Nimefanikiwa kupata mil 15 naomba ushauri maana hii ndo risasi yangu ya mwisho katika bunduki

2010 ni mdogo sana,atatapeliwa kirahisi
 
Nakushauri kanunue kibanda cha kuishi kama ujawahi kufanya biashara kabla..

Kama upo dar nenda chamazi, kibaha,chanika tafuta kibanda cha 13 au 14ml, iliyobaki ndio uchezee.

Huu ndio ushauri wa maana kulingana na maelezo yako.
1. Huna unauzoefu na biashara
2. Kumuajiri mdogo wako asimame biashara zako.

Nunua nyumba, inayobaki Fanya unachotaka
 
Usiajiri mtu kwa kuanzia, anza wewe ili uifanye ujue mtiririko wa mauzo na faida ipo vipi, baada ya mwaka sasa hapo ajiri mtu ukishaseti kila kitu mahali pake
 
Angalia bishara itakayohitaji mtaji mdogo kwanza, uifanye upate uzoefu kisha utakua unakuza na pesa nyingine.

Kwa herufi kubwa SIMAMIA BIASHARA YAKO MWENYEWE!!! tena kwakua ndio inaanza kaa mwenyewe kama unajua hauna muda hiyo pesa kanywe tu mkuu.
 
Anzisha biashara ya kununua na kuuza kuku mwanangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ