Nimefanikiwa kutoroka

Nimefanikiwa kutoroka

Mtakanuhu

Member
Joined
Sep 19, 2018
Posts
44
Reaction score
56
Kwetu hali ni mbaya sana ...
Kijana ukifikia miaka 15, unavishwa kakofia .. kofia hiyo inakusababishia matatizo makubwa sana. Huwezi kuuliza swali lolote .. na hata ukiuliza ukajibiwa huwezi kujua umejibiwa nini.
Ukishavishwa kofia unakuwa kama mtumwa wa fikra. Anachosema mmiliki wa kofia ndo hicho hicho. Akiamrisha kwenda kuwaua binadamu wenzio - wala huwezi kuhoji - ni kutekeleza amri tu.
Unajua nilifanikiwaje kutoroka huko kwetu ...
Alipatikana mtu mmoja ambaye alikuwa amevaa kofia ile kumbe ilikuwa ni kofia feki. Yeye alikuwa na uwezo wa kuhoji, na wenzake hawakumtambua kuwa kofia yake ilikuwa haifanyi kazi kama za wengine. Huyu ndo mkombozi wa wale ambao hawajavaa hizo kofia.
Kwetu .. sijajua itakuwaje baada ya miaka miwili kuanzia sasa.
Ebu nikanywe chai kwanza ila nikirudi nitawajuza zaidi kuhusu huko nilikotoka.
Nikaribisheni jamani ... naona hapa kuna uhuru wa kifikra.

1. Darasa lanne
2. Darasa la saba
3. Kidato cha nne
4. Kidato cha Sita
5. Chuo +
Hizi kofia zote hazijamkomboa kijana wa kwetu; anaendelea kuamini kuwa yuko huru wakati watu wake wakiangamia.
 
Kwa nini haukutoboa kofia ili umalize tatizo kwako na kwa wengine ambao hawakustaili kuivaa au kofia ilikuwa ya chuma mkuu.
 
Mkuu ipo siku utamaduni huu wa kofia utaisha tu nina imani hiyo na watu wataanza kuona ujinga uliofanywa na wazee wa ukoo katika maamuzi ya mila hizi potofu
Ipo siku ... hadi lin mkuu? wanaendelea kuwavisha makofia vijana na wanawake ...
 
Kwa nini haukutoboa kofia ili umalize tatizo kwako na kwa wengine ambao hawakustaili kuivaa au kofia ilikuwa ya chuma mkuu.
Wachache wanaofanikiwa kuitoboa lakini wanaendelea kuwa na vitu kama vilemba; hawatoki humo kwa sababu wana namba za kuwasaidia kuhudumiwa vizuri - ila mawazo yao hayafanyiwi kazi.
 
Kwetu hali ni mbaya sana ...
Kijana ukifikia miaka 15, unavishwa kakofia .. kofia hiyo inakusababishia matatizo makubwa sana. Huwezi kuuliza swali lolote .. na hata ukiuliza ukajibiwa huwezi kujua umejibiwa nini.
Ukishavishwa kofia unakuwa kama mtumwa wa fikra. Anachosema mmiliki wa kofia ndo hicho hicho. Akiamrisha kwenda kuwaua binadamu wenzio - wala huwezi kuhoji - ni kutekeleza amri tu.
Unajua nilifanikiwaje kutoroka huko kwetu ...
Alipatikana mtu mmoja ambaye alikuwa amevaa kofia ile kumbe ilikuwa ni kofia feki. Yeye alikuwa na uwezo wa kuhoji, na wenzake hawakumtambua kuwa kofia yake ilikuwa haifanyi kazi kama za wengine. Huyu ndo mkombozi wa wale ambao hawajavaa hizo kofia.
Kwetu .. sijajua itakuwaje baada ya miaka miwili kuanzia sasa.
Ebu nikanywe chai kwanza ila nikirudi nitawajuza zaidi kuhusu huko nilikotoka.
Nikaribisheni jamani ... naona hapa kuna uhuru wa kifikra.
Angalia usije ukawa umemkimbia mvesha kakofia....ukaangukia kwa mvua pikyu yako.... duniani tambara bovu ohoo...
 
Back
Top Bottom