Nimefanikiwa kupata mil 15 naomba ushauri maana hii ndo risasi yangu ya mwisho katika bunduki

timu moja daily weka double chance weka million hukosi 250k mpaka 300k per day, ..ndo kitu nafanya siku hizi najifungia ni mwendo wa kumtafuna muhindi mpaka mtaani washaanza kuni-doubt nasukuma sembe aka ERIC MANDALA ,.... nasisitiza usivuke zaidi ya timu moja utakuja nilaum.
 
Fungua duka la vipodozi,tafuta mrembo mwenye ngozi nzuri na ana idea ya vipodozi, utauza hadi uchanganyikiwe.
Tafadhali usiweke ndugu kwenye biashara yako tena changa utalia, pia usimamiz wa karibu sana untakiwa kwa biashara mpya la sivo utavuna mabua.
 
Ipeleke hiyo hela UTT halafu ikopee bank, hapo utaweza pata around 12M kwenye mkopo, fanyia biashara unayotaka , biashara ikifaulu lipa mkopo umalizane na bank , biashara ikifeli , miaka 8 baadae utakuwa na 15M plus na interest utajiuliza upya tena
 
Kuna jamaa hapa maili mbili kwa mudi kama kakopi idea yako vile. ...ila mkuu hyo business hakikisha una uhakika wa wateja coz jamaa japo anauza ila anavyotupa pia vng
 
Yaani mnalipa mamilioni ya Ada kemebos Ili uje umuajiri huyo mdogo wako kwenye tigo Pesa!
Wastage of resources!
Hamna mkuu huyu dogo amezaliwa 2010 na sasa yupo form four na sio kemebos tu primary kasomea Entebe na wajukuu wa Museven .

So dogo ana akili Sana za Biashara ndo maana nahitaji kuanza nae maana mpango uliopo akimaliza form four ataenda ulaya baadae matokeo yakitoka .
 
Biashara yoyote kati ya hizo ulizomention nashauri usiweke mtaji zaidi ya 5M.

Weka mtaji wa 5M uusimamie vizuri ndani ya miezi6 hadi mwaka, kama biashara itakufa utakuwa umepata uzoefu na umepoteza 5M nasio 10M. Endapo biashara itafanya vizuri utaiongezea mtaji kidogo kutoka kwenye akiba pamoja na faida uliyotengeneza.

Pesa unayobaki nayo itakuwezesha kunyanyuka Tena endapo utaanguka, lakini pia kukuezesha kujump in kwenye fursa nyingine zitakazojitokeza.
 
Namba nne irudie Tena 😂
 
Mjukuu wa museven
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…