng
Issue ni kutafuta soko la watu wa uwakika wakujue na sio watu ndo wakutafute wewe au waambiwe Dodoma kuna shida sana ya Bidhaa za kupikia hasa mboga mboga ,fish etc
 
Mkuu kwanza lazima ujipongeze Kwa hatua uliyofikia.
-tafuta mrembo 1 au 2 jifungie nae hata week 2.
Huoni Azizi K anavyojipongeza Kwa mobeto?

Baada ya hapo sasa , utakuwa na akili na mawazo nn cha kufanya.

Kitendo cha kusikiliza mawazo ya Kila mtu hapa jukwaani utachanganyikiwa.
 
Wakuu.

Nipo DSM nimeuza Nyumba ya urithi na kupata mgao wa mil 15 .

Naomba ushauri nifanye Biashara gani yenye low risk .

Niliwaza hizi Biashara

Money transactions
Duka la vipodozi ambalo litakuwa na cheap products .

Duka matumizi ya Nyumbani .

Biashara zote hizi nimezitengea mtaji mil 10 na mfanyakazi atakuwa mdogo wangu ambaye namuani Ila Kwa sasa Anasoma Kemeboss Form four nategmea akimaliza shule ndo nimtumie in my hustle.

Ushauri guyz

Ushawahi kufanya biashara yeyote mkuu?
 
Ukubwa au udogo wa risk inaendana na taaluma pamoja na ujuzi wa kufanya biashara husika.

Kama hauna taaluma ya biashara hata kidogo tafuta mentor mwenye historia ya kufanya biashara iliyofanikiwa.

Taaluma yako ya biashara ni muhimu kuliko biashara yoyote. Anza hapo kwanza.
 
Hela ya urithi!!!? Inabidi ufanye sana maombi utoboe.
Ushauri wangu usifanye biashara usioioijua
 
Back
Top Bottom